Magufuli phobia imenikuta leo, wee acha tuu

JANFE

Member
Joined
Nov 10, 2015
Posts
21
Reaction score
106
Ni siku chache tu zimepita tangu fagia fagia ilipopita na watu wengine kumwagwa kwenye vyeo na nafasi mbalimbali. Sasa, leo nilikuwa nafanya kazi zangu ofisini, mara napigiwa simu na namba ngeni. Kumbe ni bosi wangu katumia namba ambayo mimi sina. Akaniita kuwa nahitajika kwa bosi mwingine (bosi wake). Mara nikakumbuka ile kauli kuwa siku hizi ukiitwa na bosi unaweza kujiunga na wale wazee wa TRA au Bandari, job inayeyuka fasta bila kutarajia. Aisee, na bosi mwenyewe mkalii, ilibidi nipitie maliwato kwanza kuweka mambo sawa.

Nilipofika kumbe napewa cheo kingine, daaaaaah!!!
Hii Magufuli phobia sijui itaisha lini
 
Hihihihhhiiiiii!! Hongera yako ila usifanye sherehe na ukalewa madaraka. Ongeza juhudi zaidi kwa sababu umeongezewa majukumu
 
Hongera brother/sister!

kumbe umeamua kutwambia kuwa umepanda cheo kijanja?hongera zako

Ujumbe umefika.
Hongera kwa kupanda cheo.

duuu.... Hiyo imekaa njema big up

Hongera sana

Umeona eennhhh!!,mbwembwe zote hizo kumbe anataka kutuambia kuwa amepandishwa cheo.

Jamani vyeo vingine ukipandishwa ni msala! Unatumika balaa hata walio chini yako wana afadhali ingawa hela nayo inaongezeka ila unaweza kuona sometimes money is not everything.
 
Acheni hizo, mimi nilipokuwa free lander, hakuna anayenifuatilia nilikua nafanya zangu mishe mtaani ujasiriamali kwa sana nilikuwa napiga hela sana, yaani hizo za kuongezewa majukumu ni kidogo sana nikipiga mahesabu. Hapa nasikitika kwa sababu mbili.; Moja sitakuwa huru kufanya mishe zangu kwa sababu kazi yenyewe itahitaji very close supervision na ndo hivyo nimepigwa pini. Mbili, kiuchumi haitanisaidia sana kivile kwa sababu kwenye miradi yangu nilikuwa napata zaidi. Nyongeza, uhuru ni kitu muhimu.
 
Ni siku chache tu zimepita tangu fagia fagia ilipopita na watu wengine kumwagwa kwenye vyeo na nafasi mbalimbali. Sasa, leo nilikuwa nafanya kazi zangu ofisini, mara napigiwa simu na namba ngeni. Kumbe ni bosi wangu katumia namba ambayo mimi sina. Akaniita kuwa nahitajika kwa bosi mwingine (bosi wake). Mara nikakumbuka ile kauli kuwa siku hizi ukiitwa na bosi unaweza kujiunga na wale wazee wa TRA au Bandari, job inayeyuka fasta bila kutarajia. Aisee, na bosi mwenyewe mkalii, ilibidi nipitie maliwato kwanza kuweka mambo sawa.

Nilipofika kumbe napewa cheo kingine, daaaaaah!!!
Hii Magufuli phobia sijui itaisha lini

Utakua mwizi tu haiwezekani uitwe na bosi wako utake kujikojolea
 
Kwani na wewe ni mzee wa makontena,kama sio kwa nini ulitaka kujiharishia. tehe tehe, aisee Magufuli na Majliwa wanafukuza huku wengine wanapanda vyeo.
 
Ukatumike ili udumu make cheo ni dhamana tu, tunaaamini utaendelea kwa kasi hiyo hiyo ..hongera!
 
Ni siku chache tu zimepita tangu fagia fagia ilipopita na watu wengine kumwagwa kwenye vyeo na nafasi mbalimbali. Sasa, leo nilikuwa nafanya kazi zangu ofisini, mara napigiwa simu na namba ngeni. Kumbe ni bosi wangu katumia namba ambayo mimi sina. Akaniita kuwa nahitajika kwa bosi mwingine (bosi wake). Mara nikakumbuka ile kauli kuwa siku hizi ukiitwa na bosi unaweza kujiunga na wale wazee wa TRA au Bandari, job inayeyuka fasta bila kutarajia. Aisee, na bosi mwenyewe mkalii, ilibidi nipitie maliwato kwanza kuweka mambo sawa.

Nilipofika kumbe napewa cheo kingine, daaaaaah!!!
Hii Magufuli phobia sijui itaisha lini
Unaonekana una madhambi uliyokuwa nayo ndio maana unaogopa ogopa kuitwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom