Magufuli ni Rais wetu, asiabudiwe, asiogopwe, bali aheshimiwe

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,668
119,281
Wanabodi,

Kufuatia kazi nzuri inayofanywa na rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kuna baadhi ya watu wanamkubali sana hadi kufikia kiwango cha kama kumuabudu fulani!, na humu JF, nimenote modes wa JF nao wanaanza kufuata mkumbo, sio tuu wa kumuogopa rais Magufuli, bali sasa na wao ni kama sasa wanataka kama kuanza kumuabudia fulani hivi!.

Kama mtakumbuka kuna wakati rais Kikwete alipokuwa akiandikwa jina la JK, au Vasco, modes walibadili hiyo title na kuandika Jakaya Kikwete, kwa hoja kuwa kumuita rais JK, ni kumdharau na kumvunjia heshima!.

Hili sasa limeanza kujitokeza kwa rais Magufuli, ukiandika neno Magufuli ni dikiteta, kwenye headlines, hilo neno dikiteta litaondolewa na modes!. Udikiteta sio tusi, ni hulka tuu ya mtu, kulazimisha wote kufanya mambo anayotaka yeye, kwa namna ambayo inakwenda kinyume cha katiba, sheria, taratibu na kanuni, kama mtu una hulka hiyo ya udikiteta, ni hulka tuu ya dikiteta, na sio kitu kibaya kivile. Hivyo kitendo cha modes kuwazuia members humu kuisema hulka hii ya udikiteta wa rais wetu, huku sasa ni ama kumuogopa, ama ni kama kutaka kumuabudia fulani!.

Magufuli ni rais wetu, tumemchagua wenyewe kwa kura zetu kwenye uchaguzi huru na wa haki, hivyo yeye kama rais wetu na kiongozi wetu Mkuu, anapaswa kuheshimiwa, na sio kuabudiwa hadi kuogopwa hivi kwa vile yeye sio Mungu kusema aabudiwe. Haya ya watu kumkubali sana rais Magufuli, na kumuogopa sana hadi kuonekana kama ni kumuabudia, ikitokea watu kumuabudia kweli kutokana na kumkubali sana, wanawaza kujikuta, kwa kumwabudu, wanamponza bure rais Magufuli. Wakuabudiwa ni Mungu pekee, binadamu hata afanye mambo mazuri, makubwa vipi, asiabudiwe!. Huko mbele ya safari, tunaweza kujikuta tutakuja kumponza bure bila sisi kujijua!.

Rais Magufuli ni rais wetu na kiongozi wetu Mkuu, yeye sio malaika kusema hakosei, rais Magufuli ni binadamu mwenzetu kama sisi, hivyo katika utekelezaji wake wa majukumu ya kila siku, japo anafanya mambo mengi, makubwa na mazuri kwa taifa letu, lakini na yeye kama binadamu mwingine yoyote, anaweza kufanya makosa ya kibinaadamu, hivyo kuna makosa ya kibinaadamu ambayo rais wetu anayafanya kufuatia hulka yake ya udikiteta!, modes msiwazuie members humu kuyajadili kumuita rais Magufuli dikiteta kwa sababu hivyo ndivyo alivyo, hiyo ni hulka yake, na Tanzania hapa tulipofika, tulihitaji mtu mwenye hulka hiyo ya udikiteta fulani ili aweze kuing'oa mizizi ya rushwa, ubadhirifu, ufisadi na uzembe ulioota mizizi katika jamii yetu.

Udikiteta uko wa aina mbili, kuna udikiteta mbaya na katili, "ruthless dictatorship" kama Hitler, na Udikteta mwema, " Benovelent Dictatorship" ambao ni mzuri. Huu udikiteta wa rais Magufuli ni udikiteta mwema, udikiteta mzuri, ila hata wale ma ruthless dictators kama Hitler, nao walianza hivi hivi, kidogo kidogo na kwenda mdogo mdogo mwishowe ndio wakageuka, hivyo huu udikiteta wa rais Magufuli ukizidi and if left unchecked, huko baadaye utakuja kutuletea matatizo kama taifa. Hivyo waacheni watu waseme, mwisho wa siku, there is a chance atasikia na kubadilika kuliko kunyamaza au kuwazuia watu kusema!, mwishowe akaja kuwa dikiteta kamili!.

