Ukiyafanya haya tutaenda Dodoma wote kabla ya 2019.
- punguza kasi ya ujenzi kwa NHC na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa sehemu nyingine zote.
- wafanye hawa wawekeze kujenga Dodoma tu kwa miaka miwili ijayo, najua tunaweza kukamilisha ujenzi wa ofisi na nyumba za baadhi ya watumishi wa level za maofisa wajuu wanaostahiki kupewa nyumba, kama mawaziri na makatibu wa wizara na wale makamishna wa majeshi na idara zingine nyeti.
- fufua bank ya nyumba (THB)
- hii bank ije kusaidia wananchi waweze kupata mikopo ya ujenzi hasa kwa wale watakaokuwa wanahamia Dodoma. hii itapunguza tatizo la uhaba wa nyumba lkn pia litaleta Motisha na kisha litalinda hadi ya mji wa Dodoma plus kuleta ukuaji wa kasi unaozingatia mipango miji!
- Achana na habari ya daraja la koko na miradi mingine mikubwa ya Dar, wekeza ktk airport ya Dodoma maana capital city yapaswa ifikike kirahisi isiwe ni kwa basi tu.