Magunia 428 ya bangi yakamatwa Arusha

Magunia 428 ya bangi yakamatwa Arusha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611

pic+bangi.jpg
​

Arusha. Shehena ya magunia 428 ya dawa za kulevya aina ya bangi imekamatwa katika kitongoji cha Longong, Kijiji cha Engalaoni wilayani Arumeru usiku wa kuamkia jana.

Akizungumza leo Jumanne, Julai 18 wakati wa operesheni hiyo maalum ya kufanya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba kwenye kitongoji hicho, Kamishina wa Intelijensia wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Fredrick Kibute, amesema wamefanikiwa kukamata dawa hizo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi.

Amesema walituma kikosi kazi cha watu wachache kuchunguza uwepo wa taarifa hizo.

“Baada ya kujiridhisha na taarifa hizo, tulianza safari kutoka Dar es salaam na juzi usiku wa manane tulianza upekuzi na kukamata magunia hayo 428,"amesema Kamishna huyo.

Amesema walikamata magunia 428 ya bangi usiku huo na magunia sita ya mbegu za bangi ambazo zilikuwa zimefichwa ndani.

"Lilikuwa jambo la kushangaza usiku huo hatukukuta watu ndani ya nyumba ingawa zilikuwa wazi, baadhi ya nyumba zilikuwa zimefungwa, zilizofungwa tuliamua kuchukua uamuzi wa kuvunja na tulikuta kila nyumba ina bangi," amesema.

Kamishna Kibute amesema pia licha ya eneo hilo kuwa mbali limesababisha viongozi wengi kushindwa kufika maeneo hayo kwa ajili ya ukaguzi.

"Huku ni mbali hasa ukiangalia ni eneo wanaloishi watu wachache, kikubwa tunaomba ushirikiano zaidi kutoka kwa wananchi juu ya uwepo wa madawa hayo kwenye maeneo hayo," amesema.

Kamishna Kibute aliwataka wananchi wa wilaya ya Arumeru kuacha mara moja biashara ya kilimo cha bangi kwa kuwa serikali ya awamu ya tano si mchezo na kuwataka watambue kuwa hawapo salama na atahakikisha anakomesha kilimo haramu cha biashara ya dawa za kulevya.


Chanzo: Mwananchi
 
Jamani hii bangi ni dili kwenye lile jimbo la marekani,nasikia imeadimika mno! kwanini tusiwauzie kama sie hatutumii hahah
 
Wasiharibu, zao zuri sana la kibiashara tatizo unafiki ndo unatuponza.
 
Dah! Ndo maana ganja linapanda bei Kila uchao.
 
Sasa wale jamaa wanao fugwa watapata wapi kilimo kikisitishwa? Hao ndio watumiaji namba moja wa bangi
 
Huu mmea hata sijui huwa una nini..... Operations kibao lakini hauishi kulimwa!!!!!
 
Nimesikitika na kulia ka mtoto mdogo kuona watu wangu wanakosa maarifa na kukamata bangi. Bila aibu wanatumia muda wao kusaka na kukamata bangi. Tumelaaniwa na kamwe hatutaendelea tusipobadilika.

Legalise It
 
Nimesikitika na kulia ka mtoto mdogo kuona watu wangu wanakosa maarifa na kukamata bangi. Bila aibu wanatumia muda wao kusaka na kukamata bangi. Tumelaaniwa na kamwe hatutaendelea tusipobadilika.

Legalise It
Mkuu mimi mwenyewe nimelaani kweli kweli kwanini wakamate bangi ? Bangi ina heshima yake please free marijuana. Nilivyoiona nishaitama tena ukizingatia kanuni ya demand and supply kwa huku.
 
Badala wahangaike na mauaji ya KIBITI wanahangaika na Dawa.Ujinga kabisa huu majambazi kila kona wanawashindwa wanatoka Dar kwenda kukamata Bange R?
 
Back
Top Bottom