Magufuli alililidanganya Bunge..

Kuna kesi iliwekwa hapa kuhusu maeneo ya Mbezi na serikali ilishindwa. Nakushauri utafute huo uzi usome utajua makosa ya kukurupuka ya Magufuli. Pia kuhusu MgongoFimbo huwa anashindwa kesi za kutosha t.

Soma vizuri nilichoandika , sijakataa Serikali kushindwa na huo Uzi naujua sana. Pia fuatilia vizuri Uzi huu!
 
Ukumbuke kuwa kes unayoitaja Baus and others Na 39 ya 1997 walalamikaji walikwenda chuo kikuu kutafuta msaada wa kisheria ndipo wakakutana Prof Mugungo Fimbo. Katika hukumu Jaji wa wakati huo alisema hivi walalamikaji wameshindwa kuonyesha yafuatayo;-

1) Hawakuonyesha ardhi hiyo waliipata vipi
2) Hawakuonyesha kuwa nyumba zao kubomolewa wataathirika vipi hivyo mahakama imeshindwa kufanya comsideration ya aiana yoyote.

Kwa kauli hizi za Jaji hauwezi kuniambia kuwa kesi hiyo ilisimamiwa na Prof mtaalamu wa Land Law. Kwa kifupi kesi hiyo ni lazima iliingilwa na mkono wa serikali kutokana na walalamikaji kutumia msaada wa kisheria badala ya kulipia huduma hiyo.

Katiak kesi ya Mbezi Mwisho mawakili wa walalamikaji walifanya home work yao vyema ndio maana ushindi ukapatikana. Na usisahau kuwa kesi hii imesfanyika kwa sehemu kubwa Werema huyo huyo ndio Mwansheria Mkuu hivyo kwa kumuingiza katika mjadala huu hauna hoja.

Kuhusu barabara kupanuliwa hilo halina lkipingamizi kwani kwa mujibu wa Kanuni za Sheria ya barabara Na 13 ya 2007 zilizotolewa 2009 zinztaja kuwa lane moja ya barabara kuu hapanchini isipungue Mita 3.25. Hivyo road reserve ya Mita 30 kila upande inataosha kujenga lanes mpya 8 kila upande na kuifanya barabara ya Morogoro kuwa nia lane 18. Ni kwanini watu walioko nje ya Mita 30 walivamiwa ardhi na makazi yao? Pia katika hoja hii huana point.

Nasikitika sana kuona umeleta hoja ya kituo cha mafuta mwanza na kutoa blant accusations kuwa Magufuli alipohama wizara ndaipo wakashinda kesi. Hebu tuelimishe mawaziri wa Tanzamia wana husika vipi katika mashauri mahakamani?.
 
Reactions: mka
 

Hapo nilipo weka nyekundu - umenikatisha tamaa na sitoweza bishana na wewe tena , ila subiria kiama kikukute. Pia tafuta mtu akueleweshe concept ya Dsm-Morogoro Expressway itakavyokuwa.

Bye Watanabe!
 
Hapo nilipo weka nyekundu - umenikatisha tamaa na sitoweza bishana na wewe tena , ila subiria kiama kikukute. Pia tafuta mtu akueleweshe concept ya Dsm-Morogoro Expressway itakavyokuwa.

Bye Watanabe!
tatizo lenu wengi ni kuzungumza au kuingia kwenye arguement bila facts wal vithibitisho, nilichokutajia hapo ni ibara ya 27 910 ya kanuni za za Sheria ya barabara na 13 ya 2007 ziliopitishwa kupitia GN 21 ya 23 Jann 2009 ndio zinztamka upana huo kwa barabara zoye kuu hap nchini (Trunk roads) hivyo ukizidisha na kugawany ndio unapata kuwa road reserve y mita 30 kila upande inaweza kujenga lanes. Simple arithimetics.
 

Wewe acha kudanganya Watanganyika:

...Kwa faida ya wasomaji waendelee kusoma Ibara ya 29(2)(a)-(g) ya Kanuni ya Sheria ya Barabara Namba 13 ya 2007 zilizotolewa kupitia GN Notice No 21 ya tarehe 23 Januari 2009.
Ibara ya 29(2)(a)-(g) inazungumzia specifically Morogoro Road road reserve widths i.e.
UN Rd to km 10 = 60m
km 10 to km 16 = 90m
km 16 to km 37 = 120m
km37 to km 69 = 60m
km 69 to km 70.60 (Ruvu Bridge) = 90m and
the remainder of the road to MG = 60m.
Halafu hizo lanes hujengi kama unaanika mpunga...kuna side walks, service roads, service lines, etc

Source: 1. UTC,JF TOPIC - Re: Mahakama yamuumbua waziri Magufuli na sheria zake za uongo

2. 10th October 2013 11:04

3. UTC alikuwa akimjibu Watanabe
 

Nakushukuru sana kwa angalaukwa mara ya kwanza umeweka reference ambayo ni Kanuni za sheria mpya ya barabara Na 13 ya 2007, kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo ni kama hapakuwepo sheria kwa ni hiyo anayojigamba nayo Magufuli "The Highway Ordinance GN 161 do 1967 was invalid since 1999. Vilivile hii kama unavyoona ni amri ya kikoloni ambayo imezidiwa nguvu na Sheria ya Ardhi ya Vijiji iliyotungwa na bunge 1999. Na mahakama imetamka kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo maeneo ambayo Magufuli anayaita ni "hifadhi ya barabara" ni mali ya wananchi toka kupitishwa kwa sheria ya ardhi ya vijiji ya 1999.

Mgogoro uliopo ni msimamo wa Magufuli kuwa hakuna atakayelipwa fidia kwa mujibu wa sheria ya The Highway Ordinance ya 1967, Kanuni ambayo mahakama kuu imetamka "is invalid invalid since 1999 ( a year kabla ya Magufuli kushika madaraka hayo kwa mara ya kwanza). Kimsingi mara baada ya kutungwa kwa sheria ya barabara ya 2007 ni lazima wenye ardhi husika walipwe ikiwemo vipimo vyote ulivyovitaja hapo juu.

Kuhusu lanes nilitaka kuwthibitishia wale ambao wameaminishwa kuwa bila sisi tulioko nje ya 30 metres kuondolewa barabara haziwezi kujengwa. Ukweli ni kuwa katika hizo mita 30 kila upande lanes 16 mpya zinaweza kwa kuizngatia vipimo vinavyotajwa na kanuni zao, kwa vile hatuna uchumi wa kujenga hizo lanes 16 mpya eneo hilo linatosha kujenga lanes kwa uwezo wetu na likabaki eneo la kuweka hayo yote unayoyataja.

Nakushukuru kwa kuikubali hiyo kanuni niliyoitaja pia na upana nilioutaja unaweza kuzalisha lanes za kuutosha uwezo wa uchumi wetu hakuna sababu yoyote ya Magufuli na Tanroad kuendelea kuvamia maeneo yetu yaliyoko nje ya 30 metres ilihali kwa mujibu wa sheria zao wenyewe eneo hilo linatosha kujenga lanes nyingi kiasi hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…