Magufuli Vs Kikwete - Magufuli na Tahadhari

Magufuli Vs Kikwete - Magufuli na Tahadhari

SamTu160, post: 15943674, member: 354763"]Huu ujinga jiaminishe mwenyewe.... Ajira za boda boda?
Fly over JK hausik kabisa, jiwe la msingi limewekwa na nani?[/QUOTE]
Kuweka jiwe la msingi c tatizo je mchakato Wa huo ufadhili umeanza lini je uchambuzi yakinifu mpaka kufikia hatua ya kuweka je you think is something of overnight think big don't take things for granted mwishowe utasema utasema daraja la Kigamboni ni la yule aliyelizindua tunajua mnataman iwe hi yo lkn haiwezekana ni saw a na kusema uwanja Wa taifa ulijengwa na jk simply aliuzindua fikirisha akili yako
 
ila mnapomsifia kikwete a ngalieni hayo maendeleo aliyoyafanya kafanya kwa cost ipi? maana kikwete amelipaisha sana deni la taifa, Magufuli akikopa mihela yoote hiyo iliyokopwa awamu ya kikwete unadhani ataleta maendeleo kiasi gani?

hapa kuna fact moja tu, Kikwete alikuwa hana control na hii nchi, hii ilikuwa na faida zake kama uhuru wa habari, upinzani kukua, biashara nyingi kuchipua lakini hasara zake ni nyingi mno kama vile kukopa fedha nyiingi kwa maendeleo yasiyoendana, biashara na fedha haramu kuwepo nyingi mtaani hadi magufuli anaonekana anafanya maisha kuwa magumu zaidi anapijaribu kusafisha
 
v) Uwanja mpya wa kimataifa wa ndege JNIA terminal 3 ni mzuri kuliko hata amsterdam
vi) BOT twin tower
Vii) Meli/boti Mv Dar es salaam
viii) Lami kutoka Ntwara mpaka Kigoma...
ix) Kiwanda cha cement Ntwara
x) Kiwanda cha viuatilifu vya kuteketeza Mbu Kibaha...
xi) Vyandarua Bure nchi nzima na kutuhimiza kuweka kabla ya kulala kila saa 3 usiku
Xi) Shule za sekondari WAMA Ntwara
xii) kubwa kuliko yote... Uhuru wa habari, mitandao ya kijamiii huru....,

NACHELEA KUSEMA HATATOKEA RAISI KAMA KIKWETE........,


Watokwa mapovu karibuni....
  • BOT Twin towers ilijengwa kuanzia mwaka 2001/2006 - Kikwete anakujaje hapo
  • Lami- nchi nzima ni fedha za MCC na wafadhili, JK anatoka wapi
  • Cement- ni mwekezaji DANGOTE, - JK anatoka wapi
  • Vyandarua bure - Msaada wa Watu wa Marekani (USAID) - JK anatoka wapi hapo
  • Sekondari WAMA, fedha za wafadhili kutoka Uholanzi, chini ya Taasisi ya Mama Salma - JK anatoka wapo hapo
Usiwe na mahaba niue, pasipo kuwa na evidence na uyasemayo!
 
Thread kama hii ndiyo iliyoletea rais kuitwa "bwege".
 
Ukitaka kujua mazuri ya JK mbona ni mengi sana tu

1. Kuwezesha wanawake
2. ARV kwa wagonjwa wa Ukimwi
3. Uhuru wa habari (TBC bungengeni kwa miaka 10)
4. Kuongezeka udahili wa wanafunzi vyuo vikuu
5. Kusaidia wasanii kwa kuwatungia sheria ya hati miliki , pamoja na kujenga Kituo cha kulelea vipaji cha Kikwete Academy
6. Kuboresha mishahara ya Wafanyakazi kila baada ya muda fulani
8. Kuvuta maji kutoka Ruvu chini, mabomba yameshatandikwa, Shida ya Maji Dar itakuwa Historia
9. Kuongezeka ukusanyaji wa mapato kutoka bilioni 177 mwaka 1995 mpaka bilioni 900 mwaka 2015
10. Kuanzisha mfuko wa Utafiti
11. Kuanzisha mfuko wa mbegu za kilimo badala yakutegemea mbegu kutoka nje
12. Barabara za magari yaendayo kasi
13. Madaraja makubwa kwa madogo
14. Barabara za lami nchi nzima
15. Shule za kata
16. Vyuo vikuu mfano UDOM, Nelson Mandela
17. Microeconomy iliwezeshwa , mfano MPESA, TIGOPESA, VIKOBA
18. Kutandaza Mkongo wa Taifa
19. Uchumi wa Gesi
20. Mchakato wa Bandari ya Bagamoyo itakayofanya kazi in parallel na bandari ya Dar, huku ya Tanga ikihandle mambo ya mafuta
21. Umeme hadi vijijini
22. Demokrasia pana, Viongozi wa Upinzani mara nyingi walikutana na JK Ikulu kuweka mambo sawa
23. Transparency, kwa kuruhusu Ripoti ya CAG iwe inajadiliwa bungeni, zamani kabla ya hapo ripoti hizo zilikuwa zikiishia kwa raisi
24. Diplomasia ya hali ya juu, tumesuluhisha madagaska, tumeisaidia comorro kumuondoa muasi kanali Bacar, Tumemrudisha Nkurunzinza madarakani, Tumewaondoa wahamiaji haramu wa kinyarwanda, Tumesuluhisha Kenya, Tumesuluhisha South Sudan
25. Kaiacha nchi katika mikono salama

Acheni Masikhara nyinyi JK ni miongoni mwa Viongozi bora kabisa kupata kutokea katika nchi hii, Subirini Hangover ya Kupata mtawala mpya iwaishie then mkirudi katika sober state mtaona kuwa JK was a Leader!



Ningeweza kukupa like mara 100 ningefanya hivyo mdau.... waache watokwa mapovu waishi na husda zao JK jembe, kafanya ya maana sana hapa Tz.
 
  • BOT Twin towers ilijengwa kuanzia mwaka 2001/2006 - Kikwete anakujaje hapo
  • Lami- nchi nzima ni fedha za MCC na wafadhili, JK anatoka wapi
  • Cement- ni mwekezaji DANGOTE, - JK anatoka wapi
  • Vyandarua bure - Msaada wa Watu wa Marekani (USAID) - JK anatoka wapi hapo
  • Sekondari WAMA, fedha za wafadhili kutoka Uholanzi, chini ya Taasisi ya Mama Salma - JK anatoka wapo hapo
Usiwe na mahaba niue, pasipo kuwa na evidence na uyasemayo!


Hao wafadhili uliwaleta wewe? Kwani mi nimesema katumia pesa zake mfukoni? acha kujiabisha
 
Mbona hii system ya JF inapunguza ukubwa wa kusoma quote, we unatumia technolojia gani?
natumia app ya jf kwenye simu nikiwa sipo ofisini, na sio mimi tu kuna wadau kibao pia wanatumia app
 
Back
Top Bottom