The Boss,
Hayo mambo acha tu!!!
Mimi mama yangu ni mtu wa Lindi! Enzi hizo tupo wadogo ikabidi twende likizo kule! HUwezi amini nini kilitukuta!!!
Tulitoka Lindi kurudi Dar es salaam wiki moja kabla ya mashule kufunguliwa!!!
Hadi tunafika Dar sister angu ambae alikuwa mmwanafunzi; alikuwa tayari amechelewa wiki mbili... which means, Lindi - Dar ambayo ni safari ya saa 5-6 ilituchukua wiki 3!!!!!
"Better" option ilikuwa ni kupitia Songea! Sasa hebu fikiria... mtu unaenda Lindi au unatoka Lindi kwenda Dar lakini unalazimika kupita Songea... wapi na wapi!!!!
Mbaya zaidi, Lindi to Songea ni mbali zaidi kuliko Lindi to Dar es salaam!!! Lakini unalazimika kusafiri umbali mrefu zaidi kuliko kule unakoenda ili tu ukakutane na barabara ambayo nayo itakuongezea umbali mara 2 zaidi na kufanya safari mzima kuwa zaidi ya 1300 km badala ya 450 km!!!
Lakini hata ukisema upite barabara ya Songea; ilikuwa kutoka Masasi hadi kuipata Songea mnaweza kutumia siku 2 hadi 3!!!
Ulichosema ni ukweli mtupu!!! Bwana Mkubwa huyu ndo angeikuta Tanzania ile sijui angefanyaje!!
Na anavyoboa utadhani kuna mtu alimlazimisha!! Always trying act cry innocent aliyebebeshwa zigo as if kuna mtu alimlazimisha!!!
Kapewa nchi almost mahitaji yote muhimu bado analilia wakati akina Mwinyi wameingia madarakani wakikuta mkoa mzima una shule chini ya 5 za sekondari!!!!
Li-Dar es salaam lote hili nalo shule zilikuwa zinahesabika!!!
Enzi hizo tunatoka Kurasini, shule St. Anthony's... basi mvua zikichanganya mnalazimika kuteremkia Mtongani manake unakuta kuanzia pale relini hadi Mission hapapitiki!!