Magufuli bado hajanishawishi

hivi kwa akili yako ya ndege ulitegemea hivi vyote vipatikane kwa siku 30 zakuingia madarakani? Unajua kwanini muda wa urais uliwekwa miaka mitano na sio siku 30? Nyie ndio mnasali mkiomba mtu ashindwe. Akili za ndege hizo.
 
Naona wengi mnachangia kwa mihemko ya kisiasa, lakini nieleweke kuwa sijazungumzia habari za kwa mda huu awe amefanya hayo yote, nimezungumza kutokana na sifa anazopokea, nimehofu anaweza akavimba kichwa na kuhisi katufurahisha na kututendea haki watanzania, ikumbukwe kikwete nae alianza kwa mbwembwe mala chenji ya rada lakini mpaka sasa hivi hatujui hiyo chenji ilifanya kazi gani, mala kilimo kwanza ndio kwanza pembejeo zikapanda, mala timuatimua ya wakurugenzi na wakuu wa wilaya wazembe ndio kwanza akaleta wazembe zaid ya waliotangulia, mimi bado masisitiza na kumkumbusha magufuli kuwa bado hajaanza kazi ya kuwatumikia wananchi, bali ameanza kazi ya kukusanya fedha, ni wachache wenye kunielewa kwa sababu wengi mmejawa na mihemko
 
Jamani hata mji mzuri wa roma haukujengwa siku moja uvumilivu unatakiwa changamoto ni nyingi.
 
Hivi hizi jitihada ambazo ameanza nazo kama alivyoahidi kwenye kampeni wakati akinadi sera za chama chake zenye lengo la kukusanya mapato na kubana matumizi yasiyo na lazima/tija, kuzuia ufisadi unaofanya gharama za maisha zipande, watumishi wa umma kuchapa kazi nk bado haujashawishika tu?
Kero ulizoainisha zinasababishwa na pengine utendaji usio mzuri au ukosefu wa fedha, sasa unategemea hizo kero ulizoainisha hapo juu zitaondokaje kama hataanza na njia aliyotumia?
 

kwa hiz wiki tatu ajakushawishi??unaitaj maombi mzeyaa.thats process.....
 
nimekusoma mkuu wewe ni Genius!!point zako zimeenda chuo kikuu..tunataka bei za vyakula vishuke na sio barabara na vitanda.usanii mtupu huu wa kutafta sifa kwenye media.Mind games hizi zinachezwa

umeona enn..,
 
Unjua kinachofanyika tanzania ni uhaba wa mafanikio, sasa watu tunashangalia dalili za mafanikio kabla ya mafanikio yenyewe, zanzibar ni sehem ya tanzania, zanzibar isipotulia tanzania haijatulia, mgogolo wa zanzibar umefikia pabaya lakini yeye hana habari nao, niseme tu kuwa magufuri ameanza vizuri lakini bado hajaanza kuwatumikia wananchi, sasa mimi siwezi nikatoa pongezi kwake nimapema mno naogopa unafki nisije nikasifu baadae nianze kulalamika, nitakuja kusifu kitu chenyewe nitakuwa na uhakika nacho
 

Well,Kama rais sasa asitegemewe kwanin mulizunguka Tz nzima mukasema mutapunguza umasikini Tz kwa kasi ya ajabu once mukishika madaraka?? saiv ndo munaleta majibu watu wapambane kutafuta chakula.

Eti TASAF wewe kwa mtazamo wako kweli TASAF ulikuwa mradi wa kupunguza umaskini Tz?? TASAF ilikuwa ni system ya kunufaisha watu wachache kwenye jumuiya na wakubwa serikalini tu fund iliyotolewa na kinachomfikia mlengwa ni 0 -.

kuhusu overnight na siku 30 za rais kwanini ndani ya siku 30 amwezea kuleta mkandaras na kuanza kuchimbua barabara pale morocco hadi mwenge, vitanda muhimbili vilinunuliwa bila hata quotation wala invoice?? Rais huyo huyo asiweze kutumia hizo fedha kuleta vyakula kwenye mashirika ya umma wananchi wakauziwa kwa bei nafuu ili wafanyabiashara wote Tz wanaouza chakula wakalazimika kupunguza bei chakula mtanzania akanusurika kwanza na hii njaa?

Ata hao wagonjwa ambao amewanunulia dawa kuepuka sherehe za Ukimwi wanahitaji kula mara 3 Zaidi kuliko hizo dawa au akili zako zililenga mtu ameze dawa na njaa??

mi nadhan bado hii ni danganya toto na mchezo wa kuigiza kwa watanzania. Hizo kazi munazohimiza watu kufanya ziko wapi? zitafutwe wapi? juzi nimeskia pia mtapunguza wafanyakazi serikalini ivi uko nje rais ameshatengeneza hizo ajira?? au kwasababu muna power ya kwenda kwenye media na kusema lolote?
 

Elimu zetu ndivyo zilivyo Kiongozi, Matanzania ndivyo yalivyo.
 
Tumpe muda kuna majibu yataka kutumbuliwa na yamewiva tayari moja in like lililolipwa billion 8 bila ya kufanya kazi HAPA KAZI TU
 
Watanzania sijui nani katuloga! tumekuwa wepesi mmo, tumekuwa kama watoto wadogo anachapwa mda huohuo anapewa ziwa ananyamaza, tumekuwa wapole mno kwenye haki zetu wenyewe, umeme unakatika mwezi mzima lakini ukirudi watu tunashangilia na kumpandisha cheo meneja, ebu tubadilike tutazarauliwa mpaka lini?
 
Kwa hiyo Sasa unataka vishuke bei leo leo au kesho
 

Utajijua kwani umelazimishwa kushawishika pumzika huko uliko
 
Amshawishi kwani yeye ni nani nchi hii. Mwache JPM atekeleze wajibu wake. Hahitaji kumshawishi mtu kampeni zimeisha sasa kazi tu
 

Unafikiri hayo uliyoyataja yanapatikana kwa njia gani? Nje ya kijana matumizi na kodi,
 
Mpaka sasa sijaona cha kumpongeza nitakuja kua wa mwisho kumpongeza for now naona anafagia nyumba tu na hilo siwezi kumpongeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…