Mahakama Kisutu yapiga stop mkutano wa Yanga wa Oktoba 23, 2016

Najiuliza hivi ni nani mwenye njaa kati ya wanaojikomba kwa Manji na wanaopinga utaratibu wa manji kuwekeza Yanga?
 
Naona uzi umeshambuliwa na mikia fc,mambo ya yanga hayajadiliwi kwenye vikao vya kahawa kila kitu ni kupitia mkutano na utafanyika tu.
 
aijengee Yanga uwanja ili iweje? umesikia wapi kuwa Barrick Gold / Acacia wanachimba dhahabu wanaiacha Tanzania? au gesi ya Mtwara inatolewa bure kuzalisha umeme wa Tanesco??
Ushawai ona timu inakodishwa duniani?
 
Subirini tu haya maandalizi watayalipa hao wanafiki wachache waliopeleka mahakamani.chaajabu kama kweli wanaipenda yanga kwanini waogope mkutano mkuu ?
Kule mkutanoni wapo watu wengi fuata upepo, ao m/kiti akisema hawaoji chochote wala kidadisi
 
Sina upande wowote ila mi hilo la kumilikiwa na mtu mmoja hiyo timu lilikuwa zuri ila tatizo ni staili anayotumia mkatakaba umejaa vipengele vya kuwakandamiza zaidi Yanga hata hiyo bodi ya wadhamini sijui hawakuliona hilo na hata ukisema eti mkaseme kwe mkutano pale utazomewa na watu walonunuliwa au kupewa posho ili wapitishe yaliyopangwa
Harafu hii kitu bana eti mkodishaji ndo huyohuyo mwenyekiti wa timu,sasa hapo watasaini vipi huo mkataba. Harafu mtu anataka kukodisha anaanza kukwambia nakudai sh bil.11 wakati huko mwanzo hakuwahi kusema kama kuna deni,kina Lloyd Chunga waliwahi ongoxa kwa shida bila hata hela hawakuacha hata nusu ya hilo deni wapo kina Madega wao walipoondoka waliacha bil.kadhaa kwe akaunti

Bado tuna safari ndefu sana na mpira wetu wa Tanzania....mi naona hakuna tofauti hata na miaka ya nyuma enzi za kina Sunday Kayun na kina Muhidin Ndolanga ni yale yale....nilipataga matumaini kweli mwaka 2004 wakati wanaenda kuibadili FAT kuwa TFF nikajua mambo mazuri yanakuja kumbe wapi
Timu inapima mafanikio kwa kuifunga Simba na Simba nayo inajipima mafanikio kwa kuifunga Yanga.....ujinga mtupu......ngoja nijandae nikaangalie EPL bora maana hapa hakuna tunachokitaka wala kukijua
 
Mbona hayo maombi hayana muhuri wa kupokelewa na mahakama
 
Subirini tu haya maandalizi watayalipa hao wanafiki wachache waliopeleka mahakamani.chaajabu kama kweli wanaipenda yanga kwanini waogope mkutano mkuu ?
Mmeshaongwa buku kumi na viroba ili wakija muwapige.Wao wameamua wawazuie kwa mbele.
 
Yanga hamtafika popote kwa kumtuka au kumkejeli mzee akilimali.Ninachoamini ni kua kuna wanayanga wengi sana walionyuma ya huyu mzee.Bila kukaa chini na kumaliza tofauti kwa amani na busara yanga yenye migogoro inanukia.
Akae chini na nani huyo msaliti
 
Kweli mkuu angejitoa basi u mwenyekiti halafu wengine ndio wafanye mchakato. sio kila kitu anasimamia yeye tena kwa mikutano ya dharura. mi ni Simba ila kwa hili unaona kabisa watani wanaamua kwa kukurupuka.
We ni simba ? Mkia upo wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…