Magufuli anafaa kutawala maisha

Magufuli anafaa kutawala maisha

njeeseka

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
1,374
Reaction score
985
Ni kama vile kuna baadhi ya watu hawaamini km kwa sasa Tanzania ina Kiongozi imara, Jasiri na Mzalendo.

Speed yake ni kubwa na inatishia hata mustakabali wa maisha ya baadhi ya watu waliozoea za kuunga unga.

Nimesoma gazeti fulani linamtaja Mfanyabiashara mmoja ambaye amebwaga manyanga mchakato wa kununua KOKO BEACH na kuamua kumuunga mkono Mhe Magufuli badala ya kumpinga.

Kuna watu ktk Mkoa fulani waliomba ikiwezekana katiba ibadilishwe ili Rais wetu wa sasa akae zaidi madarakani, wengine walipinga tena kwa vijembe.

Mim binafsi naona km naanza kuwaelewa hawa watu hasa baada ya kusikia kauli ya MHE RAIS MSTAAFU kupitia chombo cha habari akitufumbua macho kwamba Rais wetu sio wa mchezo mchezo na ingekuwa mapenzi ya wanainchi kurefusha muda ingekuwa swadaktaa.

Haya ni maneno mazito kuwahi kutolewa na Mtu muhimu ktk taifa hili tuyachukulie kwa uzito mpana.

Tukiacha tofauti za kiitikadi za vyama vya siasa, ni wazi kuwa kwa sasa hakuna Rais Bora, Africa hata Duniani kama Magufuli.

Tuungane tumtunze Rais wetu ili aishi muda mrefu tufaidi ili atuvushe salama, hii ndiyo SAFARI HALISI YA MATUMAINI kuelekea Tanzania mpya, ileeee.
Hongera Mheshimiwa, nimeanza kukuombea.

IMG_20170626_190018_036.JPG
 
Maisha yote ya uhai wa taifa hili ni kazi ya ccm hata Miaka mitano bado mnawaza awe wa kudumu, tunaumwa bongo zetu!!
 
msilete hizo propaganda zenu hii nchi inaendeshwa kikatiba...hatutaki kusikia hicho kitu
 
Tulieni muache mihemko, kama ni ridhaa ya wananchi kutaka aendelee kuna shida gani?
Kwani katiba iko kwa ajili ya nani, sio wananchi?
Wakiamua aendelee hamna atakayepinga.

Habari ndio hiyo na nionavyo hata speed haipungui kama mlidhani ni moto wa mabua sijui nguvu ya soda, mmeliwa "jaribu kuchanganya soda na gongo uone kama hutalewa"
 
Ukibadili katiba akakaa miaka 20 siku akitoka akaingia wa upinza mtaanza tufupishe katiba atawale japo miaka 5 tu.
 
Tulieni muache mihemko, kama ni ridhaa ya wananchi kutaka aendelee kuna shida gani?
Kwani katiba iko kwa ajili ya nani, sio wananchi?
Wakiamua aendelee hamna atakayepinga.

Habari ndio hiyo na nionavyo hata speed haipungui kama mlidhani ni moto wa mabua sijui nguvu ya soda, mmeliwa "jaribu kuchanganya soda na gongo uone kama hutalewa"
Mimi nitapiga kura aendelee
 
Ukibadili katiba akakaa miaka 20 siku akitoka akaingia wa upinza mtaanza tufupishe katiba atawale japo miaka 5 tu.
Issue sio chama, tunakosea hapa, issue ni right candidate, kama yupo upinzani au chama tawala na anafaa, why not.
 
Walio wengi vijan Jf wana mihemuko ya maisha acheni hizo pambaneni na hali zenu za ugumu wa maisha chadema achen kumuwaza Lowasa ccm achen kumuwaza Magufuli kamwe hawatakufanya uwe na life zuriiiii mtazamo tu huo
 
Huyu Mzee Mwinyi, Mimi ninamweshimu sana kwa kauli zake kwani aliwai sema Tz in kichwa cha mwendawazimu hadi leo atujawai fanyikiwa kwnye soka.So kwanza aifute kauli yake kwnye Soka!
 
Kutawala ni mtu ambaye ataishi milele!
Acheni kumkufuru Sir god nyie lumumba....
Yu wapi Hitler,tu wapi Idd amin,tu wapi mobutu,
Yu wapi gadafi,Yu wapi Sadam husen,Yu wapi Chávez....
Kuna watu wanalopokalopoka tu

Ova
 
Back
Top Bottom