Magufuli: Walioanguka kura za maoni kuula

Magufuli: Walioanguka kura za maoni kuula

mkafrend

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Posts
3,045
Reaction score
1,503
Mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, akihutubia mkutano wa kampeni mjini Tunduma mkoa wa Songwe jana. PICHA: ADAM MZEE
Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amewapooza wagombea wa chama hicho waliodondoshwa kwenye kura za maoni kwa kuwaahidi atawapa ajira hivyo kuwataka wasikikimbie chama hicho.

Hali kadhalika, Dk. Magufuli amewataka wana-CCM hao kutoendeleza makundi kwa kuwa yatahatarisha ushindi wa chama hicho. Aidha, amewaombea msamaha wagombea wa Majimbo ya Sumbawanga Mjini, Kwela, Kalambo mkoani Rukwa na Momba mkoani Sogwe.

"Nawaomba muwasamehe saba mara sabini kwa kuwa hawachagui malaika bali binadamu ambaye siyo mkamilifu," alisema Dk. Magufuli.

Alisema yawezekana yapo ambayo hawakuyatekeleza kama inavyotakiwa na makosa mengine ambayo yamekuwa kinyume na matarajio ya wananchi, lakini anawahitaji afanye nao kazi na ahadi zote watakazoahidi watazitekeleza kwa maendeleo endelevu ya wananchi.

ATAKA MAKUNDI YAVUNJWE
Akiwa Jimbo la Kwela ambalo mgombea wake ni Ignus Malocha, alisema kura za maoni zimeisha na kinachotakiwa ni kuvunja makundi na kufanya kazi ya kuipa ushindi CCM.

"Inawezekana mbunge wenu hakufanya hadi mlipotarajia, namuombea msamaha kweli kweli, nipeni, huyu ni binadamu hatuchagui malaika, mchagueni Malocha msihadaishwe na maneno mengi," alisisitiza.

Akiwa Jimbo Kalambo ambalo mgombea wake ni Josephat Kandege, alisema waliobwagwa kura za maoni hawapaswi kulalamika na kuacha kuunga mkono mgombea aliyepita, kwani akiwa rais nafasi za kazi zitakuwa nyingi kila mmoja atapata.

"Nakwenda kuwa rais, nafasi za kazi ni nyingi sana. Mligombea kwa kuwa mnataka kufanya kazi, nitawapa kazi, lakini hakikisheni huyu anashinda," alisema.

Katika Jimbo la Momba ambalo mgombea wake ni Dk. Lucas Siyame, alirejea ombi la msamaha kwa wananchi hao kwa kuwa mgombea huyo alihimiza ujenzi wa barabara ya Sumbawanga hadi Tunduma, lakini kwa sababu ambazo hazieleweki walimuangusha.

"Tunaambiwa tusamehe saba mara sabini, kama kuna dhambi aliifanya msameheni na ikifika Oktoba 25, mmpe kura za ndiyo," alisema.

Alisema wagombea wengine wasiwe na shaka kwani serikali ya awamu ya tano itakuwa na nafasi nyingi za wachapakazi na waadilifu na kutokana na nia yao ya kutumikia watu, hawatakosa nafasi hizo.

"Licha ya jitihada za wakati huo, lakini mkampiga chini, ila namuombea msahama, mrudisheni wakati huu nifanye naye kazi, tunahitaji maendeleo bora kwa wote na hayo yataletwa na mafiga matatu kwa maana ya diwani, mbunge na rais," alisema.

Dk. Magufuli alisema kufanya kosa siyo kosa bali kosa kurudia kosa.

Akiwa Jimbo la Sumbawanga Mjini ambalo mgombea wake ni Aeshi Hilary, pia aliwaomba wananchi wafute makosa na kuanza upya kwa kumpa kura za ushindi.

Akiwa Jimbo la Mpanda Mjini, alitoa ahadi ya kazi kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kipindi kilichopita kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Said Arfi, na kuangushwa kwenye kura za maoni za CCM, huku akisema alikokuwa alikuwa amekosea njia.

"Kazi zipo nyingi nitakuwa rais wa nchi hii, kazi zipo nyingi wala usiwe na shaka, sitakosa nafasi ya kukupa, najua uwezo wako katika kazi," alisistiza.

Akihutubia wananchi wa eneo la Nzokala, Lusaka na Laela, alisema katika mchakato wa kumsaka mgombea urais wa CCM walikiwa 38, lakini alichaguliwa kupeperusha bendera ya chama hicho lakini wamevunja makundi na kumuunga mkono.

Aliagiza wagombea hao kupeleka orodha ya wagombea wote wa kura za maoni kwenye majimbo yao kwa ajili ya kuwapatia kazi baada ya kuingia Ikulu.

Aidha, alisema ahadi zote anazotoa atatekeleza na kwamba kubwa kwake ni utekelezaji wa huduma za jamii kama ujenzi wa zahanati vijiji vyote, vituo vya afya kwenye kata, hospitali wilayani na hospitali za rufaa mikoani na kuhakikisha dawa zinakuwapo na siyo maduka binafsi kuwa na dawa na maeneo ya umma kukosa dawa.

