Kuna maneno na mazungumzo mengi na marefu juu ya kurudishwa mahakama ya Kadhi. Na kila linapozungumzwa jambo hilo linafananishwa na dini za kikristo.
Kwa wale tunaojua historia ya mahakama ya kadhi, tunajua kwamba ziliidhinishwa hapa nchini na utawala wa Waingreza pale walipoweka mfumo wa utawala usio wa moja kwa moja kama ulivyokuwa kwa Wajerumani.
Utawala usio wa moja kwa moja uliwatumia Waafrika waliokubaliwa na wenyeji kama wakala wa Waingreza katika kutawala mambo fulani fulani; kama kusuluhisha baadhi ya migogoro ya wenyeji, kusimamia utozaji wa kodi nk.
Utaratibu huu ulifuata sheria na mila za mahali husika kama vile kwa watu wa Kilimanjaro, wa Mbeya nk. Katika mikoa ya pwani, toka Mtwara hadi Tanga, ilionekana hawakuwa na mfumo wa kijadi unaoleweka kwa wengi.
Watu wa sehemu hizi walikuwa na makundi mengi yenye tamaduni na mila nyingi kiasi kwamba ilikuwa vigumu kupata mfumo mmoja wa kienyeji wa kutawala.
Ndiyo maana hawa wakapewa mfumo wa kiislamu, dini ambayo ilikuwa imestawi sehemu hizo. Mikoa au sehemu nyingine za Tanganyika zilitumia mifumo ya sheria za Kienyeji au mila zao.
Baada ya uhuru, uongozi wa wakati ule uliona ni muhimu kujenga taifa, ambalo halikuwepo; kwani Tanganyika ilikuwa ni kipande cha ardhi, alichojimegea Mwingreza kwa faida yake.
Watu walioishi kwenye kipande hiki cha ardhi hawakuwa na kitu cha kuwatambulisha; maana yake hawakuwa na mila, utambulisho wala tamaduni zinazofanana. Nia ya uhuru ilikuwa kujenga kitu kipya ambacho hakikuwepo, na sasa bado hakijakuwepo sawasawa.
Ili kufanikisha adhma ya kujenga taifa jipya, viongozi hao, waliamua baadhi ya mifumo ya utawala iwe ya kitaifa na siyo ya kikabila wala ya kidini. Kwanza walifuta utawala wa kijadi wa Watemi.
Pili wakafuta sheria zote za kijadi kama zile za Wanyakyusa, Wahaya, Wanyaturu na kwa upande wa pwani, sheria za kiislamu.
Inawezekana waasisi wa taifa letu walifanya makosa wakaondoa mambo yetu matakatifu. Basi,TUNAPOTETEA MAHAKAMA YA KADHI, NA TUTETEE MAHAKAMA ZA KIJADI. Kwa nini tunaona yale yaliyoletwa na wageni, Waarabu na Wazungu ni bora zaidi kuliko ya kwetu? Hivi kweli huu mjadala ni wa kujenga Uafrika wetu au ni wa kuzidi kutughaibunisha? Ni tafakari tunduizi!