Ila nashauli pajengwe chuo kikubwa ndani ya hospitali cha mambo ya afya ili kuufungua mji wa musoma katika biashara kwani mji umezorota hauendelei viwanda vyote vilikwisha kufa mfano mutex maisha magumu, Leo hii mji wa musoma unazidiwa hata na singida nafikili hata manyara ya juzi itaupita mkoa huu,hivo juhudi binafsi Zinatakiwa kuchukuliwa kuuokoa mkoa huu uliodumaa kimaendeleo,Leo Serengeti inahesabika kuwa ya Arusha mapato yote yanaenda arusha hakuna hata hoteli moja ya utalii viongozi wetu tunaowachagua hawajengi hoja za msingi kuuendeleza mkoa huu,huu mkoa ulibalikiwa kutoa viongozi wakubwa kitaifa lakini hakuna hata mmoja anaeupigania wengi wao ubinafsi umewajaa kila mtu anajali maslahi ya wilaya yake inauma sana