Alisema atahakikisha huduma ya umeme, majisafi na salama vinapatikana kwas kuwa kama aliweza katika ujenzi wa barabara, hivyo mengine hatashindwa.
 
Ni uwanja wa fikra pevu si vzr kutoa lugha ya matusi jamini
 
Kwa hiyo ukuu wa wilaya na mkoa watagawiwa waliokataliwa na wananchi..
Ccm imetuchoka kweli
 
ahadi kwa ccm haina maslai cha muhimu kwa ccm ni kutangaza yale yote waliyoyafanya hata kama ni machache watu watayapima lakini kuaidi ahadi nyingine ni kupotea njia namuomba Makufuli kwenye mikutano yake awe anasema tumefanya hili na hile tumeshindwa kulifanya kwa nini basi,asiingie kwenye mtego wa ahadi, ahadi awaachie vyama pinzani maana vyenyewe havijapata na fasi ya kutimiza ahadi zao, huo ndio ushauri wetu sisi kina gogo la shamba maana ndio kazi yetu kutoa ushauri
 
Mafuriko yamemfika magufuli kwenye utosi.
CCM wanaondoka kwa kuwa hakuna namna nyingine tena.
 
Sasa si ndiyo yale yale ya JK kuendekeza ushikaji, tulishasema ccm haiwezi kujibadili, suluhisho ni moja tu "PIGA CHINI CCM"
 
ahadi kwa ccm haina maslai cha muhimu kwa ccm ni kutangaza yale yote waliyoyafanya hata kama ni machache watu watayapima lakini kuaidi ahadi nyingine ni kupotea njia namuomba Makufuli kwenye mikutano yake awe anasema tumefanya hili na hile tumeshindwa kulifanya kwa nini basi,asiingie kwenye mtego wa ahadi, ahadi awaachie vyama pinzani maana vyenyewe havijapata na fasi ya kutimiza ahadi zao, huo ndio ushauri wetu sisi kina gogo la shamba maana ndio kazi yetu kutoa ushauri
Ahadi za magufuli ni aina fulani ya rushwa
 
Kwa hiyo wanapeana nafasi sio,mi nilidhani tunachagua wa kutuongoza kumbe ni kutengeneza nafasi.Kura yangu hapati
 
ahadi kwa ccm haina maslai cha muhimu kwa ccm ni kutangaza yale yote waliyoyafanya hata kama ni machache watu watayapima lakini kuaidi ahadi nyingine ni kupotea njia namuomba Makufuli kwenye mikutano yake awe anasema tumefanya hili na hile tumeshindwa kulifanya kwa nini basi,asiingie kwenye mtego wa ahadi, ahadi awaachie vyama pinzani maana vyenyewe havijapata na fasi ya kutimiza ahadi zao, huo ndio ushauri wetu sisi kina gogo la shamba maana ndio kazi yetu kutoa ushauri

Kwanini aseme tumefanya hivi kwani amewahi kua rais? Wizara alizowahi kuongoza anasema kabisa kwamba nimefanya hivi hata yeye bila kusema kazi zake zinaonekana.
 
Eeeeehhh...ooohh....nooo... nooo 🚶🚶🚶👐👐👐

Hivyo atawa kazi wafuatao...!!

1: Ngeleja...

2: Prof. Muhongo..

3: Mama Tibaijuka

4: Membe

5: Migiro..

6: Pinda

7: Bilal

8: Balozi Amina

9: Sitta

10: Prof. Mwandosya

11: Yule mkulima wa Kigoma

13: Kolakola

14: Wale wote wazembe walio anguka kura za maoni ATAWAPA KAZI.. hiyo ndio SERIKALI YA MAGUFULI... huu utani kabisa


etc etc etc....

Hivi hakuna wa kumshauri MAGUFULI...

Is he OK..!? anaongea nn huyu...!!?

Anyway... sbb CCM ndio mwisho wake acha aongee madudu tu....!!!
 
hahah! Hizo Kazi, Ni Kazi Gan Kwani?....Naona Anasema Kazi Zitakuwa Nyingi Tu!
 
Duniani kote wanaokuunga mkono ndiyo wanaopewa kazi. Hata CHADEMA wakishinda hawatawapa kazi walioko upande wa pili CCM. Magufuli anajaribu kutibu majeraha ya kura za maoni. Walioshindwa wanaona kama vile hakuna maisha baada ya hapo. Kauli imechelewa mno ilipaswa itolewe na Mkwere (M/KITI wa CCM) mara baada ya mkutano mkuu wa chama pale Dodoma. Magufuli naanza kumpa credit za nyongeza. Watu (wapumbavu na malofa) kama akina Sumayi wasingeondoka iwapo maneno kama haya yangesemwa mapema. Maneno ya kusema waliokatwa ni makapi yamezidisha machungu kwa waliokatwa, yameleta utengano zaidi, yalileta dharau. Sasa Magufuli anafuta kauli kama hizo ili kukijenga chama. Chama ni watu siyo ubabe, siasa ni maneno matamu (rhetoric words) yanayowavuta watu karibu siyo ujeuri na ubabe unaowaogofya watu na kuwakimbiza mbali. Big Up Magu!
Ahadi za magufuli ni aina fulani ya rushwa
 
Back
Top Bottom