Mahabusu ajisaidia kizimbani, atishia kumwaga kinyesi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahabusu ajisaidia kizimbani, atishia kumwaga kinyesi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 7, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  VITUKO vya mahabusu kufanyika kwenye Mahakama mbalimbali zimezidi kuendelea kujitokeza, ambapo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Morogoro, mmoja wa watuhukiwa wa kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Baven Hamisi (25) juzi alijisaidia haja kubwa na kutishia kuwamwagia kinyesi polisi, mashahidi na mwendesha mashitaka wa kesi hiyo.

  Tukio hilo lilitokea juzi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimumkazi mkoani, Jafari Mzonge na hivyo kulazimika kuahirisha kesi hiyo ya unyang’anyi wa kutumia silaha iliyokuwa ikiwakabili washitakiwa wanne akiwemo na aliyetishia kuwamwagia kinyesi.

  Hata hivyo, mshitakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Msamvu katika Manispaa ya Morogoro, baada ya kufanya kituko hicho, Hakimu Mzonge alimhukumu kwenda jela miezi sita kwa kitendo chake cha kuidharau Mahakama.

  Kituko hicho alichokifanya ni miongoni mwa vituko vingine ambavyo aliwahi kuvifanya mara baada ya kesi hiyo kufika katika hatua ya kusikilizwa ambapo awali alishawahi kuvua nguo na kuvaa mifuko ya plastiki, kujipaka tope na kuongea vitu visivyoeleweka hali iliyomfanya hakimu huyo adhani kuwa ni mgonjwa wa akili.

  Katika siku ya tukio hilo, mshitakiwa alifikishwa mahakamani hapo akiwa na wenzake ambapo kesi hiyo ilikuwa kwenye hatua ya kusikilizwa na kwamba shahidi wa kwanza wa upande wa mashitaka alikuwa tayari kutoa ushahidi wake.

  Hata hivyo, bila ajizi, ndipo mshitakiwa huyo alipoanza kuvua nguo na kujisaidia haja kubwa na kutishia kurusha kinyesi hicho kwa yeyote atakayemshika.

  Mbali na Hakimu huyo kutoa adhabu kutokana na mshitakiwa huyo kuidharau mahakama, lakini pia aliamuru mshitakiwa huyo kupimwa akili ili kubaini afya ya akili yake japokuwa ndugu pamoja na washitakiwa wenzake wanadai kuwa ni mzima na amekuwa akifanya
  shughuli zake kama kawaida akiwa gerezani.

  Kesi ya msingi inayomkabili mshitakiwa huyo ni ya unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo inadaiwa kuwa yeye na wenzake walitenda kosa hilo Oktoba 25 mwaka jana majira ya saa 5:30 usiku barabara ya stesheni ambapo wakiwa na visu walipora pikipiki aina ya San LG namba za usajili T998 BJH yenye thamani ya sh milioni 1.7 iliyokuwa ikiendeshwa na Omar Hashim.

  Baada ya kesi hiyo kuhairishwa itarudi tena Januari 14, mwaka huu katika mahakama hiyo na itakuwa katika hatua ya kusikilizwa.
   
Loading...