Magufuli anawezaje kusema kuwa serikali iliyopita ilikuwa fisadi wakati alikuwa kwenye System Pia?

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,942
18,669
Mi nashangaa sana huyu Raisi wetu anavyojinadi kila siku et serikal iliyopita ilikuwa fisadi wakati hata yeye alikuwa kwenye iyo serikal.
171042acbd37e290f76e9383f91aad9d.jpg

Kwa mfano pale anapozungumzia ujenzi wa bomba la gesi kufanywa na wachina ambapo serikal ya Tanzania na contractor wa china walishirikiana kupiga pesa kwenye huu mradi. Hivi sio yeye alikuwa ni waziri wa ujenzi kipindi bomba la gesi linajengwa.
Au ntakuwa nimesahau alikuwa waziri wa uvuvi.

Serikali anayodai ilikuwa na mafisadi , hao mafisadi anao wazungumzia sijui ni wa namna gani maana viongozi waliopo serikali hii ni wale wale. hata anaowatumbua anawatoa shinyanga na kuwapeleka dodoma.

Ni yeye aliyeanzisha mahakama ya mafisadi kwa mkwala mzito ila leo mahkama imepigwa doro. watumishi wa mahakama wanaponda tu pesa za walipa kodi. Yeye hana machungu sababu halipi kodi. Hata chakula anachokula tunamgharamikia sisi.

Inabidi watanzania tufikia hatua tuamke sasa. Haiwezekani tunafanywa kama wa toto. Fisadi fisadi hata kumfikisha mahakamani hakuna.

Tumewachoka sasa
 
Wenye akili mtafunguka tu.

Mahakama ya mafisadi ni sarakasi za kisiasa.

Note: "nchi ilikua imepinda hii , "

"nchi ilikua imeoza"
"kuna makaburi mengine siwezi kuyafukua yasije yakanishinda kuyafukia"

Hao waliyoipindisha ,walioiozesha, na hayo makaburi ni wakina nani??? Kwa maana inaonekana kuanzia vyombo vya dola, mpaa yeye mwenyewe mamlaka kuu hawezi kuwashughulikia...

Kiukweli kwenye hili Baba J ana hatia...
 
Lowasa wala hajifichi kama ni mamluki,
Yeye anasimama hadharani, kwenye mkutano wa kampeni na kuwaomba wananchi wachague wagombea wa ccm kwa kura nyingi.

Alafu bavichaa wanashangilia tu
 
Mi nashangaa sana huyu Raisi wetu anavyojinadi kila siku et serikal iliyopita ilikuwa fisadi wakati hata yeye alikuwa kwenye iyo serikal.
171042acbd37e290f76e9383f91aad9d.jpg

Kwa mfano pale anapozungumzia ujenzi wa bomba la gesi kufanywa na wachina ambapo serikal ya Tanzania na ya china walishirikiana kupiga pesa kwenye huu mradi. Hivi sio yeye alikuwa ni waziri wa ujenzi kipindi bomba la gesi linajengwa.
Au ntakuwa nimesahau alikuwa waziri wa uvuvi.

Serikali anayodai ilikuwa na mafisadi , hao mafisadi anao wazungumzia sijui ni wa namna gani maana viongozi waliopo serikali hii ni wale wale. hata anaowatumbua anawatoa shinyanga na kuwapeleka dodoma.

Ni yeye aliyeanzisha mahakama ya mafisadi kwa mkwala mzito ila leo mahkama imepigwa doro. watumishi wa mahakama wanaponda tu pesa za walipa kodi. Yeye hana machungu sababu halipi kodi. Hata chakula anachokula tunamgharamikia sisi.

Inabidi watanzania tufikia hatua tuamke sasa. Haiwezekani tunafanywa kama wa toto. Fisadi fisadi hata kumfikisha mahakamani hakuna.

Tumewachoka sasa

Ameshasahau kama alikuwa kwenye system maana hata wanaccm wengi wamesahau kama ccm ndio ilikuwa inatawala nchi siku zote wanashambulia utawala uliopita kana kwamba walikuwa upinzani ndio watawala
 
Katika miaka yote ishirini+ aliyokuwa kwenye system, Magu hajawahi kukataa posho au stahiki yoyote kuanzia za kwenye ubunge hadi uwaziri. Ila leo ndio anaziona kharam!

Ameamua kukomoa watumishi na makato ya ajabu bodi ya mikopo ila yeye binafsi amesoma PHD kwa kodi zetu, tena kwa kasma za wizara alizoongoza wala si mkopo wa bodi, na kwa maana hiyo halipi hata kumi...

Unafiki ni dhambi mbaya sana!
 
Ameshasahau kama alikuwa kwenye system maana hata wanaccm wengi wamesahau kama ccm ndio ilikuwa inatawala nchi siku zote wanashambulia utawala uliopita kana kwamba walikuwa upinzani ndio watawala
Safi sana mkuu. Hawa watu ni wajinga sana wanafikiri hatujui kinachoendelea. Wamesahau utafikiri 2015 ndiyo sisiem imeanza kutawala. Hiv waliokula pesa za wahanga wa bukoba wakina nani km siyo sisiem.
KIBAYA ZAIDI WAMETAFUNA MPAKA PESA ZILIKUWA ZINATUMIKA KUAJIRIA WATU NA MIKOPO HALAFU WANAKUJA NA VISINGIZIO VINGI.
Poor sisiem hii laana lazima iwatafuna, sasa hiv mvua hainyeshi sabb ya dhambi zenu.
 
Katika miaka yote ishirini+ aliyokuwa kwenye system, Magu hajawahi kukataa posho au stahiki yoyote kuanzia za kwenye ubunge hadi uwaziri. Ila leo ndio anaziona kharam!

Ameamua kukomoa watumishi na makato ya ajabu bodi ya mikopo ila yeye binafsi amesoma PHD kwa kodi zetu, tena kwa kasma za wizara alizoongoza wala si mkopo wa bodi, na kwa maana hiyo halipi hata kumi...

Unafiki ni dhambi mbaya sana!
Sawa. Mradi mkubwa kama huo haukujadiliwa kwenye cabinet?Kama aliona kuna ufisadi mbona hakujiuzulu?
 
Back
Top Bottom