Magufuli hakujiandaa kuwa rais, atatuangusha tu

Huu ndo mjadala unaopendeza, unatoa hoja unarudishiwa hoja sio matusi utafikiri tupo vijiweni.
 
Kwa hiyo Mkapa alileta maendeleo? Mimi nilisikia aliuza mashirika na benki kwa bei ya kutupa, akafanya biashara akiwa ikulu, akanunua rada kwa bei ya juu, engineer wa EPA, kajibinafsishia mgodi wa kiwira, akajiuzia nyumba za serikali, akaanzisha kampuni ya biashara akiwa ikulu, akawaua wapemba baada ya kuwapora ushindi wao mwaka 2001 akitengeneza wakimbizi wa kitanzania kwa mara ya kwanza katika historia.

Mashinery atakayoitumia Magufuli ili kutawala(CCM) hata ufanyaje haiwezi deliver, it is rotten to the core huwezi aminisha watu kuwa itaweza engineer mabadiliko positively labda negatively, jawabu ni rahisi piga chini CCM introverts wakajenge Lumumba
 

Mnaposema amenunua uraisi hivi mliona risiti au ni hearsays tu?
 
unavyo tolea mfano mkapa kuhusu mafanikio ni sawa mafanikio yalikuwepo sana kwann ucmtolee mfano huyu aliko sasa hivi??????
 

Hivi kwa nini iwe like moja tu? Nilitaka kuongeza nyingine imekataa!
 
Kwa hiyo unataka kutuaminisha aliyekatwa ndiye fisadi ndani ya CCM? Kwa miaka takriban nane ambayo alikuwa nje ya serikali ufisadi ulikoma?

Alihusika na ESCROW, mabehewa mabovu TRC? EPA,uuzaji wa nyumba za serikali? Ikulu wako hasa msemaji wake Salva Rweyemamu hujibu mapema sana tuhuma zinazohusisha Ikulu ili akina Tomaso tujiridhishe mbona kakaa kimya baada ya EL kusema mamlaka ya juu(JK) ndiyo ilihusika kulazimisha mkataba wa RICHMOND usainiwe,sasa tumemjua mwenye dili hebu tuaminishe katika tuhuma lukuki za ufisadi zilizotokea hapa nchini na EL. Kama huna basi kaa kimya
 

Dunia hii ina maajabu mengi sana!
Kuna siku rangi zitabadirishwa majina yake, bluu itaanza kuitwa nyekundu, nyekundu itaitwa njano, njano itaitwa kijani!
Jua litaitwa mvua na mvua itakuwa jua!
 
Sheria inamzuia kuanza Kampeni. Subiri muda wa Kampeni uanze.
 
Fisadi Kikwete anataka kutuwekea boya ili limlinde kwa ufisadi aliofanya na mwanaye Riziwani. Bahati nzuri Mungu akatupa Watanzania jembe liitwalo Edward Ngoyai Lowassa
 

Ndugu yangu usitu tusi watanzania tafadhali sana.....hata huyo kenyata mtoto wake alituhumiwa kuwa ni muuaji ktk fujo za 2008 na pia familia yake ni FISADI lkn wakenya wakayawoka hayo pembeni then wakachagua mtu ambaye atawasogeza parefu kutoka hapo walipo
 

Vizuri sana umeweza kugundua Kuwa kikwete pia aliwekwa kwa hela kwahiyo ushindi wake ulikuwa wa kutumia hela yani ushindi wa kununua kama umsemavyo huyu wa ukawa

Sasa unawaambia nini wana ccm kuhusu rais wao alie madarakani Kuwa alinunua urais na alipaswa kulipa madeni ya waliomnunulia urais huo

Huoni Kuwa unazunguka palepale kwa kusema eti huyo anaetaka urais kwa kununua atalipa madeni

Au ndio upungufu wa muono fikra na kujielewa kwako???
 
Magufuli kuna wakati anaongea as if he is under the gun point! Hana collocation kabisa na vision!
 
Msitutoe kwenye hoja za msingi. Awe amejiandaa au hakuandaliwa, matatizo yanayolalamikiwa na wananchi wengi hayajaletwa na Magufuli, yameletwa na mfumo mbovu wa CCM. Yeyote anayesimama kutetea mfumo huo hatapata kitu mwaka huu. Hiyo ndiyo point. Msitupotezee muda kujadili kuandaliwa au kutoandaliwa. Hiyo siyo ajenda ya wapiga kura.
 

Hakuwa fisadi pekee ni mmoja wao, ndiposa maandiko matakatifu ya nasema rushwa hupofusha na wewe imekupofusha

Unataka kutumia muendelezo wa rushwa kama dekio la kumsafisha mmoja wao. Hizo skandali ulizo taja ni baada ya Nyerere kufa. Huyu superstar wa ufisadi hata Nyerere alikufa akiwa na records zake.
 
MAFUNGUO HANA MVUTO MBELE YA WANANCHI HANA USHAWISHI WOWOTE NI VIGUMU SANA KUIONA MAGOGONI LABBA APITE PALE MBELE NA GARI YAKE YA TINTED RAISI HUWA HAOKOTWI BALI LAISI ANAANDALIWA MAFUNGUO KAOKOTA DODO WE UMAFIKIL ANGEIPATA MH MEMBE HII NAFASI UNGEONA CHECHE ZAKE NA UNGE AMINI KWELI HUYU MTU ALIKUWA ANAUTAKA URAIS SIO HUYO FUNGUO WENU....poleni sana kwakupewa kiongoz asiye na mvuto kwa taifa hii ni hasara kubwa sana ya CCM
 

Tunataka mtoke muwaambie wananchi huyo ambaye mlizunguka nchi nzima mkiwaaminisha kuwa ni fisadi kageuka vipi ghafla kuwa mgombea wenu wa urais? Malaika wa safari ya uhakika, looh! Duniani kote maajabu haya ya unafiki wa kisiasa ulikomaa yanapatika Tanzania tu.

Hatutaki kusikia hizo hoja zenu dhaifu za kuokoka kisiasa. Wapinzani wa siasa Tanzania mmegekuka kuwa kichekesho eti sasa kuna waongofu wa kisiasa na wanapatikana kambi ya upinzani.

Kuokoka kuko makanisani tu. Acheni utapeli wa kisiasa.
 

Na ndio maana mlimuundia wizara ya kitowewo kwa kuwa mlijua ni tishio kwa upm wenu na bado aka perform, mkatoka serikalini mkamuacha akiwa anaendelea kufanya utumishi wake ulio tukuka kwa wananchi.
 

La Brujita kumbe tuko pamoja, asante cz umenisemea....its like u were in my thought
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…