Magufuli kasababisha nikosane na demu wangu

Wa kwangu nmeachana nae kabsaa maana yy ananiambia hapendi siasa na kura hapigi ila cha ajabu anakua anaisifia ccm wakati mm TEAM MABADILIKO
 
Ukiwa na demu gamba hatari sana. Ila kama unampenda jifanye kumsapoti tu kwani kura yako utajua wa kumpigia. Hata mimi demu wangu ni gamba tena sugu ccm. Ila najua jinsi ya kuishi naye. Siasa zinapita na maisha yanaendelea. Chagua Lowassa chagua mabadiliko.

Halafu mimi mkuu nashindwa kuelewa magufuli kawapa nini hawa... nina vimichepuko vitatu vyote ccm nikiwambia stori za lowasa aseh wanafura kama donati....
 
Wakuu,

Hapa ninahasira mbaya,iko hivi Leo nilikua na ahadi ya mpenzi wangu aje alale kwangu sasa nikaandaa mamisosi ya kutosha ili kakipenzi kangu kafurahi,kweli akaja mida ya saa moja hivi,mara saa mbili ikafika tukiwa tumekaa sebuleni tukafungua news ITV,sasa si unajua kipindi hiki Ni cha kampeni news ya kwanza ilikua lowasa ee bwana eee mimi sinamfagilia huyu jamaa na ukawa?

Nikaonyesha furaha yangu jamaa alivyojaza nyomi!haaa mwenzangu si akaanza kuponda,anamfagilia Magufuli,kama masihara tumebishana mpaka ukawa ugomvi na msosi akagoma kula,nikashikwa na hasira kwa nini hali chakula na nimekitoa mbali,na mimi nikasema kama mbwai acha iwe mbwai nikamwambia hata ukisusa nakula mpaka kiishe unafikiri hela nimeokota?

Wakuu ni kama nimemwagia petrol kwenye moto si ashikwa hasira akatoka na kubamiza mlango akaenda kwake.kwakweli hapa nilipo ninahasira mbaya sana sijui usiku huu utakuchaje! Magufuli ninahasira na wewe sana hata kama unaingiaga hapa Jf habari ndo hiyo sikupi kura yangu.

Jembe afrika
Hongera kaka umeushinda mtihani alio feli Dr.Silaaa!!!
 
Back
Top Bottom