Magufuli, Pro. Ndalichako kuna hili jipu la TCU

mzee wa kismati

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
2,292
795
TCU NALO NI JIPU

Sasa katika vyuo vyote nchini Tanzania kumekuwepo na Ongezeko la hichi wanachokiita FEDHA KWA AJILI YA TCU, SH 20000 ambayo kila mwanafunzi wa elimu ya juu hawezi kufanyiwa usahili/usajili bila kulipia hiyo fedha!!!

Katika Makala hii, ninayo machache ambayo nataka nawe kama mwanafunzi mwenzangu uyatafakali na kuyaelewa n ahata kupiga kelele juu ya huu ninao uona kuwa ni JIPU LA KUTUMBULIWA kwani inaonyesha ni wizi wa hali ya juu ambao TCU (TANZANIA COMMMISSION FOR UNIVERSITY) ili kula Pesa zetu watoto wa maskini na watoto wa wakulima ambazo ni Zaidi ya bil 3 kwa makadilio ya chini ya wanafunzi wote Tanzania ambao nimekadilia kama wanafunzi 150,000 tu kwa vyuo vyote kama watatoa fedha hiyo
Sasa ya kujiuliza fedha zote hizo Zaidi ya bil 3 wanayoichaji TCU kwa wanafunzi wote Tz inatumikakatika kufanyia nini?Hilo ndilo swali waliloshindwa kuwaeleza wanafunzi wa kila chuo!!Lakini hata wakisema ni kwa ajili ya kuiendesha taasisi yao bado unalo la kujiuliza!!! Cha pili cha kujiuliza je miaka yote kabla ya hapo ilikuwa inajiendeshaje na kwanini ianze mwaka huu,?Ni kwa maboresho gani wanayofanya mpaka ichajishe kiwango hicho chote tena kwa watoto wa wakulima?
Lakini swali la Msingi linakuja ni kwamba hii TCU,sisi kama wanafunzi wa Elimu ya Juu tunamalizana nao mkataba baada tu ya kulipia 30,000 mara ya kwanza kwa ajili ya kutupangia vyuotunavyopaswa kwenda!!Baada ya hapo hakuna mwingiliano wowote wa TCU na wanafunzi wa ChuoZaidi itabaki labda mwingiliano kati ya Chuo husika na TCU kwa ajili ya maswala ya QUALITY ASSURANCE,ambayo ni jukumu la chuo husika kulipa pesa hiyo kutokana na ada za wanafunzi lakini sio mwanafunzi kulipa direct TCU.Sasa Je kwanini tuwalipe TCU wakati hawana Msaada tena kwetu na tulishawalipa mara tu tulipoanza usahili wa kutafuta chuo!!!HUuoni kuwa huu ni WIZI MTUPU

Na ilivyo ni kwamba swala la wanafunzi kulipa directTCU bado lipo kama mswada ambao bado haujapitiswa bungeni!Hivyo hichi wanachokifanya TCU sasa ni kukiuka maadili ya sharia ambavyo isingepaswa kupitishwa maana fedha hizi zinawaumiza watoto wengi wa wakulima kubebeshwa mzigo wasiopaswa kulipia
Hivyo wewe kaka Mwanafunzi au Kiongozi wa Serikali ya wanafunzi,Piga kelele mpaka MTUMBUA MAJIPU,ALIONE JIPU HILI,LIPATE KUTUMBULIWA.Hata kama wengine mmeshaanza kulipa bado unaweza kukisaidia kizazi kijacho nyuma yako wasibebeshwe mzigo huu.Viongozi wa serikali za wanafunzi mavyuonni na TAHILISO hakikisheni mnasimama upande wa kuwatetea wanafunzi wenu katika kulihoji na kulifuatilia swala hili ili tupate ufumbuzi tujue hii fedha tunaitoa kwa kazi gani?Msiwe wepesi kutanguliza matakwa yenu,ni haki yenu kuhoji n ahata kufuatilia sehemu husika ili ikiwezekana waliokuwa wamekwisha kulipa warudishiwe pesa zao

Asante kwa kulizingatia hili.Unaweza kulifoward Makala hii mpaka iwafikie wanafunzi wote ili tupate kusaidiana

Shujaa Charles
 
Ama hakika huu ni ufisadi uliokithiri, Kwa nini mwanafunzi alipie pesa kwa ajili ya quality assurance? Ni mambo gani yanayofanyika katika zoezi la quality assurance? Je mambo hayo yanayofanyika yakiwa na maana ya quality assurance ni nje ya majukumu ya kila siku ya TCU?. Je, ni kweli yaweza gahamia kiwango hicho cha pesa?. Hii ni zaidi ya Bilioni 3, kwa maana wanaolipia ni wanafunzi wote wa Diploma, degree na wanafunzi wa shahada za juu. Haya mambo yalifanyika wakati Professor makini (Ndalichako) hayupo. Bila shaka ataliangalia hili na kuhakikisha utaratibu huu wa kukamua pesa kutoka kwa wazazi unakomeshwa mara moja.
 
Back
Top Bottom