Magufuli: Subirini ushindi wa Tsunami

Magufuli: Subirini ushindi wa Tsunami

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,374
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, amewahakikishia wana-CCM na Watanzaia kwa ujumla kuwa mwaka huu, chama kitapata ushindi wa Tsunami na si wa kishindo wala kimbunga.

Dk Magufuli alisema hayo nje ya ofisi ya chama hicho mkoani Mtwara juzi alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho ambapo alisisitiza kuwa wapinzani watapiga kelele sana, wataongea sana lakini ushindi kwa CCM ni lazima na upo pale pale.

Alisema ushindi huo unatokana na matawi yaliyoanguka ndani ya chama na kuhama na kwamba watu hao wameiacha CCM ikiwa safi na salama zaidi. Alisema watu hao walikuwa wakitumia fedha nyingi kurubuni watu wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM ambapo chama kiliwakata na kukimbilia vyama vingine vya upinzani.

Aliwataka wana-CCM wasikatishwe tamaa na watu wa aina hiyo na badala yake washikamane, wawe kitu kimoja na kwamba mwaka huu, chama kitafanya kampeni za kisayansi. Aidha, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema ni kazi rahisi kumnadi Dk Magufuli kutokana na vigezo na sifa alizonazo.

Mwigulu, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alisema walioshindwa kwenye mchakato wa kura za maoni na kuhama ndani ya chama, hivi sasa wanahaha kutafuta urais wenyewe ambapo wanatoa mpaka hela ili kutafuta uongozi, lakini wataumbuka mapema.

Akizungumza na mamia ya wana-CCM waliojitokeza kumpokea katika hiyo ofisi ya chama ambapo alifika kwa ajili ya kuwasalimia na kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mgombea na kumdhamini, Dk Magufuli aliwataka makada hao na Wtanzania kwa ujumla kutoyumba kwa kuwa Watanzania walio wengi bado wanakipenda Chama.

"Ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga ni wa Tsunami, watapiga kelele sana, watakuja na propaganda nyingi sana, lakini ushindi wa CCM ni lazima. Ni lazima tupate ushindi wa rais, wabunge, wawakilishi na madiwani," alisema. Alisema walikuwa watu 42, wakati wakiomba kuteuliwa na chama hivi sasa, CCM ina kundi moja tu la ushindi.

"Hako ka tawi kamoja ndio kakameguka kwenda uko mbali, mti ambao unataka upate mbao zake nzuri matawi kudondoka chini ni vizuri ili upate mbao safi. "Lakini baada ya kudondoka hilo ni jambo la kawaida kwa chama kikubwa kama CCM.

Hata ukiangalia tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wapo waliotoka wako akina Kambona walitoka na wengine walifukuzwa na wengine walijua watafukuzwa wakakimbia wenyewe kabla ya kufukuzwa kama hao," alisema.

Alisema iwapo atachaguliwa kuongoza dola atapenda awe mtumishi wa watu, asiyekuwa na majivuno ili aweze kuwatumikia wananchi na atomize matarajio yao. Dk Magufuli alisema wakati wa kampeni ukifika zitafanyika za kistaarabu na kisayansi na kwamba zitakuwa za shina kwa shina, tawi kwa tawi, kata kwa kata, jimbo kwa jimbo, wilaya, mkoa na taifa.

Aliwataka wana-CCM wasimame imara kwani wananchi wengi wanakipenda Chama. Dk Magufuli akizungumzia uzoefu wake ndani ya CCM, alisema alikuwa mbunge katika kipindi chake cha miaka 20, ambapo vipindi viwli alipita bila kupingwa na alikuwa waziri kwa miaka 20 katika wizara mbalimbali.

Alisema anaifahamu vizuri Mtwara, Tanzania, CCM na kero za Watanzania anazifahamu vya kutosha hivyo akipewa nafasi watashudia wenyewe kasi ya utendaji kwa maendeleo ya taifa. "Nilichaguliwa na mkutano mkuu kutoka kila kona ya nchi kwa asilimia 87, wale walionichagua waliwakishia Watanzania wote.

Niwahakikishie kuwa mwaka huu, tutashinda zaidi," alisema. Aliwataka wana-CCM katika umoja wao kutulia na kutoyumbishwa na maneno ya porojo kwa kuwa chama kinajiuliza kwa kile walichofanya kwa wananchi na si maneno matamu bila vitendo.

