Leo ni siku muhimu kwa wana-Karatu kumsikiliza mgombea wa CCM,Mh JP Magufuli atakapohutubia hapa mjini muda wa mchana kuanzia saa 8. Mwishoni mwa wiki iliyoisha mgombea wa CDM aliwapigisha jua na vumbi wananchi wa Karatu baada kutangaziwa kuwa atatua hapa,lakini hakutokea kwa kushindwa kukamilisha ratiba aliyopangiwa. Mbowe angebanwa awaeleze alikompeleka Dr Slaa.
Leo wananchi wanajiuliza kama huyu wa CCM naye atatiza ahadi yake ya kuongea nao. Karatu ni sehemu ambayo wenyeji wako makini na miadi,hawapendi kudanganywa wala kudharauliwa. Ni vigumu kusoma upepo wa kisiasa hadi dakika za mwisho. Maandalizi yanaendelea uwanja utakaotumika kwa shughuli hiyo.