Magufuli Anasafiria Nyota ya Kikwete

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
LICHA ya Serikali ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kutuama katika tuhuma ya uzembe, ufisadi na rushwa, sehemu ya utawala wake unatajwa kumbeba Rais John Magufuli, anaandika Regina Mkonde.

Hatua ya Serikali ya Rais Magufuli kupunguza bei ya umeme inatajwa kuandaliwa na mtangulizi wake Rais Kikwete na kwamba, miundombinu Shirika la Umeme nchini (Tanesco) na mingine iliyoandaliwa na mtangulizi wake, inamsaidia kuinua uchumi wa nchi.

Serikali jana imetangaza kupunguza bei ya umeme pia kuondoa kodi ya huduma kwa mwezi Sh. 5520 hatua ambayo imepokelewa kwa mikono miwili na wananchi huku baadhi ya wachambuzi wakieleza kuwa, hatua hiyo haitoleta mabadiliko kwenye uchumi wa nchi kulingana na asilimia ndogo ya mabadiliko katika bei.

Akizungumza na MwanaHALISI Online Bashiru Ally, Mhadhiriwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) amesema, mafanikio hayo si ya Rais Magufuli isipokuwa ni ya mtangulizi wake.

“Ni vigumu kusema kuwa anachofanya rais ni jitihada zake na kwamba Rais Kikwete hakufanya kitu, tusisahau kuwa miradi mingi ya umeme na miundombinu ilijengwa na Rais Kikwete,” amesema Bashiru na kuongeza;

“Huyu amekuja kuanzia sehemu aliyoishia mtangulizi wake na yeye ataacha misingi na changamoto ambazo zitakuja kutatuliwa na anayefuata.”

Hata hivyo, Bashiru amepongeza hatua hiyo kwa kuwa, katika hali fulani itawasaidia wananchi kupunguza makali ya maisha hasa wajasiliamali wadogo wanaotegemea kuingiza mapato kupitia nishati ya umeme.

“Wazalishaji watanufaika baada ya kushuka kwa bei ya umeme, kutasaidia kupunguza mfumuko wa bei nchini kama unavyopanda wakati gharama za umeme zinapopanda,” amesema Bashiru.

Mtaalamu wa masuala ya uchumi nchini, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kwamba, Rais Magufuli bado hafikia viwango vya kukomboa uchumi wa nchi.

Amesema, hatua ya kushusha bei ya umeme haijafikia kiwango cha kusaidia uchumi wa nchi kama ambavyo baadhi ya watu wanavyoweza kudhani.

“Ukitazama kwa ndani utaona kwamba hakuna mshuko mkubwa wa bei ya umeme iliyofanyika ukilinganisha na kushuka kwa bei ya petrol kulikotokea mwaka jana, sababu bei ya Petrol mwaka 2015 ilishuka sana na kufikia nusu ya bei iliyokuwa ikiuzwa,” amesema Prof. Lipumba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF).

Ameeleza kuwa kama bei ya umeme ingeshuka kwa asilimia 20 ingesaidia kuimarisha uchumi wa wananchi hasa wale wenye viwanda vidogo.

“Iwapo bei ingeshuka kwa asilimia 20 ingesaidia kujenga uchumi wa nchi kwa asilimia kubwa pia kungekuwa na umeme wa uhakika hali ambayo ingesaidia kuimarisha uchumi,” amesema Prof. Lipumba.

Akizungumzia kuhusu Tanzania kunyimwa misaada na Mfuko wa Chanagamoto za Milenia (MCC), Profesa huyo ametoa wito kwa serikali kurejesha misingi mizuri ya demokrasia na kujenga uaminifu duniani kote kulingana na namna ilivyojinasibu kuwa nchi inayoendeshwa kwa misingi ya demokrasia na uhuru.

“Wahisani waliamua kufuta misaada yao baada ya kuona uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu visiwani Zanzibar haukufuata demokrasia hali iliyotafsiriwa na wahisani kama kwenda kinyume na makubaliano baina yao na MCC,” amesema.

Anasema Tanzania iliingia mkataba na MCC na ikasaini makubaliano ya kuendeleza misingi ya demokrasia na haki na ndiyo sababu ya kukubaliwa kupewa msaada wa Sh. 360 Bilioni ambazo zimezuiliwa.

Prof. Lipumba anafafanua kwamba fedha hizo zililenga kuwekeza kwenye sekta ya nishati ili nchi ipate umeme wa uhakika utakaokidhi mahitaji ya viwanda hivyo kutopatikana kwa fedha hizo kuna athiri uchumi wa nchi.

Prof. Benson Bana, Mhadhiriwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema, kushuka kwa bei ya umeme kutasaidia kupunguza mfumuko wa bei.

“Umeme unatumika kwa wingi viwandani hivyo kushuka kwa gharama za umeme kutasaidia kupungua kwa mfumuko wa bei,” amesema Prof. Bana.

