Hoi hoi tunalia, machozi yatukauka
Baba tulikuzoea, vitani ulituongoza
Jemedari wetu shupavu,sasa umetangulia
Ilikuwa mitano tena,sasa imekuwa buriani!
Ulijua itakuchua, barakoa ulitwambia,
Tuzipuuzie kwa dhati, asilani tusizingatie
Kazi tuzichape,huku kifo tukikisubiri
Hati hati yako hatima, kumbe uliijua!