Magufuli unaitakia nini Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli unaitakia nini Tanzania?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by wiseboy., Apr 12, 2018.

 1. wiseboy.

  wiseboy. JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2018
  Joined: Aug 11, 2014
  Messages: 3,060
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  Urais tumekupa sisi,kifupi wewe siyo bosi wetu ,sisi ndo mabosi wako ,kwa sababu serikali si ya kwako bali ni mali ya watanzania wote mil 50.
  Lakini imefikia hatua sasa sisi hatuna sauti,tukikukosoa tunaonekana wasaliti wa taifa,kila jambo tusifie tu hata kama nchi inapotea.
  Sasa hivi kuna mtu anaitwa Makonda,huyu anadai Dar es salaam ni mkoa wake,yaani Dar ni jiji la watanzania wote leo limekuwa jiji la mtu mmoja tu.
  Makonda uliyemwambia apige kazi baada ya kuvamia kituo cha Clouds Radio na ukamfukuza kazi waziri wako wa habari Nape,yote hii ni kumlinda Makonda ili azidi kuichafua serikali unayoiongoza.
  Makonda amevimba kichwa,kila kukicha anakuja na mapya,sasa hivi amekuwa muhusika mkuu wa wanawake waliotelekezewa watoto,wakati kuna mamlaka husika na hayo mambo,kaenda mbali zaidi anasema "ole wake mwanaume atakayeitwa ofisini kwake na tuhuma za kutelekeza mtoto asiende,eti atamkamata,".
  Makonda wewe ni mahakama,ukimkamata huyo mtu utamfanyaje?
  kali kuliko zote,ni mama mtu mzima mwenye umri usiopungua miaka 32,na yeye kwenda kulalamika kwa makonda eti alitelekezwa na Lowassa ,ok inawezekana ikawa ni kweli,lakini mazingira ya tukio ni ya kishamba na ya kupangwa kabisa.
  Maswali ya kujiuliza.
  1.Tangu Fatuma azaliwe miaka zaidi ya 32 iliyopita hakujua kuwa Lowassa ni baba yake?
  2.aliwahi kwenda popote kudai haki ya kutambuliwa kama mtoto wa Lowassa ikashindikana?
  3.mihimili ya kutoa haki haikuwepo hadi Makonda alipoteuliwa kuwa mkuu wa mkoa?
  4.Lowassa ni mtu maarufu kimataifa,ni chombo gani cha habari kiliwahi kuandika juu ya Fatuma kutelekezwa na Lowassa hadi makonda alipoibuka?
  5.Fatuma au mama yake au ndugu yake yoyote waliwahi kupeleka malalamiko mahakamani ya kutelekezwa kwa Fatuma na Lowassa,na mahakama zote Fatuma akashindwa kesi na sasa Makonda ni supreme court?
  Rais magufuli,huu ni mchezo wa kuchafua watu kisiasa,na hautaiacha salama hii serikali.
  Ni chuki za wazi na kupaka watu matope na kuharibu heshima zao,ndo maana nahoji unaipeleka wapi Tanzania?
  Vp kesho akiibuka kijana wa miaka 25 akadai wewe ni baba yake ulimkimbia nini kitatokea?
   
 2. Heci

  Heci JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2018
  Joined: Aug 14, 2016
  Messages: 921
  Likes Received: 822
  Trophy Points: 180
  Watanzania tumezidi ubaya. Mijitu miwili inaswaga watu zaidi ya million hamsini kama ng'ombe, hamna utii wa Sheria Wala kufuata katiba
   
 3. Mkonga100

  Mkonga100 JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2018
  Joined: Mar 21, 2017
  Messages: 646
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 80
  Mapovu tyu
   
 4. a

  abdukarim JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2018
  Joined: Mar 29, 2017
  Messages: 421
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 180
  Magu nachukia mpaka bac, unwaua watanzania huku ukiwa unacheka, unauwa elim yao ili watoto wao waendelee kuwa maskini. Wengne watakupwnda ila mm skupendi kabisa.
   
 5. Me too

  Me too JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2018
  Joined: Feb 9, 2015
  Messages: 3,442
  Likes Received: 2,282
  Trophy Points: 280
  mkuu vipi mbona la lowassa limekuuma? vipi hao wamama walioenda hapo hayo maswali yanawahusu sana hasa hili  JE MAHAKAMA YA HAKI ZA BINADAMU HAWAKUIJUA TOKA AWALI? kwanini hawakufata mfano wa HAMISA?

  mambo mengine ni sisi wanannchi tu kuzichakachua akili zetu. hiyo yote watu muonekane kwenye media.
  kwani makonda aliwashika mikono hao wamama na kuwatoa majumbani kwao?
  huono ni sisi wenye Taifa ndio tulioteleza nakujianika kwa makondabadala ya kuzijenga familia?

  NB: taifa -Taifa.
   
 6. wa stendi

  wa stendi JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2018
  Joined: Jul 7, 2016
  Messages: 4,415
  Likes Received: 2,951
  Trophy Points: 280
  Tafuta kilipuzi basi kuwaokoa wenzako
   
 7. wa stendi

  wa stendi JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2018
  Joined: Jul 7, 2016
  Messages: 4,415
  Likes Received: 2,951
  Trophy Points: 280
  Ila mkuu usihukumu mtu bila kuwa na uhakika je.unaushahidi yeye ndo anaeua?
   
 8. J

  Jamaa_Mbishi JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2018
  Joined: Jun 15, 2013
  Messages: 5,364
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280

  Dogo sikia...hawa viongozi wetu naweza kusema karibia ya wote wana watoto waliozaa nje ya ndoa zao. Huyu msichana si mjinga, unafikiri kwanini anataka apimwe DNA yeye na Lowassa? Na mbona siku za nyuma alikuwa anasaidiwa na one of Lowassa's blood? Si kila kitu siasa jamani, jiulize kama wewe ndo huyu demu uliyetelekezwa na baba yako (Lowassa), how would you feel?
   
 9. b

  bonphace phallo Member

  #9
  Apr 17, 2018 at 1:58 PM
  Joined: Aug 27, 2015
  Messages: 5
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Katiba mpya tunataka.
   
Loading...