"Chama nakifahamu, shida za wana-CCM nazifahamu, matarajio yao nayafahamu, shida za wananchi nazifahamu hivyo kama nitachaguliwa nitawatumikia kwa uadilifu mkubwa ili kuwaletea maendeleo," alisema.

Chanzo: Habari Leo
 
CCM mbele kwa mbele, ngoja UKIWA wajidanganye na nyomi ya jana ambao robo tatu hawana vitambulisho vya mpiga kura.Ushindi mapemaaa kabisaaaaaa.
 
Namuonea hurumaaaaa Magufuli....

Yaani, pole sana Magufuli, ur in a wrong party, at a wrong time and place...!!!


Lowassa kashamaliza kazi...tunasubiri kuapishwa tu.
 
Yeah majangili anawafahamu, waua albino anawajua, wait a twiga pia...Sasa hatutaki wa,kuwalea Bali wa kuwasweka jela...



Hatutaki tena wapiga gitaa na madisko ikulu...km mnataka kupiga tumba kajiungeni DDC Kibisa !!!
 
Mwenyekeiti wao alishawaonya kwamba habari ya ushindi wa kishindo haipo tena siku hiziz. Na kwamba wasitegemee kwamba mtu akiteuliwa na CCM basi yeye ni rais ambavyo imekuwa siku nyingi. Ila kwa mafuriko ya jana inabidi ajipe matumini maana yale mafuriko yanaweza kukuua kwa pressure aisee!
 
CCM mbele kwa mbele, ngoja UKIWA wajidanganye na nyomi ya jana ambao robo tatu hawana vitambulisho vya mpiga kura.Ushindi mapemaaa kabisaaaaaa.
Hapana, watu walijiandikisha ili wapate vitambulisho kwa ajili ya matumizi ya kiraia , and not specifically kwa ajili ya kura. Hivyo usijidanganye, imetokea coincidence kuwa uchaguzi umecoincide na need for the people to be in dire need of identity cards for civil use!
Had it not been for the need of national identity cards, the turn out for voters registration would have been low!
 
Hapana, watu walijiandikisha ili wapate vitambulisho kwa ajili ya matumizi ya kiraia , and not specifically kwa ajili ya kura. Hivyo usijidanganye, imetokea coincidence kuwa uchaguzi umecoincide na need for the people to be in dire need of identity cards for civil use!
Had it not been for the need of national identity cards, the turn out for voters registration would have been low!

Point, nilikuwa sijalifikiria hilo mkuu, Tena baada ya Lowassa kuhamia Ukawa speed ya kujiandikisha iliongezeka
 
RAIS Maghufuli alikuwa anahutubia wapi?? tena anapita bilavl kupingwa huyu jamaa anapendwa kiasi hicho
 
Magufuli ndo kayasema haya???
Hadi namuonea huruma, tatizo jingine ni kama chama kimemtelekeza,
Hivi hawa watu hawajajipanga??? nimeangalia mkutano wa Magufulii jana Mtwara
Ni aibu tuuupu, nadhani hawakumsupport hela ya kwenda kubeba wanavijiji vijijini
 
Katika tafiti zote zilizopita ilionekana Lowassa anaongoza na Dr Slaa anamfuata kwa karibu. Maghufuli hata kwenye tano bora alikuwa haonekani, sasa imani ya kushinda inatoka wapi?

Baada ya Lowassa kuchukua fomu ya Ukawa Maghufuli akapotea hata kwenye media na mikutano yake huko Mtwara ilikuwa kama ya mgombea udiwani. Jeuri ya ushindi inatoka wapi?

Pamoja na kitengo kupenyeza lupia kwa Ukawa kwa lengo la kuvuruga bado Ukawa wamebaki wamoja na wanasonga mbele. Majigambo yanatoka wapi?

Sina hakika kama Maghufuri anaweza kupata kura laki moja mikoa ya Arusha na Manyara. Lakini je Lowassa hatakomba kura za kutosha Geita? Hilo linahitaji miwani kuliona?

Ccm inabomoka kila siku, wanachama wanakimbia kwa maelfu. Wanategemea goli la mkono! Goli la mkono wakati unachezwa nusu uwanja?
 
Wamarekani Na Wachina Wametabiri kuwa Magufuli atashinda.
Sasa hapo watu wa ukawa mkae tayari kupokea Kichapo kitakatifu kutoka Kwa Polisi iwapo mtapinga matokeo.

Hii nchi mali ya Watu. Hivi nyie Watz mpk leo hamjaliona Hilo?
 
Namwonea huruma huyu Baba hadi sura imeanza kupoteza nuru aisee
 
Back
Top Bottom