Magunia 64 ya bangi yakamatwa bila watuhumiwa

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18
</SPAN>




Tuesday, November 10, 2009 10:51 AM
MAGUNIA 64 yaliyokuwa na kilo zaidi ya 100 katika kila gunia ya mmea haramu wa bangi yamekamatwa Wilayani Arumeru bila ya wahusika.


Magunia hayo yalikamatwa katika operesheni ya Jeshi la Polisi Mkoani Arusha ya kukamata dawa za kulevya aina ya bangi wilayani Arumeru.


Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo mkoani humo ambaye pia ni Mkuu wa upelelezi mkoani humo, Bw. Leonard Paul alisema bangi hiyo ilikamatwa katika vijiji viwili tofauti vya Kisimiri Juu na Lesenoni wilayani Arumeru.


Alisema operesheni hiyo ilianza juzi majira ya saa 7:00 mchana na kumalizika saa 2:30 usiku wa kuamkia jana ambapo jeshi hilo lilikamata magunia hayo yaliyokuwa yamehifadhiwa katika nyumba za watu mbalimbali vijijini humo.


Kaimu Kamanda huyo alibainisha kwamba magunia hayo ya bangi yalikuwa mbioni kusafirishwa kuelekea katika nchi za jirani na kusema katika operesheni hiyo jeshi hilo
halikufanikiwa kumkamata mhusika yoyote katika tukio hilo kwa kuwa wakazi wengi wameyakimbia makazi yao.


Hata hivyo, alisema kwa sasa bangi hiyo imehifadhiwa katika chumba maalumu katika kituo kikuu cha polisi kati ikisubiri kuteketezwa huku mkakati uliopo sasa ukiwa kuwatafuta wahusika wake.



Na Emmanuel Sanjo, Arusha
 
Hata hivyo, alisema kwa sasa bangi hiyo imehifadhiwa katika chumba maalumu katika kituo kikuu cha polisi kati ikisubiri kuteketezwa huku mkakati uliopo sasa ukiwa kuwatafuta wahusika wake.

hivi wanaoteketeza bange hufanya kwa uaminifu au wanadokoa na kuiuza nyingine?
 
Back
Top Bottom