Magufuli: Tujadili uwezo wake

Magufuli: Tujadili uwezo wake

crabat

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2012
Posts
4,323
Reaction score
2,210
Magufuli nje ya matinga tunga.

Ccm wamemlitisha Magufuli waziri wa barabara kwa miaka mingi tokea ssrikali ya Mkapa.

Amedumu zaidi katika wizara ya bara bara kuliko wiza nyengine alofanyia kazi.

Sifa yake kuu inayotumiwa ma Ccm ni ujenzi wa bara bara. Wizara nyengine alizokaa hakuonekani chochote kile kinacho ashiria ufanisi wake.

Alikuwa waziri wa nyumba na kubwa alofanikisha ni kuuza nyumba za serikalili zenye thamani kubwa kwa bei ya kutupa. Pia akiwajengea mawaziri na senior staff wa serikali nyumba za cimmunity na wengi walikataa kuishi huko.

Utakavokuwa vovote Tanzania itapata Rais au Lowassa ...hili ni kutokana na harakati za siasa zinavo Onekana.

Hivyo kwa vile tunatarajia Labda Magufuli atashinda hivyo tumjadili uwezo wake.

1. Kuna suala mambo ya nje na mahusiano ya nje..jee ana msimamo gani na uwezo wake kifiplomasia uko vipi. Masuala ya EAC . AU UN SADCC Na kuna masuala ya kimataifa.

Masuala ya kushiriki kijeshi nje ya nchi...mfano somali . Kikwete ali kataa kuingilia Somali kijeshi..na haya ni masuala ya Urais.

Tanzania hatuna utaratibu wa bunge kuridhia jeshi letu kushiriki masuala ya nje. Ni rais tu ndio mwamuzi jee magufuli anao uzoefu huu na mamuzi yake bila kuathiri usalama na mahusiano ?

2. Kuna suala la Muungano. Hili suala linahitaji siasa na diplomasia ya hali ya juu.ubabe au kutofahamu siasa yake inaweza kuleta mfarakano. Pale jangwani alisema yeye anachojua ni utanzania tu...watu wengi hawaku notice lakini huo ni udhaifu.

3. Je, magufuli atakubalika na mataifa makubwa wafadhili wetu?

4 Suala la mafuta jee lipi jipya analo litaloifanya Tanzania kufaidi. Dubai na wengine sio miujiza ila ni matumizi mazuri na faida nuu ya mafuta yao.Je, vipi nasi miaka kumi ijayo tutakuwa Dubai ?

5. Suala la ajira na kujaa kwa machunga wa kichina ...hili ni tatizo..hawa wachina wanaingia kwa wastani mmubwa kila siku na chama chake its seems hawana sera ya kueleweka.

Wengi hawa ni chingas tu sio wawekezeja. Pia suala la m TX wa kizungu na Asia ..ni wengi mno.

In fact nusu ya nyumba za Upanga wanaishi ma TX wa nje na kazi zao sio proffesionalns.kule Masaki 90% wanakaa wazungu kama waajiriwa.

Ni wazi nafasi nyingi zimeshikwa wageni...jee magufuli anao ubavu wa kuwaliga stop wageni hawa?

Tumuangalie Magufuli.
 
Hakuna kitu anachojua zaidi ya SINTOWAANGUSHA
 
yaan binafsi nawashangaa wanaompigia chapuo magufuli wakidhani uraisi kila mtu ana weza,

angebaki kwenya mabarabara yake ya chini ya kiwango nafasi ile kidogo alikuwa anaweza kufanya maigizo yake.

tuwe wakweli tuache unafiki urasi hauwezi magufuli jamani
 
Katika issue ya uhusiano kimataifa i have concerns pia mara nyingi magufuli amekuwa mtu wa kurush katika decision si mtulivu kuanalyse vitu critically before kuamua .
 
Haimaniishi kwamba ukiwa rais una akiri sana ama unajua kila kitu na pili urais ni taasisi na ndo maana utaona kuna washauri wa rais latika mambo yote muhimu ..so worry not much!
 
Jaman bila kukaanga maneno,magufuli ni mtendajj,lowassa mzee wa kuanika ngoma juani hana uwajibikaji wowote ni mtu wa kutafuta support ya magenge,magufuli hana magenge,vote for magufuli
 
Ukitaka kumumaliza Magufuli mpeleke kwenye mambo ya diplomasia hajui kabisa mambo ya diplomasia hata pale ambambo hapahitajiki kutumia ubabe panahitajika kutumia diplomasia hana lingine zaidi ya kusema hapa kazi tu,hata kama ukimwambia kuwa hili unalolifanya litaangamiza nchi jibu utakalopewa ni hapa kazi tu.

