Magufuli na Raila Odinga wataiharibu EAC

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,186
9,287
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli (JPM) ni rafiki mkubwa wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya na Kiongozi wa Upinzani nchini humo, Raila Amolo Odinga (RAO). Wawili hawa wameanza kuwa marafiki miaka mingi iliyopita lakini urafiki wao ulishamiri sana miaka ya 2005 – 2015, JPM akiwa mmoja wa mawaziri wenye nguvu na ushawishi hapa Tanzania.

Kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa nchini Kenya mwaka 2012, JPM alishiriki kampeni za ODM akimuunga mkono Raila Odinga dhidi ya mpinzani wake kutoka muungano wa JUBILEE, Uhuru Kenyata, ambaye kwa sasa ndiye rais wa Kenya. Kalamu ya leo inagusia uhusiano wa JPM na RAO ili kuhitimisha kuwa upo uwezekano wa EAC kutikisika kwa sababu ya ukaribu wa viongozi hawa.

Kwanza inapaswa kufahamika kuwa kila kiongozi anao marafiki na ndugu zake na siyo rahisi kuwabadilisha pale anapokuwa ana dhamana kubwa zaidi ya uongozi. Tatizo linaloweza kujitokeza huwa ni pale ambapo kiongozi “A” anakuwa na rafiki yake mkubwa sana kutoka nchi “Y” urafiki huu unaanza wakati ambapo kiongozi “A” ana wadhifa mdogo.

Siku moja kiongozi “A” anakuwa kiongozi mkubwa wa nchi “X” ambayo inapakana na nchi “Y”. Kwamba kiongozi “A” anajikuta bado yumo kwenye ukaribu mzito na rafiki yake kutoka nchi “Y” ambaye kwa wakati husika (rafiki) ni mpinzani mkubwa wa kiongozi mkuu wa nchi “Y” ambayo iko jirani na nchi “X” na zote zina jukumu la kuimarisha uhusiano wa viongozi wa juu na uhusiano wa nchi zote mbili! Kama tutasema ukweli, katika siasa za Afrika na duniani, ni rahisi sana kumchukulia rafiki ya adui yako kama adui yako.

Kwamba mtu ambaye ni hasimu yako na anashinda na kujifungia chumbani na mtu anayepaswa kuwa rafiki yako, sijui utawezaje kujiamini na kupanga mipango sawasawa na huyu anayepaswa kuwa rafiki yako wakati ni rafiki wa hasimu yako. Bila shaka kwa ngazi za intelijensia ya dunia, huwenda makachero wa Kenya na ambao kwa sasa wana kazi ya kulinda “legacy” ya Uhuru Kenyatta kisiasa, watakuwa wanahaha na kujaribu kuchora kila “utabiri” wa nini kinaweza kuwa kinaendelea kati ya JPM na RAO.

Ikumbukwe kuwa uchaguzi mkuu wa Kenya upo tena mwaka 2017 na mahasimu wakubwa katika uchaguzi huo ni UHURUTO (Uhuru Kenyatta na William Ruto wa JUBILEE dhidi ya RAO wa ODM). Sasa ikiwa rafiki wa karibu wa RAO (yaani JPM) alimpigania na kumnadi RAO kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2012 kwenye majukwaa ya siasa za Kenya (wakati huo akiwa Rais) na leo amekuwa mkuu wa nchi, nini kinaweza kutokea? Huwenda makachero wa Kenya wakamtahadharisha Kenyatta kuwa JPM atamsaidia RAO kisirisiri hasa kwenye eneo la nguvu kazi (raslimali watu) na fedha.

Huu utakuwa ni utabiri wa maana sana kwa mwanasiasa yeyote na hautapuuzwa, Kenyatta ataupokea na kujipanga kadri awezavyo. Wakati Kenyatta akijipanga kuelekea 2017 huku akitiwa hofu kuu na ukaribu wa JPM na RAO tutegemee lolote, tutegemee kuwa uhusiano wa Kenyatta na JPM hautakuwa mzuri sana katika kipindi hicho kwa dhana ile ile ya mtu anayepaswa kuwa rafiki yako, unapogundua ni rafiki mkubwa wa hasimu wako lazima umshtukie haraka ili usije kuingia kwenye mitego usiyoijua.