Juzi nilipandisha uzi ulianzia na neno Japo ni Dikiteta ....Magufuli ni ..... modes waliliondoa neno Dikiteta!. Hata kama kwenye contents nilisema udikiteta wake ni benovelent, lakini bado neno dikiteta kwenye headline liliondolewa!.

JF tuendeleze ile spirit yetu ya "we dare talk openly" as long as we speak the truth!, hatumtukani mtu, hatumkashifu mtu, bali tunasema ukweli wa jinsi mtu ulivyo.

Rais wetu ni kiongozi wetu, sio bosi wetu wote, rais ni bosi wa watumishi wa serikali na watumishi wa umma na wote aliowateua na viongozi, lakini kwa upande wa sisi wananchi wa kawaida, sisi ndio mabosi wa rais, sisi ndio tumemuajiri rais kwa kura zetu ili atutumikie, hivyo rais ni mtumishi wetu, na sisi ndio ma boss tunaemlipa mshahara wake yeye na serikali yake kwa kodi zetu, tena mshahara wake haukatwi kodi!, hivyo tuna uhuru na mamlaka ya kusema lolote kuhusu rais wetu na serikali yake as long as hatuja vunja sheria yoyote na bila kukiuka uhuru wake wa faragha, the right to privacy. Neno dikiteta ni tile halali!, modes msiizuie!.

Nawatakia Jumapili njema, na juma Takatifu jema.

Paskali
 
Nimekuelewa Sana Pasco,Slogan ya JF iendelee kusimamiwa na Moderators ili mradi hakuna aliyetukanwa wala kuvunjiwa heshima.
 
Wanabodi,

Kufuatia kazi nzuri inayofanywa na rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kuna baadhi ya watu wanamkubali hadi kufikia kiwango cha kumuabudu!, na humu JF, nimenote modes wa JF nao wanaanza kufuata mkumbo, sio wa kumuogopa rais Magufuli, bali nao kutaka kumuabudu!.

Kama mtakumbuka kuna wakati rais Kikwete alipokuwa akiandikwa JK, au Vasco, modes walibadili hiyo title na kuandika Jakaya Kikwete, kwa hoja kuwa kumuita rais JK, ni kumvunjia heshima!.

Hili sasa limeanza kujitokeza kwa rais Magufuli, ukiandika neno Magufuli ni Dikiteta, kwenye headline, hilo neno Dikiteta litaondolewa na modes!. Udikiteta ni hulka ya mtu, kama mtu una hulka hiyo, kitendo cha modes kuwazuia members kuisema hulka ya rais wetu, huku ni ama kumuogopa, au kutaka kumuabudu!.

Magufuli ni rais wetu, hivyo kama rais anapaswa kuheshimiwa, na sio kuogopwa!. Magufuli licha ya kuwa rais wetu na kiongozi wetu mkuu, lakini yeye sio Mungu, na sio malaika, ni binadamu kama sisi, hivyo katika utekelezaji wake wa majukumu, japo anafanya mazuri mengi, lakini kama binadamu pia kuna makosa anayafanya kufuatia hulka yake ya udikiteta!, modes msiwazuie members humu kumuita Magufuli dikiteta kwa sababu hivyo ndivyo alivyo, hiyo ni hulka yake, na Tanzania hapa tulipofika, tulihitaji mtu mwenye hulka hiyo ili aweze kuingoa mizizi ya rushwa, ubadhirifu, ufisadi na uzembe ulioota mizizi katika jamii yetu!.

Juzi nilipandisha uzi ulianzia na neno Japo ni Dikiteta ....Magufuli ni ..... modes waliliondoa neno Dikiteta!. Hata kama kwenye contents nilisema udikiteta wake ni benovelent, lakini bado neno dikiteta kwenye headline liliondolewa!.