Utendaji kazi wa Magufuli uko sawa na kipofu ambaye anapotembea hajui kuwa mbele anakoelekea kuna ukuta atakuja kujitambua baadaye baada ya kujibamiza kwenye ukuta ndipo atakapokuja kushituka kuwa njia aliokuwa ana ifuata ilikuwa inampeleka kwenye ukuta.
 
crabat,

..Magufuli anahitaji kuwa na mtu juu yake ambaye atam-moderate frm time to time.

..huyu akiwa ndiyo raisi wa Tz, kwa maana ndiyo alfa na omega, anaweza kusababisha madhara makubwa sana.

..jambo lingine linalotia shaka ni mtizamo wake kuhusu vyama vya siasa na demokrasia ya vyama vingi. sina uhakika kama ataheshimu uhuru wa vyama vya siasa, vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, na maandamano.
 
Last edited by a moderator:
Jaman bila kukaanga maneno,magufuli ni mtendajj,lowassa mzee wa kuanika ngoma juani hana uwajibikaji wowote ni mtu wa kutafuta support ya magenge,magufuli hana magenge,vote for magufuli

Eti watu wanamfananisha Daktari na mwanasanaa.Mtu asiyesoma au mjinga ndiye anaweza kuamini kuwa mwana mahesabu anaweza zidiwa reasoning na mwanafasihi muigizaji.
 
It is a time bomb
nitaruhusu askari kuwapiga risasi majambazi
nitawadhibiti wezi wa dawa mahospitalini , wakati central medical store wanaidai serikali
walimuwatapata laptop wakati walimu wanaidai serikali mabilioni ya mafao yao
nitajenga hospital ya rufaa ,wakati zilizopo mikoani hali ni mbaya sana hazina vitendea kazi kama vile xray , CT scan nk
Kila kijiji watapewa milioni hamsini
 
You can not compare a mathematician to an artist interms of reasoning and decision making ability.
 
yaan binafsi nawashangaa wanaompigia chapuo magufuli wakidhani uraisi kila mtu ana weza,

angebaki kwenya mabarabara yake ya chini ya kiwango nafasi ile kidogo alikuwa anaweza kufanya maigizo yake.

tuwe wakweli tuache unafiki urasi hauwezi magufuli jamani

Lowasa atamzidi Magufuli kwenye ishu za wizi na umafya.Hakuna pahala pa kumtolea mfano Lowasa kuwa ali alifanikiwa zaidi ya wizi.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Magufuli sifa yake kubwa ni UKUTUPUKAJI kwenye uraisi hatufai hata kidogo
 
We unadhani Rais analala na mkewe halafu asubuhi anasema jeshi liende somalia? Labda mgombea wa chama chenu ndo atakuwa na sifa hizo.

Maamuzi ya Rais yanatoka baada ya kujadiliana na baraza la Mawaziri, washauri wa Rais kwenye suala husika na hata usalama wa taifa pale inapobidi.

Hakuna Rais mtaalamu wa kila kitu, hata Magufuli hajui kila kitu ndo maana atakuw ana baraza la mawaziri na washauri wake
 
We unadhani Rais analala na mkewe halafu asubuhi anasema jeshi liende somalia? Labda mgombea wa chama chenu ndo atakuwa na sifa hizo.

Maamuzi ya Rais yanatoka baada ya kujadiliana na baraza la Mawaziri, washauri wa Rais kwenye suala husika na hata usalama wa taifa pale inapobidi.

Hakuna Rais mtaalamu wa kila kitu, hata Magufuli hajui kila kitu ndo maana atakuw ana baraza la mawaziri na washauri wake

Nakubali unayosema lakini uamuzi wake ni wa mwisho..in fact hili suala linatakiwa litolewe na bunge, kwani lina maslahi mapana ya nchi. Unajua kuna presha za kila aina kutoka mataifa makubwa ? Mikikiki yake ni balaaa..kuna vitisho unatakiwa kutulia..
Any way hoja hapa ni kuangalia uwezo wake na intrlingendia yake ..kama yupo fiti kabisa well basi tupo in safe hands...hivyo jadili uwezo wake usiende kwenye kulaumu
 
Back
Top Bottom