Kuhusu kukatishiwa misaada na nchi wahisani, amesema serikali haina budi kuangalia upya sera ya urafiki na diplomasia ya nchi za nje.

“Kuna baadhi ya maeneo yataathirika hivyo lazima serikali ijitahidi kubana matumizi mahali Fulani ili kuziba pengo hilo,” amesema Bana.

Amesema ingawa kujenga uchumi wa nchi itachukua muda lakini baadaye mambo yatakaa sawa na hata vizazi vijavyo vitanufaika na kuishi kwa raha kama wanavyoishi raia wa nchi nyingine.
 
Tujifunze kuwa na shukrani hata kidogo hongera magufuli kwa kushusha umeme.
 
Mwanahalisi online linamsifia Kikwete? Siamini nadhani hii habari haijatoka kwny Mtandao wa Saed Kubenea.
 
Ilipaswa iwe Raisi Magufuli anatembelea nyota ya CCM, kwa maana kwa CCM kila Raisi anayeingia anachukuwa mtangulizi wake alipoachia hata Kikwete pia alichukuwa mengi ktk kwa Mkapa alipoachia na Mkapa alichukuwa ktk kwa Mwinyi na Mwinyi ktk kwa Nyerere n.k!
Hivyo kuna sababu kwa nini CCM wanasema Raisi y amepokea kijiti ktk kwa Rais x!
 
kama mnapenda ligi fuatilieni ile ya EPL, mh, Magufuli asante kwa kupoza bei za umeme na kuondoa service charge wanaochonga waacheni wachonge, eti anatembelea nyota mh, raisi si mshirikina atembelee nyota. Mmeishiwa ya kuandika.
 
Miongoni mwa vitu bora na vya msingi vilivyofanywa na Serikali ya Kikwete ni kutandaza mifumo ya Kitelecomunication ya Optic Fiber na pia Kuifanya Tanzania kuwa Hub ya Internet Traffic ya nchi mbalimbali jirani zake zisizopakana na bahari, Kutokana na Huduma hii Tanzania inajipatia fedha nyingi sana za Kigeni, Profesa Mkoma wa TCRA amewahi kusema kuwa Kwa huduma hii, Tanzania inaweza kupata fedha za kigeni zinazokaribiana na zile zinazopatikana ktk bandari ya DSM.
Kikwete alijenga Taasisi nyingi na muhimu sana!
 
(1) Nchi haiendeshwi kwa nyota ya mtu, bali inaendeshwa kwa sera na malengo ya kitaifa.
(2) Ni kweli kuwa misaada na mikopo inasaidia katika kufikia malengo, hata hivyo, kuendesha nchi ukitegemea misaada, ni sawa na kuendesha familia ukimtegemea jirani yako awalishe na kuwavalisha watoto wako pamoja na kununua vitu kama chupi za mkeo.
(3) Soma kitabu hiki: Dead Aid: Why Aid Is Not Working and How There Is a Better Way for Africa: Dambisa Moyo, Niall Ferguson: 9780374532123: Amazon.com: Books
 
Mwanahalisi online linamsifia Kikwete? Siamini nadhani hii habari haijatoka kwny Mtandao wa Saed Kubenea.
Hukushangaa walipoanza kumsifia Lowassa? Walimtukana Lowassa na kumuita kila jina baya hapa duniani kwa miaka 8 lakini wakabadili gia angani. Baada ya Lowassa kuingia CHADEMA wakabeba dodoki na kuanza kumtakasa kwa upako!! Kwa kifupi wanasaka tonge.
 
(1) Nchi haiendeshwi kwa nyota ya mtu, bali inaendeshwa kwa sera na malengo ya kitaifa.
(2) Ni kweli kuwa misaada na mikopo inasaidia katika kufikia malengo, hata hivyo, kuendesha nchi ukitegemea misaada, ni sawa na kuendesha familia ukimtegemea jirani yako awalishe na kuwavalisha watoto wako pamoja na kununua vitu kama chupi za mkeo.
(3) Soma kitabu hiki: Dead Aid: Why Aid Is Not Working and How There Is a Better Way for Africa: Dambisa Moyo, Niall Ferguson: 9780374532123: Amazon.com: Books
Mkuu nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro upo? Ulipotea sana karibu.
 
Niponipo kama sipo Mzee wangu, maana JF imekuwa kama kijiwe cha uchochoroni siku hizi. Kwa hiyo watu wengine tusiojua matusi tumejiweka kibindoni kwa vile mijadala mingi ni ya matusi, ambayo hatuiwezi, kuliko hoja.
 
Kweli mkuu ila naona kama jamaa zetu hawasikii kilio hiki! Tumesema, tunasema mwisho tutachoka manake hakuna mabadiliko.
 
Back
Top Bottom