JF tuendeleze ile spirit yetu ya "we dare talk openly" as long as we speak the truth!.

Rais wetu sio bosi wetu, ni bosi wa watumishi aliowateua na viongozi, lakini kwa sisi wananchi wa kawaida, sisi ndio mabosi wa rais, sisi ndio tumemuajiri kwa kura zetu ili atutumikie, na sisi ndio tunaemlipa mshahara wake kwa kodi zetu.

Nawatakia Jumapili njema, na juma Takatifu jema.

Pasco
Nikweli moderator wa JF wanaboa sana sikuhizi, sio katika post tu, Unaweza ukaanzisha thread ikapotezwa lakini thread kama hiyo ikaanzishwa na mtu mwingine ikawepo....JF ibaki katika ubora wake
 
Pasco kumbe na wewe ulimuajiri Magufuli kwa kura yako? Halafu kuna watu wanadai kura za Lowasa ziliibiwa. Wenye akili wengi ndani ya CHADEMA tulimwajiri Magufuli kwa kura zetu, maana tulijua Magufuli ndiye anayeweza kutekeleza sera za CHADEMA(ile ya Dr Slaa) kwa vitendo. Umeongea vema sana Pasco kwa hali tuliyokuwa tumefikia Tanzania tunahitaji dikteta kuturudisha kwenye mstari. Rwanda walifanya hivo - Tumeona dikteta Kagame anavyoijenga kwa spidi nchi yake.
 
Ukiwa na mtazamo wako kuwa rais ni dikteta haimaanishi ndio dikteta kweli kwa maana mtazamo waweza kuwa tofauti na watu wengine
Mimi ninavyoona kuna watu wamepaniki kutokana na utendaji na maagizo anayotoa mh rais hii inatoka na kulelewa miaka 10 na mzee wa msoga.... Hadi wakalemaa na kuamini hakutatokea rais mwenye maamuzi ya bila kuunda kamati na michakato ktk kushugulikia wazembe na wabadhirifu ya mali za umma
Ila naamini itafika muda mtamwelewa tu maana toka aanze kazi ni miezi 5 tu
 
Uwezi kumtukana rais wa nchi alafu watu wakuache tu.

Unajua kuna watu wana matatizo.Utamwitaje mtu dictator aliyechaguliwa kwa kura na wananchi?
Halafu mtu anaamka tu anasema Magufuli dictator!

Pasco mwanzisha hii maada ana tatizo. Nafikiri kuna kitu kikubwa mno alipoteza kwa Lowasa kushindwa uchaguzi.Katika watu ambao wako bitter hadi leo ni PASCO.Kuna siku niliandika kuwa huyu PASCO anahitaji ushauri wa kisaikolojia kaathirika kichwani tena sana.Sio Pasco tuliyekuwa tunamjua Jamii Forums.
 
Pasco kumbe na wewe ulimuajiri Magufuli kwa kura yako? Halafu kuna watu wanadai kura za Lowasa ziliibiwa. Wenye akili wengi ndani ya CHADEMA tulimwajiri Magufuli kwa kura zetu, maana tulijua Magufuli ndiye anayeweza kutekeleza sera za CHADEMA(ile ya Dr Slaa) kwa vitendo. Umeongea vema sana Pasco kwa hali tuliyokuwa tumefikia Tanzania tunahitaji dikteta kuturudisha kwenye mstari. Rwanda walifanya hivo - Tumeona dikteta Kagame anavyoijenga kwa spidi nchi yake.
Mkuu Chintu, matokeo ya uchaguzi, yanahesabiwa kwa collective responsibility ya the winner takes it all.

Kama wamepiga kura watu 21, mshindi akapata kura 11, aliyeshindwa akapa kura 10, mshindi na mshindwa wamepishana kwa kura 1, matokeo yakiishatangazwa kuwa fulani kashinda, then huyo aliyeshinda ni mshindi wa wote, waliomchagua, na wasiomchagua!.

