Magufuli hakudai risiti aliponunulia watu soda Mwanza. Tumuige?

SeriaJr TW

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
246
224
Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna nafasi kwa wafanya biashara ya ukwepaji kodi.

Anahimiza wananchi kuhakikisha wanalipa kodi kwa kila bidhaa au huduma wanayolipia kwa kuhakikisha wanapewa risiti ya malipo hayo.

Inadaiwa kuwa, akiwa Jijini Mwanza juma lililopita aliingia mgahawani kupata chakula. Baadae akatoa laki moja ya ofa ya soda kwa wananchi waliokuwa jirani.

Aliwanunulia soda, alifanya manunuzi ya shilingi laki moja lakini video iliyoonesha tukio zima haioneshi akidai risiti yake.

That is how other people behave maeneo yao. Ndio utamaduni ambao umeshaathiri kila mwananchi.. Tumuige Magufuli na kuuendeleza utamaduni wa kutojali risiti au tumkumbushe na yeye awe anadai?

Au msaada hauna kodi?
 
Mnachotakiwa kufanya kwa sasa ni kukaa pale Ufipa mjenge chama chenu, bado mna nafasi na historia yenu inawabeba mmekuwa mkikua kila baada ya uchaguzi. Haya majungu sasa mnaweza kuwaachia SAU ambao hawana uelekeo wa kuongoza nchi.
 
Zile fridge ni outlet za coca sawa na maduka ya mpesa kodi hulipwa na coca cola.
 
Inamaana Coca Cola wanatoa kwenye faida yao ndio wanakulipia kodi.. Nijuavyo, mtumiaji wa mwisho ndiye hubeba mzigo wote . Sasa nisaidie nijue Coca wanakulipiaje?
 
Kwa kweli mbavu zimeniuma kwa kichekoo.. Siasa ni mchezo wa ajabu sana...
 
Kwa mama mntilie pale mgahawa ule tena wanauza chakula bei juu kabisa Ana mpaka mafriji walitakiwa kudai risiti acha uccm kutetea kila kitu
ninavyo fikiri mimi swala la risiti litakuwa lilishugulikiwa na usalama wa taifa au wasaidizi wake wengine lile kundi linalomzunguka kila mtu ana kazi yake brother!
 
Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna nafasi kwa wafanya biashara ya ukwepaji kodi.

Anahimiza wananchi kuhakikisha wanalipa kodi kwa kila bidhaa au huduma wanayolipia kwa kuhakikisha wanapewa risiti ya malipo hayo.

Inadaiwa kuwa, akiwa Jijini Mwanza juma lililopita aliingia mgahawani kupata chakula. Baadae akatoa laki moja ya ofa ya soda kwa wananchi waliokuwa jirani.

Aliwanunulia soda, alifanya manunuzi ya shilingi laki moja lakini video iliyoonesha tukio zima haioneshi akidai risiti yake.

That is how other people behave maeneo yao. Ndio utamaduni ambao umeshaathiri kila mwananchi.. Tumuige Magufuli na kuuendeleza utamaduni wa kutojali risiti au tumkumbushe na yeye awe anadai?

Au msaada hauna kodi?
ni hoja ya msingi ila ya hovyo kweli... nenda pale airport mwanza kaulize je hyo order ilikuwa ya bahati mbaya au planed? au unadhan kula pale ni bahati mbaya? cjui huwa mnaenda darasan kufanya nn..
 
Mnachotakiwa kufanya kwa sasa ni kukaa pale Ufipa mjenge chama chenu, bado mna nafasi na historia yenu inawabeba mmekuwa mkikua kila baada ya uchaguzi. Haya majungu sasa mnaweza kuwaachia SAU ambao hawana uelekeo wa kuongoza nchi.

Moja ya mifano mizuri sana ya baadhi ya watanzania ambao uwezo wao wa kuchambua na kutafakari mambo unapungua kwa kasi ya ajabu...wamebakiwa na misamiati michache sanaa ya BAVICHA, UFIPA, NYUMBU....
 
ninavyo fikiri mimi swala la risiti litakuwa lilishugulikiwa na usalama wa taifa au wasaidizi wake wengine lile kundi linalomzunguka kila mtu ana kazi yake brother!
He kumbe ni kufikiri tu
 
Back
Top Bottom