Najua sote tunaikumbuka vita ya Uganda. Vita hii inaligharimu taifa letu hadi leo, uchumi wetu umewahi kuporomoka katika historia yake yote kwa sababu ya vita hii. Unajua moja ya chanzo chake? Ukiachilia mbali suala la Idd Amin na uamuzi wake wa kujitangazia kuwa sehemu ya ardhi yetu ni ya kwake, ukweli ni kuwa “Urafiki kati ya Nyerere na Milton Obote” ulikuwa kichochezi kikuu cha vita ile.

Mwalimu Nyerere alijua Idd Amin ni dikteta wa kutupwa na aliamini swahiba wake, Obote, angeliweza kutoa uongozi wa maana Uganda na kulifanya eneo lote la Afrika Mashariki libaki kuwa salama, kama angelirejea madarakani. Na kwa sababu Obote alipopinduliwa alikimbilia Tanzania na kupewa hifadhi na Nyerere huku akiweka kambi ya kijeshi hapa Tanzania kwa maana ya kujipanga kurejea madarakani kwa kumuondoa Amin, tunaweza kukubaliana kuwa Idd Amin alikuwa na kila sababu ya kutuletea chokochoko.

Kwanza ni kwa sababu tulimhifadhi hasimu wake mkubwa kabisa na mtu ambaye kama Idd Amin angelikutana naye hata ndotoni, angelimtoa roho. Pili tulikuwa tunamsaidia Obote kujipanga kuivamia Uganda kijeshi akiwatumia wanajeshi wa Uganda waliokuwa wanamuunga mkono.

Ndiyo maana pamoja na kuwa OAU (wakati huo) iliweka juhudi kubwa kutatua mzozo ule ili kuepusha vita, Tanzania iliamua kuingia vitani ili kumpiga Idd Amin na kurejesha amani na utulivu Uganda. Japokuwa katika mipango ya Mwalimu Nyerere nadhani pia alipenda Idd Amin aondoke ili rafiki yake kipenzi, Obote, arejee madarakani. Baada ya vita ya Uganda na tulipofanikiwa kumuondoa Idd Amin na kumuweka Obote, hakukaa muda mrefu, akapinduliwa, akakimbilia Zambia mpaka kifo kilipomkuta miongo miwili baadaye.

Mfano wa vita ya Uganda ni maelezo ya hali halisi ya nini huwa kinaweza kutokea ikiwa viongozi wa juu wa nchi jirani wakiwa hawaaminiani. Jambo dogo sana likitokea linakuzwa na kushtukiwa kwa kasi na uzito mkubwa, ndiyo maana serikali ya Kenya na muungano wa JUBILEE kwa vyovyote vile watakuwa wanafuatilia kwa karibu sana uhusiano wa JPM na RAO.

Na kwa hiyo kama uhusiano huo usipochukuliwa kwa umakini na wahusika (JPM na RAO) huwenda ukateteresha kabisa uhusiano kati ya JPM na Kenyatta na kwa hiyo kisasi cha uhusiano wao mbovu kikahamishiwa kwenye ikulu zetu na hatimaye Tanzania na Kenya zikarejea kwenye uhasama.

Inapotokea kuwa viongozi wakuu wa nchi jirani hawaaminiani kwa kiasi kikubwa, likitokea jambo lolote lile, hata kama ni dogo kiasi gani au lisilokwepeka, kwa kawaida litalazimishwa liaminike kuwa limesababishwa na uhusiano mbovu baina ya wakuu wa nchi.

Mathalani, Kenya na kwa sasa inahaha kutafuta namna ya kurudisha mradi wa bomba la mafuta litokalo Uganda hadi bandari ya Tanga, ambao unasimamiwa na kampuni ya TOTAL ya nchini Ufaransa. Awali, bomba hilo lilikuwa litoke Uganda hadi bandari ya Mombasa, Kenya lakini kwa sababu muhimu za kiusalama wataalamu wakaona lazima lipite Tanzania na kwa hiyo litapaswa kutotumia bandari ya Kenya.

Wakati rais Uhuru Kenyatta anahaha kurudisha mradi huo Kenya na kwa hiyo kuna mvutano kati yake na JPM kwenye mradi huo (inasemekana hadi Kenyatta amekwenda kukutana na rais wa Ufaransa), ni wakati huo huo ndipo RAO na JPM wanakutana Chato kwa mapumziko ya kifamilia. Kwa hiyo kwa wale wasioujua, makachero wa Kenya lazima kwa namna yoyote ile watamweleza Kenyatta kuwa RAO pia anatumika kuihujumu serikali yake isifanikishe mradi huo ili asije kuupigia debe wakati wa kampeni.

Hili huwezi kulidharau. Mambo yakishafika hatua hiyo ndipo huwa marais wa nchi jirani wanakosa maelewano kabisa na nchi zinaingia kwenye migogoro ya kidiplomasia. Kwa hakika, ukaribu wa JPM na RAO lazima utizamwe kwa jicho la tatu. Lazima mtu avae viatu vya Uhuru Kenyatta kisha akae ikulu ya Kenya na atizame Helikopta ya RAO inavyotua Chato na anavyopolekewa na mahaba makubwa na mtu ambaye Uhuru analazimika kufanya naye kazi kama mkuu wa nchi.

Ama, fikiria kuwa Edward Ngoyai Lowassa (ENL) anatua kwa helikopta kule Ukikuyuni – Kenya, kufanya mapumziko na Uhuru Kenyatta na tena uchaguzi wa Tanzania uko mwaka mmoja baadaye na JPM anahitaji kulinda nafasi yake, moja kwa moja JPM atajua iko mipango ya Uhuru kumsaidia ENL ili yeye (JPM) aangushwe. Na JPM hatamchekea tena Kenyatta.

Haya si mambo ya kutoyapuuza. Hatuwezi kumchagulia rais wetu marafiki na ndugu, lakini tunataka ifahamike kuwa vipo vitisho ambavyo haviwezi kudharauliwa na ambavyo kihistoria vimewahi kuziingiza nchi katika matatizo na migogoro mikubwa ya kidiplomasia na vilikoanzia ni kwenye uhusiano na ukaribu wa mkuu wa nchi moja na mpinzani mkuu wa mkuu wa nchi ya pili. Lazima tufikiri yale yasiyoonekana ili tuyafanye yasije kutokea na kutuathiri.
 
Wakenya walitaka kutuchagulia Lowasa awe Raisi imekula kwao.Daftari la wapiga kura mikoa ya Arusha na kilimanjaro iko haja ya kulipitia upya.Kuna wapiga kura kibao walitokea kenya mbali hadi nairobi kupiga kura na kurudi kwao
 
Huulizi kwa nini TV za kenya na magazeti yalikuwa sanaaaaa na LOWASA!!!!!
tarariaaaaaaaa!!!!!!.

Kenyata na LOWASA ,Magufuli na ODINGA ,ngoma drooo.EAC inaendelea.
Wewe hunaga hoja,kisiasa tunakuita acoders ,we una mahaba mazito na ccm hata kama ikifanya pumba
 
Wakenya walitaka kutuchagulia Lowasa awe Raisi imekula kwao.Daftari la wapiga kura mikoa ya Arusha na kilimanjaro iko haja ya kulipitia upya.Kuna wapiga kura kibao walitokea kenya mbali hadi nairobi kupiga kura na kurudi kwao
Mdogo wangu ukipunguza pumba hadhi yako itarudi
 
Wewe hunaga hoja,kisiasa tunakuita acoders ,we una mahaba mazito na ccm hata kama ikifanya pumba

Michango ya matajiri wa kenya kuchangia KAMPENI ZA Lowasa nashukuru ililiwa na matapeli wa siasa wa Tanzania na imesaidia kuongeza mzunguko wa pesa nchini.Si haba.Kwa hili niwashukuru matapeli wa siasa walioziingiza pesa za wakenya nchini na kuzisambaza kwa madereva wa boda boda,washabiki mbali mbali wa kuzungusha mikono ya mabadiliko nk.

Matapeli mara ingine husaidia uchumi wa nchi.
 
Mbona hadi sasa mnatumbuana ccm kwa ccm hakuna ukawa alietumbuliwa
 
Kwa ufupi,hatuna uhusiano mzuri na wakikuyu.Kwa maana Magu anaonekana kubase sana na upinzani(CORD).Kwa siasa za kenya zilizojengwa katika msingi wa ukabila.Magufuli anaonekana kuwa kipenzi kikubwa cha watu wa asili ya Luo Nyanza,Magharibi(waluhya)wakamba na makabila mengi ya pwani ya Kenya.Ambao kimsingi ni wapenzi wa muungano wa CORD.

