Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Ni jambo la kawaida sana mara kwa binadamu kuifikiria kesho itakuwa nzuri zaidi kuliko ilivyo leo. Ndiyo maana tuna misemo kama:
Usiache mbachao kwa msala upitao
Kipya kinyemi japo kidonda
Baniani mbaya kiatu chake dawa
Usidharau wakunga na uzazi ungalipo, n.k.
Watanzania wana matumaini makubwa sana kutoka kwa Rais Magufuli, wakiamini kuwa mtangulizi wake hakufanya kitu na alilididimiza Taifa kwenye umaskini, uzorotaji wa huduma za afya, ufisadi na uzembe, na ukosefu wa uadilifu katika utumishi wa umma.
Naye Kikwete alipoingia madarakani, watu wengi walimwona angefanya miujiza na kuifanya Tanzania kuwa nchi tajiri, yenye watu wenye maisha mazuri, chini ya kauli mbiu zake:
Maisha bora kwa wote yanawezekana
Nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya
Akatuahidi kuifanya Kigoma kuwa Dubai, uwanja wa ndege wa kisasa huko Kagera, Meli ya kisasa ziwa Viktoria, na mengine mengi.
Leo tunaye Ngosha wetu, chini ya kauli ya Hapa Kazi tu. Ametuahidi Tanzania kujitegemea na kugeuka badala ya kuwa mpokea misaada mkuu na kuwa, 'donor country'.
Tahadhari kubwa ambayo Magufuli anatakiwa kuichukua, aangalie asije akafanya pungufu kuliko tunayemdharau kuwa hakufanya kitu.
Mh. Jakaya Kikwete huko uliko upate mapumziko mema, na mahali ulipowatendea Watanzania kwa dhamira njema na safi, upendo na kwa uadilifu, Mungu akubariki. Pale ulipofanya makosa kwa bahati mbaya, Mungu akusamehe. Pale ulipofanya makosa kwa makusudi, usikose kutubu wakati Mola wako bado amekupa muda.
Kuna wakati nami nilimlaumu Kikwete, lakini tuendavyo nina mashaka kama kweli tumekuwa bora zaidi sasa kuliko tulivyokuwa. Kikwete pamoja na mapungufu yake maana tulimuita ombaomba lakini ameacha alama kwenye Taifa lake:
Rais Magufuli afahamu kuwa mwananchi wa kawaida haangalii kama amepatiwa matibabu kutoka kwenye hospitali iliyojenga kwa msaada au kwa kujitegemea, haangalii kama wateja kwenye biashara yake ya chakula wanatumia hela waliyoipata kiuhalali au wameifanyia ufisadi serikali, haangalii kama ameajiriwa na kampuni ambayo mmiliki wake ni muadilifu au alifisadi hela ya umma. Unaweza kutumbua majipu mengi sana lakini kama mwananchi wa kawaida zamani katika kuhangaika kwake alikuwa anapata shilingi 5,000 sasa hapati hata 1,000, kwake itakuwa vigumu sana kuamini kuwa uongozi wa sasa ni bora kuliko wa zamani.
Kwa sasa watu wadogo huko mitaani maisha yao ni magumu sana. Tunawaambia wafunge mikanda lakini hawa hata sehemu ya kufungia mikanda hawana. Wengi waliokuwa wanajenga wamesimama, waliokuwa wanauza matofali hayanunuliwi, kwa sababu matofali hayanunuliwi, cement nayo madukani inadoda, mafundi ujenzi wadogo wadogo hawapati kazi za ujenzi, akina mama nitlie waliokuwa wanashinda kwenye ujenzi kuwauzia chakula vibarua, hawana kazi pia, n.k.
Kwa upande wa serikali ya Magufuli, kwa sasa ni karibia nusu mwaka unaisha. Nini kikubwa kilichofanyika? Wengi watasema kutumbua majipu, ambayo kimsingi lengo lake ni kurudisha uwajibikaji, kuzuia upotevu wa hela ya serikali, kusimamia makusanyo ya kodi na matumizi yake. Lakini hayo siyo malengo kuu bali ni mambo ya kabla (prerequisites) kwa nia ya kutimiza malengo makuu ambayo kimsingi aliyasema ni kuongeza ajira na mapato ya serikali kwa kupitia viwanda vikubwa na vya kati.
Maswali yangu:

- Chuo Kikuu Dodoma
- Barabara za lami maeneo mengi japo nyingine hazina ubora
- Ukarabati wa majengo mengi ya hospitali
- Ununuzi wa vifaa mbalimbali vya tiba katika hospitali nyingi za serikali
- Daraja la Kigamboni
- Daraja la kuunganisha na Msumbiji
- Vifaa vipya vya kijeshi na magari ya kisasa ya washawasha
- Barabara za mabasi yaendayo kasi
- Taasisi ya Moyo
Rais Magufuli afahamu kuwa mwananchi wa kawaida haangalii kama amepatiwa matibabu kutoka kwenye hospitali iliyojenga kwa msaada au kwa kujitegemea, haangalii kama wateja kwenye biashara yake ya chakula wanatumia hela waliyoipata kiuhalali au wameifanyia ufisadi serikali, haangalii kama ameajiriwa na kampuni ambayo mmiliki wake ni muadilifu au alifisadi hela ya umma. Unaweza kutumbua majipu mengi sana lakini kama mwananchi wa kawaida zamani katika kuhangaika kwake alikuwa anapata shilingi 5,000 sasa hapati hata 1,000, kwake itakuwa vigumu sana kuamini kuwa uongozi wa sasa ni bora kuliko wa zamani.
Kwa sasa watu wadogo huko mitaani maisha yao ni magumu sana. Tunawaambia wafunge mikanda lakini hawa hata sehemu ya kufungia mikanda hawana. Wengi waliokuwa wanajenga wamesimama, waliokuwa wanauza matofali hayanunuliwi, kwa sababu matofali hayanunuliwi, cement nayo madukani inadoda, mafundi ujenzi wadogo wadogo hawapati kazi za ujenzi, akina mama nitlie waliokuwa wanashinda kwenye ujenzi kuwauzia chakula vibarua, hawana kazi pia, n.k.
Kwa upande wa serikali ya Magufuli, kwa sasa ni karibia nusu mwaka unaisha. Nini kikubwa kilichofanyika? Wengi watasema kutumbua majipu, ambayo kimsingi lengo lake ni kurudisha uwajibikaji, kuzuia upotevu wa hela ya serikali, kusimamia makusanyo ya kodi na matumizi yake. Lakini hayo siyo malengo kuu bali ni mambo ya kabla (prerequisites) kwa nia ya kutimiza malengo makuu ambayo kimsingi aliyasema ni kuongeza ajira na mapato ya serikali kwa kupitia viwanda vikubwa na vya kati.
Maswali yangu:
- Je, mpaka sasa nini mafanikio ya kufikia malengo haya makuu?
- Je tupo njiani tayari kuelekea huko kwenye Tanzania ya viwanda au hata njia hatujaiona?
- Viwanda vingapi vimeanza kujengwa au mipango yake ya kujengwa imekwishakamilika?
- Viwanda hivi ni katika sekta zipi, na vitaajiri watu wangapi?
- Serikali inatarajia kupata mapato kiasi gani kutoka katika viwanda hivyo?