Magufuli awataka kina mama kutembea kifua mbele

swissme

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
13,662
19,880
Rais wa Rwanda Paul Kagame leo 08 Machi, 2019 amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 2 hapa nchini na kurejea nchini kwake, ambapo hapo jana alifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

maguuuuuuuuuuuuuuu.jpg

Mara baada ya kuagana na mgeni wake Rais Magufuli amesalimiana na wananchi wa Dar es Salaam waliojitokeza kumuaga Rais Kagame ambao wengi wao walikuwa ni wanawake na kuwatakia heri ya Siku ya Wanawake Duniani.
Rais Magufuli amewashukuru wanawake wote kwa mchango mkubwa kwa taifa na amesema serikali inatambua na kuthamini juhudi zao mbalimbali.
“Mungu awabariki sana akina mama, mnafanya kazi nzuri kwa ajili ya taifa hili, endeleeni kuimarisha umoja wa Watanzania wote, serikali ninayoiongoza inathamini sana kazi nzuri zinazofanywa na akina mama, endeleeni kutembea kifua mbele, Mungu atawalinda, na mimi sasa hivi naondoka kwenda kumuona mama yangu hospitalini katika siku yake hii, pia natoa shukrani

SASA YEYE HAJUI KUWA HATA BENN SAANANE ALIPENDA KUMUONA MAMA YAKE? BENN ANGEPENDA KUMUONA MAMA YEKE?

SWISSME

======

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amewapongeza kina mama nchini kwa jitihada mbalimbali wanazozifanya na kwamba waendelee kutembea kifua mbele kwa kuwa Serikali inawathamini.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo leo Ijumaa Machi 8, 2019 katika uwanja wa ndege wa zamani wa Julius Nyerere ikiwa ni muda mfupi baada ya kuagana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame aliyekuwa nchini kwa ziara ya siku mbili.

“Nawapongeza wananchi wote waliojitokeza kumsindikiza Rais Kagame, mmeonyesha ukarimu wenu kwa Watanzania. Nimefurahi sana kuona kina mama mpo wengi na leo ni siku yenu.”

“Mungu awabariki mnafanya kazi nzuri sana, endeleeni kuimarisha umoja kwa Watanzania wote, Serikali ninayoiongoza inathamini sana kazi nzuri zinazofanywa na kina mama. Endeleeni kutembea kifua mbele na Mungu atawatunza na mimi sasa hivi nakwenda kumuona mama yangu hospitalini,” amesema Rais Magufuli huku akishangilia na kina mama waliokuwa uwanjani hapo.

Mbali na hilo, Rais Magufuli alivikabidhi Sh1 milioni vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza uwanjani hapo wakati wa hafla ya kuagana na Rais Kagame.

“Hiki kidogo mtakwenda kunywa chai. Nawapongeza sana mmekuwa mkionyesha ukarimu kwa wageni wanaokuja na kupokelewa vizuri,”amesema Rais Magufuli.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema aliyekuwapo uwanjani hapo ameshukuru Rais Magufuli kwa zawadi hiyo na kusema “Magufuli oyee… nani kama Baba Magufuli? Hakuna baba kama Magufuli.

Soma zaidi: Kagame aondoka Tanzania baada ya kumaliza ziara yake

Chanzo: Mwananchi
 
Kuwa yeye anakwenda KUMUONA mama ya ke hospital je swali KWANI BENN SAANANE HAKUPENDA KUMUONA MAMA YAKE?

SWISSME
 
Huyu jamaa sijui vipi tu yani hajui hata BENN SAANANE NAYE ANGEPENDA KUMUONA MAMA YAKE

SWISSME
 
Wanafiki hawaachi asili.

Rais Magufuli

IJUMAA , 8TH MAR , 2019
NA MWANDISHI WETU
Rais wa Rwanda Paul Kagame leo 08 Machi, 2019 amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 2 hapa nchini na kurejea nchini kwake, ambapo hapo jana alifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

maguuuuuuuuuuuuuuu.jpg

Mara baada ya kuagana na mgeni wake Rais Magufuli amesalimiana na wananchi wa Dar es Salaam waliojitokeza kumuaga Rais Kagame ambao wengi wao walikuwa ni wanawake na kuwatakia heri ya Siku ya Wanawake Duniani.
Rais Magufuli amewashukuru wanawake wote kwa mchango mkubwa kwa taifa na amesema serikali inatambua na kuthamini juhudi zao mbalimbali.
“Mungu awabariki sana akina mama, mnafanya kazi nzuri kwa ajili ya taifa hili, endeleeni kuimarisha umoja wa Watanzania wote, serikali ninayoiongoza inathamini sana kazi nzuri zinazofanywa na akina mama, endeleeni kutembea kifua mbele, Mungu atawalinda, na mimi sasa hivi naondoka kwenda kumuona mama yangu hospitalini katika siku yake hii, pia natoa shukrani

SASA YEYE HAJUI KUWA HATA BENN SAANANE ALIPENDA KUMUONA MAMA YAKE? BENN ANGEPENDA KUMUONA MAMA YEKE?

SWISSME
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom