Magufuli na CCM yako acheni kutumia ujinga wa Watanzania kuendelea kujinufaisha na kutawala nchi

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Magufuli na CCM yake na vibaraka wao wa Lumumba buku 7 wanaendelea kuchukua madaraka ya nchi hii kutokana na ujinga wa Watanzania.

Hizo porojo za CCM na Watanzania wajinga kwamba nchi haijaribiwi ni upumbavu na ujinga uliotukuka, CCM imekaa madarakani zaidi ya miaka 60 lakini Bado shida ni zile zile.

Magufuli na CCM yake anapiga porojo kuhusu barabara ambazo sio zinaunganisha nchi au wilaya au mkoa bali zinaunganisha mtaa na mtaa, Magufuli ndani ya utawala wake hakuna barabara yoyote iliyounganisha mkoa na mkoa zote kazikuta na kawadanganya watanzania na ujinga wao eti yeye ndo kafanya juhudi kuzijenga,muongo mkubwa sana huyu John.

Leo baada ya kusomba Wanafunzi na wanakijiji wa Mwakarundi, Isela na mwingineko na kuwajaza pale Kirumba kaanza kuwadanganya kuhusu uwanja wa ndege wa mwanza et kaupanua toka km 2.5 mpaka 3.5 huyu Magufuli muongo mno tangu zamani uwanja wa ndege wa Mwanza run away yake ni ndefu kuliko ya Dar aache porojo na uongo uongo huyu jamaa.

CCM mmetumia ujinga wa Watanzania muda mrefu na mnaendelea kuwadanganya uchumi wa atki na mengine sijui reli, Mara ndege sijui uwanja wa ndege.

Ila Magufuli ni moja ya marais dikteta, mnafiki na hajiamini, miaka 5 kafanya kampeni peke yake, wanaCCM wenzake wakatamba 2020 hakuna haja ya kufanya kampeni Magufuli anatosha Sasa ya nini kuhangaika kufanya kampeni kama mnakubalika?

Ndugu Watanzania wenzangu CCM imeshagundua Watanzania wengi ni wajinga na wanatumia mwanya huo kuzidi kutudanganya.

Tuwakatae hawa watu hwatufai. Magufuli hatufai tena.
 
Magufuli tunamshukuru kwa yote aliyotufanyia lakini tunaomba apumzike hatumtaki, hatukutaki baba.

Mitano inakutosha, shukuru hata kwa hiyo mitano tu maana kuna watu wanaililia na hawaipati, lakini mkuu hivi unatumia ProtonVPN au umeamua tu kujilipua?
 
Kama yeye 2015 tulimjaribu kwa nini hataki tuwajaribu wengine? Shida ya yule mzee anaroho mbaya sana! Hajui siasa yeye anachojua ni ubabe tu!
 
Oktoba mimi nampigia kura Mzee Pombe pole sana kwa matatizo unayopitia, kwa upande wangu awamu hii imekuwa yenye neema kiuchumi na kijamii.
 
Laiti ujinga ungekuwa unamfanya mtu kichwa kinabonyeabonyea au pua inaongezeka urefu, humu mitaani tungeona yakujionea!
 
Back
Top Bottom