Magufuli leo atakuwa hapa Nyamongo

Magufuli leo atakuwa hapa Nyamongo

ccm na makufuli ni janga la taifa

wamewauwa wananchi wa nyamongo kwa miaka kibao sasa

unakumbuka majeneza yaliyotelekezwa njiani miaka ileeeeee, sitashangaa nikisikia ccm na makufuli yake wakizomewa huko nyamongo
 
Hatimae leo itakuwa ni zamu ya Nyamongo na viunga vyake
Ndani ya wilaya ya Tarime!

Mafuguri hapo awali ilikuwa apite tu bila kuongea na wananchi wa Nyamongo
Ila
Ghafla ratiba imebadilishwa kuwa kuna umuhimu wa kuongea na wakazi wa hapa!

Hivyo atawasiri kuanzia asubuhi hii!

Ikumbukwe kuwa tangu juzi na Jana kulikuwa na ujio wa mwenge hapa Nyamongo na Jana uliekea Serengeti!

Tar 23 ya mwezi huu itakuwa ni zamu ya Lowasa kuongea na wakazi wa hapa Nyamongo, wilayani Tarime.

Guys, watanzania wenzangu, haya yote ni kheri!
Ila kubwa tukumbuke kuwa
Kuna maisha baada ya chaguzi!

Amani yetu ni ya muhimu zaidi! na utu wetu, utanzania wetu ni wa thamani kubwa mno! kuliko hata hivyo vyama vya siasa!
Ndugu,
Umeongea maneno yaliyojaa hekima na Busara.

Kwa kutambua gharama ya amani yetu, utu wetu na Utanzania wetu ndiyo maana Magufuli amekuwa akihimiza amani, utu na mshikamano katika kila mkutano wake.

Kukosekana kwa amani ndiyo kifo cha CCM. CCM haiwezi kuruhusu hali hii itokee nchini.
 
Kwa akili finyu unadhani kuzomea ni sifa au ushujaa kwenye jamii yenye fikra pevu.

Kuzomea ni dalili ya ukosefu wa hoja na kwa maana hiyo, unataka wengine wasisike kwa sababu wewe huna suala la maana la kuwaambia wanaosikiliza.

Kwako upumbavu ni werevu!
 
Mkuu najua wengi wetu kwa sasa tunatambua umuhimu wa amani baada ya kuona machafuko ktk nchi baadhi tena yakiwa yanatokea baada ya uchaguzi!

Sisi kamwe tusikubali nchi yetu ifike huko coz tunatambua thamani ya undugu wetu na utanzania wetu!
Ubarikiwe zaidi.
 
Hapo nyamongo ndiyo kamanda tundu lissu akiwa na mzee lyatonga mrema walianza harakati za utetezi kwa wale wachimbaji wadogowadogo wa madini,nafikiri akija hapo watakuwa bado wanamkumbuka .
 
Aubili aman ya kweli si kutishia wananchi kwa kulinganisha nchi yetu na libya.
 
Frank Gotora, Wasalimie, Mama Frank, Mzee Philimon Kama Yupo Nyamongo, Maili, Nyang'anyi, Mwele Wangi, Marwa Ryoba, Kiribo, Mwita Kitutu, Wambura Keraryo

Hahahahaha dah umenigusa sana!
Yeah wote hao wapo hai
Nitawapa Hi
Dah unawafahamu sana sina shaka na wewe!
Karibu sana
 
Sasa kama mnahubiri amani , inakuwaje habari za Libya na Misri mnaziongelea kwenye mikutano yenu. Siye tunawatoa kwa amani 25 Oct kwenye sanduku la kura.
 
Aje kunadi sera, akianza habari zake za kutia hofu watu na kututisha, kuwa nchi itakuwa kama libya naondoka muda huo huo, na nitampuuza.
 
Sasa hata kama magufuli akija nyamongo unadhani atawageuza wanyamongo waipigie ccm kura?nasema hivyo nikiwa na maana kuwa wanyamongo mnaipenda sana chadema na hata viongozi woote tangu wenyeviti wa mitaa,vijiji hata madiwani ni chadema
 
Ndugu,
Umeongea maneno yaliyojaa hekima na Busara.

Kwa kutambua gharama ya amani yetu, utu wetu na Utanzania wetu ndiyo maana Magufuli amekuwa akihimiza amani, utu na mshikamano katika kila mkutano wake.

Kukosekana kwa amani ndiyo kifo cha CCM. CCM haiwezi kuruhusu hali hii itokee nchini.
Hivi Magufuli anahubiri amani au anachochea mauaji na machafuko?
Yeye anasema tukichagua upinzani kutatokea vita ana maana gani? Kama anajua upinzani ni vita ni kwanini serikali inawaangalia wapinzani wasiwadhibiti mapema kabla madhara hayajatokea?

Magufuli ndio anayehatarisha amani ya hii nchi kwa kuchochea mauaji nna machafuko na MUNGU atamlipa kwa kauli zake za kichochezi.
 
Hatimae leo itakuwa ni zamu ya Nyamongo na viunga vyake
Ndani ya wilaya ya Tarime!

Mafuguri hapo awali ilikuwa apite tu bila kuongea na wananchi wa Nyamongo
Ila
Ghafla ratiba imebadilishwa kuwa kuna umuhimu wa kuongea na wakazi wa hapa!

Hivyo atawasiri kuanzia asubuhi hii!

Ikumbukwe kuwa tangu juzi na Jana kulikuwa na ujio wa mwenge hapa Nyamongo na Jana uliekea Serengeti!

Tar 23 ya mwezi huu itakuwa ni zamu ya Lowasa kuongea na wakazi wa hapa Nyamongo, wilayani Tarime.

Guys, watanzania wenzangu, haya yote ni kheri!
Ila kubwa tukumbuke kuwa
Kuna maisha baada ya chaguzi!

Amani yetu ni ya muhimu zaidi! na utu wetu, utanzania wetu ni wa thamani kubwa mno! kuliko hata hivyo vyama vya siasa!

= Magufuli
= atawasili

Maneno yako ni ya hekima kubwa sana.

#HapaKaziTu
 
jeneza-Tarime.jpg

Ndugu zangu,

PICHA ya jeneza lililotelekezwa barabarani imeongea zaidi ya maneno milioni moja. Kwa Watanzania, imetutia simanzi, imetutoa machozi. Ndani ya jeneza hilo pichani kuna mwili wa marehemu Emmanuel Magige iliyotelekezwa kijijini Nyakunguru, Tarime. Emmanuel Magige hakuwa jambazi. Ni Mtanzania mwenzetu mwanakijiji wa kawaida. Aliyetelekezwa si Magige tu, kuna maiti nyingine tatu.

Mauaji ya Nyamonngo yanatukumbusha Arusha, yanatukumbusha Mbarali. Yanatutia hofu mpya pia. Hatujui kesho yatafanyika wapi.Kupunguza aibu hii ni kwa wote waliohusika na mauaji haya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Jeneza la Emmanuel Magige lililotelekezwa barabarani ni kielelezo cha mahali tulipofikia. Kuna chuki inajengeka. Na katika tofauti zetu hizi za kiitikadi tusifike mahali tukashindwa kuongea kama Watanzania. Tusifike mahali tukachochea machafuko makubwa ya kijamii. Wanasiasa wana jukumu la kutanguliza busara katika kila maamuzi wayafanyao.

http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/mauaji-tarime-polisi-wadaiwa
 
waliua wananchi ili wageni waibe madini kiulaini madalali wakubwa hawa
 
Back
Top Bottom