Magufuli aongoza kikao cha kamati ya usalama na maadili ya CCM

Baraka Mkuu

Member
Sep 22, 2016
21
73
Machi 10, 2017
Dodoma

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Machi, 2017 ameongoza Kikao cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika Chamwino Mkoani Dodoma.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wake wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd.
 

Attachments

  • IMG-20170310-WA0024.jpg
    IMG-20170310-WA0024.jpg
    98.7 KB · Views: 55
  • IMG-20170310-WA0028.jpg
    IMG-20170310-WA0028.jpg
    67.5 KB · Views: 46
"Maadili" ya kukazia umuhimu wa vikao rasmi kuhusu kero za muungano ni mojawapo ktk ajenda ya kikao?

 
Siku ambayo Upinzani Utachukua hii nchi itabidi Mali zote za CCM zitaifishwe.
Tatzo mnaamin tofauti... Jengen of is yenye Hadhi kama chama kikuu kwel cha upinzani... Sio kupanga chumba na sebule
 
Deni halilipwi na umeme haukatwi, Magu ni mwoga sana, aliishindwa lugumi ndio ataweza kuikatia Zanzibar umeme.
 
Siku ambayo Upinzani Utachukua hii nchi itabidi Mali zote za CCM zitaifishwe.
Sio zote. Zipo ambazo ni halali yao lakini kama Viwanja vya mipira vilijengwa kwa nguvu ya wananchi enzi za chama kimoja so vinatakiwa kuwa Mali ya wote na vimilikiwe na halmashauri husika
 
Hii Kamati ya Maadili 2015 ikiwa chini ya Jk ndio Ilichinja Yule Mchinjwaji Maarufu anaechinjwa Tangu Enzi za Baba wa Taifa 1995
 
Back
Top Bottom