Magufuli badili salamu

Magufuli badili salamu

Pelle mza

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2008
Posts
3,050
Reaction score
1,694
Assalamu alaikum = Alaikum Wassalamu
Tumsifu Yesu Kristu = Milele Amina
Bwana Asifiwe = Amina
Mwanakondoo ameshinda = Tumfuate

Hizi salamu zina chembechembe ya ubaguzi, iko wapi salamu ya akina Kinje!
Magufuli kuwa mbunifu uje na salamu moja inatosha
Wana-JF msaidie.........
 
Assalamu alaikum
Tumsifu Yesu Kristu
Bwana Asifiwe

Hizi salamu zina chembechembe ya ubaguzi, iko wapi salamu ya akina Kinje!
Magufuli kuwa mbunifu uje na salamu moja inatosha
Wana-JF msaidie.........

umekosa cha kujadili! ulitaka akusalimieje
 
sema ww usituambie ss... Alafuu acha kusema kuwa salamu zina ubaguzi... Acha kufikiri kinyume....
Rais mteuliwa hana ubaguzi na kama kama ukiangalia mikutano yake mingi alikuwa akisalimu wanchi kwa lugha nyingi bila kusahau selemaa. Mwisho wa salamu huwa husema yeye atakuwa rais wa watanzania hata asiye na kabila thus hana ubaguzi.....
Au awe anasalimia NIAJE kama alivo wasalimu obama nchini kenya?????
 
Salamu iwe hivi "Wananchi amani Tanzania" tutajibu "Idumu" alaf anaendela na hotuba au kitu kingine!
 
wakatoliki oyeeee .... wataisoma number mwaka huu ... wahi GGM ukapokee kitofa chako kama Mzee Mkapa ...
 
sema ww usituambie ss... Alafuu acha kusema kuwa salamu zina ubaguzi... Acha kufikiri kinyume....
Rais mteuliwa hana ubaguzi na kama kama ukiangalia mikutano yake mingi alikuwa akisalimu wanchi kwa lugha nyingi bila kusahau selemaa. Mwisho wa salamu huwa husema yeye atakuwa rais wa watanzania hata asiye na kabila thus hana ubaguzi.....
Au awe anasalimia NIAJE kama alivo wasalimu obama nchini kenya?????

wrong toilate mr.. hii unge m quote mleta uzi
 
..hata mimi hizi salamu za kidini sizipendi.

..siyo Magufuli peke yake anayetakiwa kuachana na utaratibu huo.

..hata viongozi wa vyama vya upinzani nao wanatumia salamu hizo za kidini. na wao waache.

..viongozi waseme tu wanachotaka kukisema bila kuingiza salama za kidini.

..mambo haya yameanza awamu hii ya JK.

..Mwalimu Nyerere, Alhaji Mwinyi, na Mzee Mkapa, hawakutumia salamu hizi.

cc Pelle mza
 
Last edited by a moderator:
Ipo haja ya kubadili salamu. Leo nilimsikia Mkurugenzi wa NEC Ramadhani Kailima amesalimia kwa salamu ngeni sana kwangu. Alisema "Mwanakondoo ameshinda" walioijua wakajibu "Tumfuate" nilipoulizia kwa my colleague akasema hio ni salamu ya Moravian Church. Sasa tutataja madhehebu yote?
Salamu isiyobagua ni "Habari zenu ndugu zangu!"
 
..hata mimi hizi salamu za kidini sizipendi.

..siyo Magufuli peke yake anayetakiwa kuachana na utaratibu huo.

..hata viongozi wa vyama vya upinzani nao wanatumia salamu hizo za kidini. na wao waache.

..viongozi waseme tu wanachotaka kukisema bila kuingiza salama za kidini.

..mambo haya yameanza awamu hii ya JK.

..Mwalimu Nyerere, Alhaji Mwinyi, na Mzee Mkapa, hawakutumia salamu hizi.

cc Pelle mza

Hamna kitum kinaniudhi kama salamu hizi. Hizi zinatakiwa kutumika kila salamu na waumini wake. Kwanza mlolongo unakuwa mreeefu bila sababu ya msingi ni kupoteza muda tu. Salaamu za kidini peleka misikitini na makanisani. Tunataka salamu ambayo ni Neutral!!! kama motto wako hapa ni kazi tu kwa hiyo hamna muda wa kupoteza wa misalaaamu miiiiiiiiiiingi! Kwanza chimbuko lake ni kuwa kuna mtu fulani alianza salaamu ya dini moja. dini ny8ingine hazikukubali na kuanza nzao despite ya kuambiwa maana kwa kiswahili ile salaamu. Hivyo salamu za Dini Dk. Magufuli achana nazo.
Halafu milolongo ya wafanyakazi sijui kujipanga kutumia muda wa kazi kumpongeza sijui kumkaribisha fulani tupa kule pia ni ucheleweshwaji tu wa majukumu kwa aliyeteuliwa! Aliyeteuliwa akaribishwe na mwenyeji awasalimie wafanyakazi kwa kikao cha wafanmyakazi aendelee na kazi.

Masuala mengine ya kikazi nitayaandika kwenye thread nyingine kwani tunataka mabadiliko kwa vitendo kwa ujumla tunataka utendaji maofisini uuu- overhaul
 
Back
Top Bottom