Magufuli ni wa kawaida sana

Magufuli ni wa kawaida sana

Hii inaitwa Stockholm Syndrome. Na hili ni tatizo jingine kwa Tanzania yetu. Tunafanywa mateka kisha twamtetea mtekaji.

Wewe ni Mtanzania, mhanga wa kila uhuni wa kisiasa. Suala si nani asiye wa kawaida Bali nani ni wa kawaida na asiyeweza kuikwamua Tanzania yetu.

Lakini kujibu swali la nani si wa kawaida ambalo kimsingi ulipaswa ujijibu mwenyewe, tumeshuhudia ujasiri wa akina Makongoro calling a spade a spade kwamba CCM imeporwa. Ushamskia Magufuli akiwa na ujasiri huo?

Tuna akina Dkt Slaa waliomudu kututajia wabakaji wa uchumi wetu, wakatishwa kupelekwa mahakamani (actually Riz alienda mahakamani sijui kesi yake vs Slaa imefia SAP) lakini hawakutetereka.

Tuna akina Warioba waliokebehiwa na JK, wakapigwa na akina Makonda lakini wakaendelea kutetea Katiba Mpya.

And you are hereby asking me " nani si wa kawaida"? Why are we so used to settling for less when we actually deserve the best?

Hatutaki maneno..tunataka action...kama Slaa sio wa kawaida mbona anafumbia macho ufisadi unaofanywa na Mbowe?? Kasome waraka wa the late Chacha Wangwe...
We ndo walewale
 
Magufuri ni mchapakazi na anafahamika pia,kama kubebwa na jk ni sahihi sababu kuna watu walitaka kutumia pesa ili waingie wao ikulu,jk aluposema anakura moja muhimu ndiyo iliyotumika kama ilivyotumika na nyerere kwa mkapa,hivyo magufuri ni sahihi na ni mchapakazi,watu wasimbeze kwa interest zao na chuki zao,wajenge hoja,kwanza hata huyo riz watu wanaongea tu,kila kizuri cha riz,hakyna mwenye evidence,wabongo tupunguze kutunga maneno

Halafu wewe huyohuyo pembeni walalamikia hatma ya Tanzania yetu
 

Attachments

  • 1436861397009.jpg
    1436861397009.jpg
    9.4 KB · Views: 117
Labda tusaidie tusiojua. Kipi hasa alichofanya Magufuli unachoweza kukiita 'out of this world'? Bomoabomoa? Daraja la Kigamboni? Kuuza nyumba za serikali? Bil 250 za ripoti ya CAG?

TATIZO NI MAZOWEA YA KU-SETTLE FOR LESS

Kwasasa Tanzania inahitaji rais anayetimiza majukumuyaje...hiyo pekee itatupeleka kwenye 2nd world country...Siku Magufuli anaapishwa, hiyo siku tutaanza kumuandaa candidate ambaye ni "exception" atakayechukua nafasi ya JP come 2025
 
Hatutaki maneno..tunataka action...kama Slaa sio wa kawaida mbona anafumbia macho ufisadi unaofanywa na Mbowe?? Kasome waraka wa the late Chacha Wangwe...
We ndo walewale

Hivi kwa busara kidogo tu,hicho unachoita ufisadi wa Mbowe kingekuwepo, akina Mwigulu na Nape wasingekishikia bango au wangepoteza muda wao kuzusha kesi za ugaidi?
 
Hivi kwa busara kidogo tu,hicho unachoita ufisadi wa Mbowe kingekuwepo, akina Mwigulu na Nape wasingekishikia bango au wangepoteza muda wao kuzusha kesi za ugaidi?

Kwahiyo unabisha kuwa wakati wa uchaguzi Mbowe alikuwa "anakopesha" chama bila documentation zozote afu uchaguzi ukiisha anadai arudishiwe kwa interest ya 100% ?
Huo waraka aliuandika Marehemu Chacha (pamoja na uozo mwingi ndani ya chama-Mbowe hajawai kujibu hizo tuhuma)..siku chache baadae Wangwe akauwawa!
You seem to be lacking alot of information!!
Slaa angeanza kwa kusafisha nyumbayake mwenyewe...
 
Mkuu, tusipowaelimisha hawa wenzetu wavivu wa kufikiri na wepesi wa kusahau tutaendelea kupata kile tusichostahili kila baada ya miaka mitano au kumi. Tusiwapuuze Bali tuendelee kuwaamsha hata kwa bakora ikibidi. Tanzania tunayostahili inawezekana ila tu umoja na mshikamano wa wahanga wa huu uhuni endelevu wa kisiasa.