Nimekuwa nafuatilia mitandao ya kijamii ya Uhuru Kenyatta.Wakikuyu wengi wanamtazama Magufuli kama threat,mpaka kufikia hatua ya kumtukana.Majina kama ''MAPDOLOCK,mtu wa ushagoo,Pombe''yamekuwa yakitamkwa sana kwenye comment za watu wa central kenya,kwa maana ya WAGIKUYU.
 
Unachosema ni kweli" lkn sasa Magufuli hawezi mkataa Odinga inawezekana Odinga sahv akamuhitaji Magufuli sana kama rafiki na Mshauri"
Sioni shaka labda Uhuru ajishuku maana urafiki wa JPM na Odinga haukuanza leo au ghafla.
Inawezekana Labda Magufuli alimpigia Kampeni Odinga kipindi kile ili Odinga aje amsaide 2015 kipindi JPM anagombania japo ikatokea Odinga akashindwa now ni Time ya JPM kumsaidia Odinga kama rafiki" japo azingatie sana kuwa yy ni Rais.
Hii ndio ile stage inafika unakua hauna namna Magu anajua anajenga image flan kwa Kenyatta lkn atafanyaje na Odinga ni rafiki yke mkubwa.
 
Wakenya walitaka kutuchagulia Lowasa awe Raisi imekula kwao.Daftari la wapiga kura mikoa ya Arusha na kilimanjaro iko haja ya kulipitia upya.Kuna wapiga kura kibao walitokea kenya mbali hadi nairobi kupiga kura na kurudi kwao
Umeota?
 
Kwa uzushi wewe uko katika kiwango cha lami.Huoni hata aibu kidogo?
 
Ushauri mzuri in kweli urafiki uwepo lakini pia lazima Jpm ajenge mahusiano yenye maslahi kwa taiga kwanza kabla ya kupalilia mahusiano binafsi Wakenya kwa ujumla wao ni kaka na Dada zetu,na baba yao kwa sasa ni Uhuru Kenyatta
 
Kwa uzushi wewe uko katika kiwango cha lami.Huoni hata aibu kidogo?
Daftari la wapiga kura Arusha na Kilimanjaro ni jipu la kutumbua.Likipata mtu wa kulihakiki na kuhakiki hao waliomo ndani ya hilo daftari kuna mtu lazima atatumbuliwa.
 
Kwa ufupi,hatuna uhusiano mzuri na wakikuyu.Kwa maana Magu anaonekana kubase sana na upinzani(CORD).Kwa siasa za kenya zilizojengwa katika msingi wa ukabila.Magufuli anaonekana kuwa kipenzi kikubwa cha watu wa asili ya Luo Nyanza,Magharibi(waluhya)wakamba na makabila mengi ya pwani ya Kenya.Ambao kimsingi ni wapenzi wa muungano wa CORD.

Nimekuwa nafuatilia mitandao ya kijamii ya Uhuru Kenyatta.Wakikuyu wengi wanamtazama Magufuli kama threat,mpaka kufikia hatua ya kumtukana.Majina kama ''MAPDOLOCK,mtu wa ushagoo,Pombe''yamekuwa yakitamkwa sana kwenye comment za watu wa central kenya,kwa maana ya WAGIKUYU.
So what are you trying to say,?
 
Unachosema ni kweli" lkn sasa Magufuli hawezi mkataa Odinga inawezekana Odinga sahv akamuhitaji Magufuli sana kama rafiki na Mshauri"
Sioni shaka labda Uhuru ajishuku maana urafiki wa JPM na Odinga haukuanza leo au ghafla.
Inawezekana Labda Magufuli alimpigia Kampeni Odinga kipindi kile ili Odinga aje amsaide 2015 kipindi JPM anagombania japo ikatokea Odinga akashindwa now ni Time ya JPM kumsaidia Odinga kama rafiki" japo azingatie sana kuwa yy ni Rais.
Hii ndio ile stage inafika unakua hauna namna Magu anajua anajenga image flan kwa Kenyatta lkn atafanyaje na Odinga ni rafiki yke mkubwa.
Unafikiri magufuli atakaa bila kumsaidia odinga mwaka 2017
 
Back
Top Bottom