Kwenye uchaguzi wetu, kuna watu walimchagua Magufuli, kuna watu walimchagua Lowassa, na kuna watu waliwachagua wagombea wengine. Baada ya matokeo kutangazwa kuwa Magufuli ndiye aliyeshinda, then Magufuli ndie rais wa wote, waliomchagua na wasio mchagua na hata wale ambao hawakupiga kura, ambapo collective responsibility ni sisi Watanzania katika ujumla wetu, ndio tuliomchagua Magufuli, msharahara, ni sisi Watanzania wote tunamlipa mshahara katika umoja wetu!. Yeye ndio rais wa Lowassa, ndie rais wa UKAWA, ndio rais wa nchi, na ndie ais wetu!.

Pasco
 
Unajua kuna watu wana matatizo.Utamwitaje mtu dictator aliyechaguliwa kwa kura na wananchi?
Halafu mtu anaamka tu anasema Magufuli dictator!

Pasco mwanzisha hii maada ana tatizo. Nafikiri kuna kitu kikubwa mno alipoteza kwa Lowasa kushindwa uchaguzi.Katika watu ambao wako bitter hadi leo ni PASCO.Kuna siku niliandika kuwa huyu PASCO anahitaji ushauri wa kisaikolojia kaathirika kichwani tena sana.Sio Pasco tuliyekuwa tunamjua Jamii Forums.
kiukweli humu JF tuna mijitu mijinga ajabu!. Kazi yao ni kujikombakomba tuu kwa viongozi ili waonekane ndie wenye uchungu na nchi hii.
Moja ya majinga haya ni lijinga hili linalodhani mtu akichaguliwa hawezi kuwa dikiteta!. Ungefanya utafiti ni madikiteta wangapi waliingia madarakani kwa kuchaguliwa!.

Udikiteta ni hulka ya mtu, na hakuna ubishi kuhusu udikiteta wa Magufuli!. Kitu muhimu sio ni dikiteta au laa, kitu muhimu ni "the motive behind udikiteta huo!", nimesema Magufuli ni dikiteta, ila ni Benovelent Dictator, ungekuwa sio lijitu lijinga, ungeangalia kwanza maana ya neno benevolent, na kuangalia benevolent dictator, ni dikiteta wa aina gani na anafanya nini!.

Kwa kukusaidia tuu, with simple reference, Magufuli ni dikiteta, na huu udikiteta, hakuuanza leo baada ya kuwa rais wa JMT, alikuwa ni dikiteta tangu zamani akiwa Waziri wa Mifugo, aliikamata meli moja ya uvuvi kwenye bahari yetu na kutaifisha kila kitu wakiwemo wale samaki maarufu kwa jina la samaki wa Magufuli. Tanzania tulishindwa kesi, na wenye meli wameshinda kesi katika mahakama ya kimataifa, Tanzania tunadaiwa mabilioni ya fidia!, hizo Airbus tutakazo nunua za ATC, mwisho wake ni kuruka ndani ya bongo, zikikanyanya tuu anga za kimataifa, ikitua ndio imefika, unless tulipe!.

Akiwa Waziri wa Ujenzi, aliamuru kituo fulani cha mafuta kule Mwanza kivunjwe ili barabara ipite, kituo kilivunjwa na kabla barabara haijapita, mwenye mali akafungua shauri mahakamani, akashinda, serikali imelipishwa fidia mabilioni, tumelipa na barabara imepinda kukikwepa kituo hicho!.

Inategemea huo udikiteta anaufanya kwa nia gani!, Tanzania tumefika mahali tunamhitaji kiongozi wa type ya Magufuli, punda haendi shurti kwa mijeledi!. Rushwa, ufisadi na uzembe, uliota mizizi kwenye jamii yetu!. Kulihitaji mtu jasiri na katili mwenye uwezo wa kutumbua majibu bila kujali maumivu watakayoyapata wanaotumbuliwa kwa sababu lengo ni kulitibu taifa letu, hivyo Magufuli ni Benevolent Dictator nchi ya Tanzania iliyomhitaji na kumsubiria kwa kipindi kirefu, hatimaye sasa tumempata!.

Paskali
 
Back
Top Bottom