Mvivu wa kufikiri ni yule anayeona mrengo mmoja tu na kuamini kuwa yuko sahihi kabisa. . . . .ana watu anawapenda na anaamini hao ndio wanaoweza. , ila haweki sifa za hao watu bali kutaja majina na waliyoyafanya, . .anasahau kuwa hoja yake ni kuwa responsibility sio sifa ila kwa watu wake anatumia responsibility kuwasifia kuwa wanafaa. . . .Kajificha kama mbuni na wishful thinking zake na akitoka huko anataka ramani iwe nyumba by a simple wink. . . . . .Ishi uhalisia. . . .

Nakuuliza tena criteria/features za mtu asiye wa kawaida tu mkuu
 
Hivi kwa busara kidogo tu,hicho unachoita ufisadi wa Mbowe kingekuwepo, akina Mwigulu na Nape wasingekishikia bango au wangepoteza muda wao kuzusha kesi za ugaidi?

Kwani kushikia bango lazima utamke kwa mdomo wako, unajua smiling killers??!! Anavujisha mambo yako tu na jioni mnakunywa chai taratibu ukiwa naye, check the game carefully sio kila saa lazima ubwatuke ndio uonekane. . . . .Multiple fronts approach
 
Sahihi mkuu,unajua tatizo baadhi yetu tunakaa kwenye vijiwe na yanapouzwa magazeti tunapewa story zisizo na kichwa wala miguu tunaanza kuzi expose bila evidence wala kuzifanyia tafiti,na mbaya unakuta mpaka mtu aliye na elimu ya chuo bado anaongea ujinga,while alipaswa kuelimisha jamii,hongera kaka,let us be fair tukiwa na story za kutaka tu umaarufu uonekane unajua mambo mbele ya wasiojua,hujengi,eleza ukweli,fundisha watu waujue ukweli,si mapenzi yako kwa fulani basi unataka yawe hivyo na wote wayakubali
 
Watanzania ni watu wamezoea 'Average Life' na 'ujanjaujanja' ndo maana mtu kama Magufuli aliyetimiza wajibu wake tunamuona kama mungu mtu, tunamuona jembe.
Wafuata mkumbo wengi wanaona Magufuli jembe wakati alikuwa anatimiza wajibu wake.
 
Tanzania kama nchi tuna tatizo kubwa. Kwa vile ubabaishaji,uzembe, ufisadi na uovu mwingine kama huko umezoeleka mno,nasi akitokea kiongozi anayetekeleza majukumu kama yalivyotanabaishwa katika duties&responsibilities au person specifications za wadhifa husika, anaonekana kama malaika.

Na hiki ndo kinachotokea sasa: Magufuli kuonekana kama mchapakazi hodari atakayeweza kuinusuru Tanzania yetu. Hatuwaoni madaktari/manesi kuwa wachapakazi hodari kwa kutimiza majukumu ya kazi zao na kuokoa maisha yetu, wala hatuwaoni walimu wachapakazi hodari kwa kufika mashuleni na kufundisha (tena Mara nyingi katika mazingira magumu) lakini Magufuli akifanya japo robo ya kazi anayolipwa mshahara mnono kuitekeleza, anaonekana kama malaika.

Ni kwamba tunatarajia ubabaishaji, uzembe,ufisadi,nk kiasi kwamba kuwajibika ambako ni wajibu kwaonekana muujiza.

In fact, the so-called uchapakazi wa Magufuli ni ku-meet expectations za mwajiri wake, ambaye essentially ni wewe mlipa kodi. Lakini expectations sio exceptions. Twawajua wanasiasa wachache tunaoweza kuwaita exceptional, na Magufuli si mmoja wao, unless tushushe bar na kumpima kwa lens ya ubabaishaji,uzembe na ufisadi ambao ndo trademark ya wanasiasa wa CCM.

Je Magufuli ana courage ya kumbana Riz na washirika wake wanaoibaka Tanzania yetu day in day out? I don't think so. And by the way, urafiki wake na JK waweza kumfanya Jk akabaki 'Rais by proxy', akaongoza nchi kwa remote control, akawa de-facto president kama walivyokuwa Lowassa na Rostam at one time, na Kinana most of the time.

Rais tunayemhitaji ni atakayeingia Ikulu na kupitia utendaji wa mtangulizi wake si kwa minajili ya visasi au kukomoana Bali kuwezesha a fresh start. All I can see in Magufuli ni business as usual, simba wa makaratasi kama JK.

Anyway, one good thing about JF ni kuwa kama archive ambayo huko mbeleni twaweza kukumbushana haya akina sie twayabashiri mapema.

Time will tell.
Dah
 
Back
Top Bottom