kinje ketile
JF-Expert Member
- Dec 12, 2015
- 4,818
- 9,171
Wakati tunaendelea na maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad na Yesu sio mbaya tujadili hii miezi miwili tangu atinge Ikulu bila ushabiki mambo yaliyofanyika!Kipindi cha kampeni alikuwa mbunifu sana,na kupindua hata kauli mbiu za vyama vingine.Alisema kama ni people's power nipeni mimi sitawaangusha,,!Magufuli kwa mabadiliko ya kweli...!Aliendelea kusema msema kweli ni mpenzi wa Mungu sitakuwa na mzaha na majipu lazima NIYATUMBUE.
Kwa mtazamo wangu kuna maeneo kweli mpaka sasa hajatuangusha kama mapambano aliyoyaelekeza kwa wakwepaji wa kodi,mipangilio na maandalizi ya kutoa Elimu bure mpaka sekondari.Kurejesha nidhamu ya kazi kwa watumushi,kufuta safari zisizokuwa na umuhimu,kipande cha barabara kutoka mwenge mpaka morocco kuanza kutengenezwa na mengine kem kem.
Lakini bado kuna changamoto tunamsubiri kuona atakabiliana nazo vipi?Mojawapo ni Katiba mpya...na hali ya siasa Zanzibar.Toa maoni yako unavyofikiri,