Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,660
- 1,801
Ni mradi wa barabara itokayo Muheza, Tanga kuelekea Amani. Amani ni hifadhi ya kimataifa ya tabia " Nature Reserve" na inasemekana ni pekee duniani na hata kufananishwa tu na hifadhi ya Galapagos, kule Ecuador. Of course, kila mtu msomi anajua umuhimu wa Galapagos katika historia ya binadamu na taaluma.
Ni huko ndiko mwana taaluma wa elimu za tabia (naturalist) na tabaka za ardhi (geologist) Charles Darwin, alipoendeleza nadharia yake ya kuwa asili ya binadamu ni nyani (Threory of evolution and natural selection- survival of the fittest) baada ya kuangalia utitiri wa wanyama waliokuwa huko. Kwa kifupi, Amani ni eneo muhimu sana.
Na lau lingekuwa Uingereza au Marekani, watu milioni 3-4 wangelitembelea kila mwaka. Alas! Liko Tanzania kwa watu wasiojua hili wala lile, isipokuwa kupiga miayo ya umaskini!
Anyway, acha niendelee na kisa cha kusikitisha cha mradi ninaouelezea. Mnamo kipindi cha Kikwete, kulitolewa fedha za kuweka barabara ya lami kutoka Muheza hadi Amani, ili kuwezesha utajiri wa huko uweze kufikiwa vizuri (Amani pia inatoa miti ya dawa, mbao za aina ya pekee).
Pesa hizi zilikabidhiwa mtendaji mmoja, nadhani Mkuu wa Wilaya ili afanikishe barabara hiyo ya lami ya kilomita 22.
Alichofanya huyu bwana alipaka lami kipande cha kilomita moja tu kutoka Muheza na pesa zilizobakia hadi leo haijulikani ziko wapi.
Vyanzo vyangu vimenieleza kuwa bw. Magufuli, akiwa Waziri wa Ujenzi alitembelea Muheza na akamfokea sana bwana huyu na kumwamuru azitoe fedha hizo.
Hata hivyo katika patashika za uchaguzi jambo hili limesahauliwa hadi leo.
Inasikitisha sana kwamba katika kipindi cha awamu ya 4 mambo kama haya yalikuwa kawaida na wanaofanya hawakuchukuliwa hatua zozote.
Ndiyo maana nakumbusha mradi huu muhimu sana ufuatiliwe.