John Magufuli: Ninautamani urais!

Nchi hii tunahitaji dikteta. JPMagufuli is the closest to a dictator we can get!. We need one desperately!

You are right Mama yuya. We need a person like Mwl Nyerere. Some one who deeply loves his people, irrespective of their social or other walks of life and someone who when he says YES, he means it and vise versa.

VIVA, JOHN POMBE MAGUFULI. Do not let us down pls, we beg you.
 
Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.

Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos’, muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.

Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.

Licha ya kauli hiyo kusababisha minong’ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.

Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.

Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuendelea na wadhifa huo.

“Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri,” alisema Dk. Magufuli.

“Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh. 3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana,” alisema.

Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.

Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.
Chanzo: Nipashe

==============
UPDATE (1):

Tarehe 18, Feb 2015: Kwa mujibu wa magazeti ya leo; Magufuli katangaza nia kutaka kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano

Hatutaki ccm jamaniiii
 
Hana Nguvu za kisiasa ndani ya CCM na wala hana sifa zozote kuwapita wenzake ndani ya CCM kama Lowassa, Membe, Sitta, Mwakyembe, Mwandosya, Wassira, Mwigulu, Nchimbi.
Ila sifa moja ya kiCCM ya msingi anayo, ambayo ni Ufisadi. Magufuli ni Fisadi mzuri sana.
Lakini pia ni mnafiki mkubwa, kwani ni juzi tu alimkana Sitta na kudai hana mpango wa Urais kabisa!!

Kweli mkuu.
 
Kulingana na hali inavyokwenda jamaa hataachia madaraka. Unajua nini jamaa anachokifanya ni kujenga syndicate ambayo kila pale atakapoleta agenda yake anahakikisha mfumo wake unamlea. Kwamfano timu ya juu kabisa ya maamuzi yote kaiteua yeye au mtu ambaye amemuweka yeye. Kwa maana ileile anahakikisha maeneo yote ya maamuzi ndani ya kikundi chake anayashikia yeye na hakika hakuna maamuzi zaidi yake yeye. Na kaamua kushika hata matawi yote bila haya anaweka watu wanaomtii yeye tu kwa maslahi yake yeye.

Haya maneno mtayakumbuka siku moja. Mwisho wa siku ile kamati ya kuchinja majina itaondolewa kabla ya mwaka wa uchaguzi, maamuzi ya nani awe yatatolewa na kikosi maalum na huenda watakuwa wawakilishi wa hizi taasisi mfano wazazi, vijana nakadhalika. Ipo siku kamati zitakaa zitaona hakuna haja ya kufanya mabadiliko na watapeleka muswada if hiyo ni hypotheis sahihi. au njia ya pili kamati itakata kila mmoja na kumbakisha kijana yule. Unajua kwa msioona mbali mnachukulia poa tu. lakini maneno yanamimba ipo siku yakizaa mtanikumbuka. Nimeanza mikakati ya kuwa na makazi nje ya nyumbani kwangu. Nimeoa ubakini ili ikifikia ule wakati nisiwe mmoja wa kunyamazishwa kwakua najua ukwel waja.

Wakuu naota tu lakini ipo siku yaja. Sina hakika naongelea timu ya mpira au naungelea nini lakini litakuwa tukio kubwa la kihistoria katika nyika yetu kutokea.

Nangu mahwelu
 
Back
Top Bottom