Magufuli ukifanya hivi hutasumbuka kupiga kampeni 2020

Uungwana Vitendo

JF-Expert Member
Nov 20, 2013
1,323
508
Mzee kuna tetesi kuwa una akaunti humu hata kama si kweli ila washauri wako wapo na systime itakupa salamu.Katika swala la nyumba na makazi ni jukumu linaloihusu serikali kwa asilimia kubwa.Leo wanavunjiwa watu wa mabondeni wanaambiwa wahame sawa ni makazi hatarishi lakini wanakwenda kuishi wapi?

Hivi mzee ukiamua kupima viwanja kwa wingi kuanzia Kibaha na kuendelea naamini utapata viwanja vingi sana.

Ukiongezea Vikindu kuendelea na Mapinga kwa ujumla pembeni mwa jiji la DSM kuna maeneo makubwa tu yanahitaji plan.Na zikajengwa kabisa huduma za kijamii kama shule ,hospitali ,masoko ,vituo vya polisi nk.

Kisha wapewe hawa wakazi wa mabondeni sidhani kama kuna atakayekataa.kwa kuanzia na bonde hili la msimbazi na mkwajuni eneo ambalo linakuja kugeuzwa kuwa la burudani.Eneo hili lina nyumba ambazo hazizidi hata 5000.

Ukuchagua sehemu moja wapo hapo juu ukapima viwanja elfu 50 ukavigawa kwa wakazi hawa na vingine vitabaki utakuwa umewasaidia wanyonge wasio na uwezo mzee.

Mzee kama watu wako wa chini wanakwambia kuwa hawa watu walipewa viwanja mwabepande sio wote waliopata nakusihi fuatilia uone maafisa wa serikali waliivyoshiriki kupiga dili.

Leo nchi ya Uturuki inaamua kuujenga upya mji wake wa Istanbul kwa kuuvunja upya mji lakini wanachi wanapewa nyumba za dharura sidhani kama hapa inashindikana.
 
Back
Top Bottom