Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,442
- 4,388
Nikitazama 'lugha ya mwili'(body language) ya Rais Magufuli, namwona ni mtu mwingine tu ambaye kwa lugha maarufu ya wadau humu JF, amekuja "kupita" tu bila ya kuwa na dhamira ya kuhakikisha kuwa kweli Dodoma inakuwa Makao Makuu ya nchi.Itaendelea kubaki makao makuu ya chama chao - nao na kiherehere chao sijui nani aliwadanganya kuwa Dodoma itafika wakati itakuwa kweli makao makuu ya nchi. Kwa hiyo Dodoma itabidi wasubiri sana kuwa makao makuu ya kweli,labda itokee Juma Nkamia akawa Rais,au kwa maana hiyo mtu mzaliwa wa Dodoma....
Nina sababu mbili:
Moja,Rais Magufuli inaonekana amepania kuing'arisha Dar kwa "mabarabara" ya kupita juu na yenye mbwembwe za kila aina,naye hupenda sana kuzindua miradi ya mabarabara na madaraja.
Pili,yeye si mkereketwa kindakindaki wa CCM na bila shaka hana "jumba bovu" mjini mle - waliomtangulia walipapenda maana wana "magofu" ya kila namna kule,na walilipenda pia chama lao.Magufuli hana mzuka wa kuzurura-zurura kwenye mji huo wenye jua kali.
Magu hana mzuka na Dodoma, Magufuli anapapenda Dar, na kwao Chatooo...Dodoma nawaona bado watakuwepo-kuwepo kwa muda mrefu kidogo kabla ya kuwa Capital City kweli,kama si kufutiliwa mbali kabisa,who knows?