Magunia 1000 ya dawa za kulevya yateketezwa

Magunia 1000 ya dawa za kulevya yateketezwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Magunia zaidi ya 1000 ya dawa za kulevya aina ya bangi yamekamatwa na kuteketezwa na Jeshi la polisi wilayani Arumeru kwa muda wa miezi mitatu huku watuhumiwa 37 wakiwa wamekamatwa na 12 wamefikishwa mahakamani.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arumeru, SP Jumanne Mkwama, amesema hatua za kisheria zinafuata kwa watuhumiwa wote na kuitaka jamii kutoa ushirikiano kudhibiti dawa hizo ambazo zimekuwa na madhara kwa taifa.

"Kinachofuata hapa ni watuhumiwa wote kufikishwa mahakamani pamoja hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao. lakini naomba niwatake viongozi waliopo ngazi za chini wakumbuke wanapaswa kutoa taarifa hizi mapema kwa jeshi la polisi pamoja na wananchi msiliachiie jeshi kazi au mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya kwani hili ni jukumu letu sote" SP Nkwama

Akizungumza na Wanahabari Kamishina wa Intelijensia wa tume ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Fredy Kibuta amesema katika msako ulioendeshwa na Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na kikosi maalumu cha jeshi la polisi Watu 14 wakiwemo wanawake sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Arumeru kwa tuhuma za kukutwa na bangi katika nyumba zao.

Ameongeza kuwa msako huo umefanyika katika vijiji vya Losinoni juu, Losinoni Kati pamoja na Engalaoni, ambapo zaidi ya magunia 400 ya bangi yamekamatwa pamoja na pikipiki nne ambazo zinasadikika kutumika kusafirisha dawa hizo.


EATV
 
Back
Top Bottom