wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,932
- 4,534
Urais tumekupa sisi,kifupi wewe siyo bosi wetu, sisi ndio mabosi wako, kwa sababu serikali si ya kwako bali ni mali ya watanzania wote mil 50.
Lakini imefikia hatua sasa sisi hatuna sauti, tukikukosoa tunaonekana wasaliti wa taifa, kila jambo tusifie tu hata kama nchi inapotea.
Sasa hivi kuna mtu anaitwa Makonda,huyu anadai Dar es salaam ni mkoa wake, yaani Dar ni jiji la watanzania wote leo limekuwa jiji la mtu mmoja tu.
Makonda uliyemwambia apige kazi baada ya kuvamia kituo cha Clouds Radio na ukamfukuza kazi waziri wako wa habari Nape, yote hii ni kumlinda Makonda ili azidi kuichafua serikali unayoiongoza.
Makonda amevimba kichwa, kila kukicha anakuja na mapya, sasa hivi amekuwa muhusika mkuu wa wanawake waliotelekezewa watoto, wakati kuna mamlaka husika na hayo mambo, kaenda mbali zaidi anasema "ole wake mwanaume atakayeitwa ofisini kwake na tuhuma za kutelekeza mtoto asiende,eti atamkamata,".
Makonda wewe ni mahakama, ukimkamata huyo mtu utamfanyaje?
Kali kuliko zote, ni mama mtu mzima mwenye umri usiopungua miaka 32,na yeye kwenda kulalamika kwa makonda eti alitelekezwa na Lowassa, ok inawezekana ikawa ni kweli,lakini mazingira ya tukio ni ya kishamba na ya kupangwa kabisa.
Maswali ya kujiuliza.
1.Tangu Fatuma azaliwe miaka zaidi ya 32 iliyopita hakujua kuwa Lowassa ni baba yake?
2.aliwahi kwenda popote kudai haki ya kutambuliwa kama mtoto wa Lowassa ikashindikana?
3.mihimili ya kutoa haki haikuwepo hadi Makonda alipoteuliwa kuwa mkuu wa mkoa?
4.Lowassa ni mtu maarufu kimataifa,ni chombo gani cha habari kiliwahi kuandika juu ya Fatuma kutelekezwa na Lowassa hadi makonda alipoibuka?
5.Fatuma au mama yake au ndugu yake yoyote waliwahi kupeleka malalamiko mahakamani ya kutelekezwa kwa Fatuma na Lowassa,na mahakama zote Fatuma akashindwa kesi na sasa Makonda ni supreme court?
Rais magufuli,huu ni mchezo wa kuchafua watu kisiasa,na hautaiacha salama hii serikali.
Ni chuki za wazi na kupaka watu matope na kuharibu heshima zao,ndo maana nahoji unaipeleka wapi Tanzania?
Vipi kesho akiibuka kijana wa miaka 25 akadai wewe ni baba yake ulimkimbia nini kitatokea?