Mwanzoni mwa utawala wake ilikuwa kila gazeti linamwandika yeye tena vizuri. Vijiwe vyote kuanzia vya kahawa, daladala, bar na maofisini story alikuwa ni yeye tena watu wakimsema kama malaika mkombozi.
Ghafla upepo ukabadilika, watumishi wakaanza kukosoa utumbuaji majipu, wafanyabiashara wakakosoa mbinyo wake kwenye kodi, wanasiasa wakahoji style yake ya uongozi. Wananchi wa kawaida wakanigwa na maisha magumu (ingawa hawa bado wamebakiza kaimani fulani). Vyombo vya habari wanalalamikia kuminywa uhuru wao.
Kiujumla upepo unavuma vibaya kwa JPM naye ameshakiri ugumu wa kiti chake mpaka akasema angejua asingegombea urais. Je, rais wetu amekosea wapi mpaka hali imegeuka mapema hivyo?