Magufuli ni FDR wa Tanzania

Magufuli ni FDR wa Tanzania

Joined
Mar 3, 2018
Posts
75
Reaction score
800
Na Elia F Michael.

Baada ya kile kinachoitwa Great Economic Depression cha mwaka 1929-33 kuipiga Marekani na Ulaya alitokea Rais pale Marekani wa 32 aliyekuwa anaitwa Franklin Delano Roosevelt (FDR) ( 1882-1945) kutoka chama cha Democrat.

Ni Rais wa Marekani ambae alikutana na hali mbaya ya kiuchumi kwenye Nchi yake kipindi ameingia madarakani kwasababu alikuta mporomoko mkubwa sana wa kiuchumi. Ili kurudisha uchumi vizuri katika Taifa hilo jeuri Duniani alikuja na mpango uliojulikana kama "NEW DEAL"

"NEW DEAL" ilikuwa imesheheni mambo mengi ya kurudisha uchumi vizuri. Moja ya vitu ambavyo vilikuwa vimepewa kipaumbele katika Mpango huo ilikuwa ni kuweka mkakati wa kuzalisha umeme kwenye bonde la Mto Tennessee chini ya programme iliyojulikana kama "TENNESSEE VALLEY AUTHORITY" (TVA).

Kwanini TVA?
Makampuni binafsi ya kuzalisha umeme Marekani yalikuwa yanauza umeme kwa gharama za juu sana kwa Raia wakati huo yeye alitaka hali za watu ziwe vizuri na serikali yake ipate umeme wa uhakika kwa Wakati huo.

TVA ni wazo ambalo FDR alilipata kwa kiongozi moja wa Jimbo la NEBRASKA kwa wakati huo jina ni George William Norris. Franklin alifurahi sana hadi akamuita kiongozi huyo kuwa ni "THE PERFECT GENTLEMAN OF AMERICAN PROGRESSIVE IDEALS"

Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi huo familia zaidi ya 15,000 ziliondolewa maeneo ya makazi ili kupisha ujenzi. Kama mjuavyo kila jambo zuri lazima liwe na gharama zake na wabaya wa maendeleo hupitia kwenye gharama za jambo jema.

Makampuni binafsi ya kuzalisha umeme yalianza kutembea hadi usiku kushawishi wale watu waukatae mradi kwasababu walihamishwa maeneo yao. Watalaam pia wa Environment Impact Assessment wakawa na yao kama inavyofanya UNESCO kwenye mradi wetu wa mto Rufiji.

Baada ya mwaka mmoja tayari mradi huo ukawa tayari umezalisha ajira Zaidi ya 9000 kipindi cha ujenzi wake na hata ulipokamilika gharama za umeme zilishuka sana na Viwanda vikawa vimepata nguvu tena ya kuendeshwa kwa umeme unaofuliwa kwenye maji na hali ikawa nzuri kuanzia ndani ya nyumba za Raia hadi mashambani.

FDR ni Rais pekee aliyeiongoza Marekani zaidi ya mihula "2" kutokana na mafanikio katika utawala wake yaani 1933-1937,1937-1941 na 1941-1945 kwa hiari ya Wamarekani mbali na kuwa ni kinyume na Katiba yao lakini wao wanasema " Americans does what is in their best interest "
Katika hili hakuna aliyewakosoa wala hawakujikosoa maana walikunwa na uongozi wa Mmarekani mwenzao!

NEW DEAL YA RAIS MAGUFULI NI IPI?
1. Mradi wa umeme katika maporomoko ya Stiegler mto Ruvu "STIEGLER'S GORGE" kwa gharama ya Tsh 6.5T.

Mradi huu unafanana na ule wa Marekani wa TVA.

2. Ujenzi wa Reli ambayo treni ya mwendokasi itapita "SGR" Kwa Tsh .2.7 T.
Itaweza kusafirisha mzigo wenye uzito wa Tani Million 17 na kusaidia kuingiliana na Mataifa ya Burundi,Kongo na Uganda.

3. Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Tanga kwa Tsh 8T.
Bomba hilo linapita Vijiji vya Tanzania zaidi ya 180, Wilaya 24 na Mikoa 8 na itasaidia Bandari ya Tanga kuingiza kipato Kingi kwa Tanzania.

Sijasahau Makutano ya Barabara ya Nyerere na Mandela eneo la TAZARA kwa Tsh 95 Billion.

Morogoro road na Mandela ( Ubungo interchage) kwa Tsh 188.1.
Agha kan+ Coco beach ( Salenda) 250Billion.

Kakonko pia kuna ya Rais Magufuli.

Ujenzi wa Jengo la Halmashauri Bil.2.6

Kakonko Bus Stand Bil 2.3.
Miradi ya maji Bil 1.92

Soko la Kimataifa Mpakani Muhange na Burundi Mil 574,181,200.
Barabara ya Nyakanazi-Kabingo Km50.

Kuelekea Miaka 4 ya Rais Magufuli nimeona nikumbushe hayo na kisha niwaache muamue. Mkijisikia kuamua kama Mimi kumfuata alipo Huyu Mzalendo basi karibuni maana wanasema Waswahili kuwa kumuunga Mkono Mzalendo sio dhambi kwani tunalindwa na Katiba ambayo na Mungu anaitambua.

Elia F Michael.
Kakonko Buyungu Tanzania.
Mbunge nje ya Bunge.
 
GIFTED FOOL
Wenzako walimu unga mkono kabla ya hivyo vitu vya stiglers gorge na SGR

Wewe mnafiki ulikuwa wapi?

Njaa inayoanzia kichwani kuelekea tumboni inakusumbua

Hata wewe kuna watu walikuunga mkono kabla hujawa diwani

Njaa, Njaa njaa mbaya sana

You are certified idiot of Nov 2019

Njaa inakufanya uuze utu wako, Njaa imekufanya ufe kifikra huku ukisubiri mwili wako kuzikwa

Huna point zaidi ya Propaganda za kutafuta cheo CCM
 
Roosevelt alikuwa akishauriana na viongozi wenzie kama Churchhill na wengine wa ufaransa ila huyu kajifungia kwake. Rosservet alipigana vita ya pili ya dunia na akiwa hatembei sababu ya polio.

Ukienda kwenye nyumba utaona hata alitengenezewa train ya kumtembeza lakini alikuwa sane and smart. Hakutoa maamuzi kwa jazba na nyuma yake ni mke wake Eleanor ndo alikuwa nguzo yake. Compare and contrast.

Roosevelt hakujenga uwanja wa ndege Connecticut maana alijua kuna JFK na viwanja vingine vidogo around.
 
Kwa hiyo "THE PERFECT GENTLEMAN OF TANZANIA PROGRESSIVE IDEALS" ni Makonda anayemshauri kukamata/kuteka matajiri ili wakombolewe kwa fidia mpate fedha za kugharimia miradi!?
 
Kitu kimoja tu naweza kumsifu Magufuli ni kwamba anajua kucheza na akili za wenye njaa na tamaa ya madaraka.

Kitu Magufuli tutamkumbuka ni kwamba atatusaidia kutuonyesha wanasiasa njaa, atawapa majukumu na atawatupa nje huko na hapo ndio atakuwa amesaidia kutuchimbia kaburi la kuwazika.

Rais Magufuli anajua kabisa yeye kwenye siasa za ushindani kwa mujibu wa katiba yetu anastaafu rasmi ila sasa hawa wanaomsindikiza kuelekea kustaafu kwake ndio wataadhibika vibaya mno wakati wakirudi Chato baada ya nyimbo za kusifu kukoma.

Magufuli akiondoka yeye mtatafuta chaka lingine na hapo ndio itakuwa hitma na kuanua matanga tu.
 
Hivi ukiwa unamuunga mkono rais ni lazima uwe taahira, yaani itafikia hatua hata rais akinya watu watampongeza kwa kunya mavi yanayonikia viziri.

Mradi wa bomba la hoima unaouongelea wewe ni upi? Ule uliokufa au mwingine? Vijana mnaotaka uteuzi mnapotaka kumsifia rais ambalo mi jambo jema mjitahidi kua na hoja za msingi na sio hisia.
 
Hivi huyu ni yule wa Buyungu? Mbunge nje ya bunge ama?
Hivi ukiwa unamuunga mkono rais ni lazima uwe taahira, yaani itafikia hatua hata rais akinywa watu watampongeza kwa kunya mavi yanayonikia viziri.

Mradi wa bomba la hoima unaouongelea wewe ni upi? Ule uliokufa au mwingine? Vijana mnaotaka uteuzi mnapotaka kumsifia rais ambalo mi jambo jema mjitahidi kua na hoja za msingi na sio hisia.
 
NEW DEAL YA JPM NI IPI?
Ungenipa chaguo nichague kwa utashi wangu bila ya shurti, ningekwambia "NEW DEAL ya "FDR" ilikuwa ni 'DEAL' kwelikweli .
Umeeleza vizuri sana hiyo sehemu iliyomhusu FDR. Ninachojua, kuwepo kwa DEAL hilo haikuwa sababu ya kuwaondolea waMarekani HAKI zao za msingi, na wala hapakuwepo na sababu ya kufanya hivyo. Upande huu ndio nyinyi mnaopenda kulinganisha hampendi kabisa kuugusia, kwa nini?

DEAL letu kama unavyolieleza katika sehemu ya pili lingenoga sana bila ya haya makandokando yasiyokuwa na sababu za kuwepo.
Na hiyo 'mihura' zaidi ya miwili unayoiingiza humu kwenye mada, isingekuwa na shida ya kuifikiria na wala kuilazimisha kama mnavyoanza kuipigia chepuo wakati huu.
Hapa kwetu, DEAL letu tutalazimishwa, kama tunavyolazimishwa sasa hivi kuhusu serikali za mitaa.

Ukipata muda, jaribu kuelezea jinsi gani FDR alivyowalazimisha waMarekani wampe hiyo ngwe yake ya ziada mnayomtafutia sasa hivi JPM kwa njia yoyote iwayo - hiari yetu au bila hiari; na juhudi kubwa alizokuwa akizifanya kuwakandamiza Republicans kwa nia ya kuwaondoa kama chama cha siasa.
Usikose kuyachambua hayo ili mlinganisho wako wa FDR na DEAL lake, na JPM na DEAL letu. Umenielewa?
 
Back
Top Bottom