Magufuli alililidanganya Bunge..

Unazungumzia kujiuzuru wakati kuna wanasiasa hata ujasiri wa kuomba radhi hawana!
 
...Watanabe rejea reply yangu #44 kwenye the same issue uliyo raise 2nd week of October kuhusu RoW specification za Morogoro kRoad!
kwa mujibu wa hukumu hii its void abinitio na kama wanapahitaji wafuate utaratibu walioelekezw na high court
 
nimefarijika sana kuona kuwa wale wasahabiki, wapenzi na die hrds wa Mhe Magufuli kidog kidog wanaanza kuutambua ukweli kuhusu alivyoweza kukumbatia na kutumia sheria feki Highway Ordinance Cap 167 kwa miaka zaidi ya 10. Kitendo chao cha kuukacha mjadala huu ni uthibitisho tosha kuwa wameelimika vya kutosha juu ya umuhimu wa kila mmoja wetu kutafuta na kujisomea sheria mbali mbali badala ya kupokea kutoka kwa watu wanaoziimba kama kusuku.
 
...Watanabe kwa kejeli kama hizo hutapata serious discussants...
 
Kajipange upya,magufuli alishachafuliwa na makampuni ya magazeti na bado akabaki magufuli yuleyule itakuwa wewe mbulula tu,tunakushukuru kwa kutuonyesha ubwege wako.
 
Sijiuzulu ng'o!

Sent from my BlackBerry 8900 using JamiiForums
 
Sijiuzulu ng'o!

Sent from my BlackBerry 8900 using JamiiForums

Yaani mnataka auache utamu wa uwaziri ili iweje? Hata mimi sijiuzulu. Lipi baya zaidi, kutumia sheria mbovu kubomoa nyumba au kuharibu misingi ya elimu na kuwadanganya waliofeli wamefaulu? Hawa wanaocheza na elimu hawawajibiki. Kwa nini yeye?
 

Hamna jipya hapa. Road reserve ikiwa ndogo ndo wa kwanza kulaumu mara ooh kwa nini hawakujua kuwa upanuzi unatakiwa baadae. Kwa ufupi makala hii ni ----- tu!
 

gazeti la Mawio Toleo Na 0067 la Oktoba 31-Nov 06, 2013
 
 

Acha kuwa kama vuvuzela

1. Kesi ya Bausi and others ya mwaka 1997 Serikali pamoja na Magufuli walishinda Kesi hiyo ktk Mahama Kuu kipindi hicho Mwanasheria wa Serikali kwa wakati huo akiwa Jaji Werema. Kesi hiyo pia iliwahusisha kina Prof Mugongo Fimbo na wezake na nyumba zikabomolewa maeneo ya kutoka Ubungo mpaka Kimara Mwisho hata mpaka Werema akapewa Ujaji .

Pia kasome sheria ya Barbara no 13 ya mwaka 2007 unaonekana hujakaa ukaisoma vyema.

Je , pamoja na Magufuli kushinda kesi hii ulitaka pia ajihudhuru?!!

2. Kesi za Samaki - akiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi alikamata Wavuvi haramu na kesi akashinda, nafikiri wajua hilo!

Je, hapa pia ulitaka Magufuli ajihudhuru?!!!

3. Haya juzi kati , Magufuli kawafukuza wakandarasi wakiitwa Progressive na wakifungua kesi mahakama kuu, vile vile akashinda.

Hapa pia ulitaka ajihudhuru??!!!

Naomba ndugu nikupe pole kwa yaliyokukuta kipindi Magufuli akitekeleza majukumu yake, pengine umeathirika kwa namna moja ama nyingine.

Na pia kesi unayosema wameshinda , inategemea na usimamizi wa kesi yenyewe - kuna mambo mengi ya kuangalia hasa nani Jaji, wakili, mwanasheria etc

Narudia tena acha umbulula!
 
wewe ni tatizo kubwa wewe yaani unasema waziwazi kwamba kushinda kesi inategemea nani jaji, wakili nk muda mfupi baada ya kuandika kwamba werema aliteuliwa kuwa jaji baada ya kutoa maamuzi in favor of magufuri alafu bado unabakiwa na nguvu za kumuita mwenzako mburula.
 

Mkuu mimi si tatizo hata kidogo ila naomba nikueleweshe kama ifuatavyo:

1. Kesi yenyewe ni Kesi ya Bausi and others kesi namba 39 ya mwaka 1997.
2. Werema enzi hizo akiwa wakili mwaminifu kabisa wa Serikali - ndo hapa nikasema inategemea kina nani wanahusika ktk kesi hiyo
3. Angalia hata mjomba wake yeye Werema aitwaye Munanka alibomoa nyumba ili kupisha Ujenzi - angalia leo hii hiyo barabara inavyowasaidia mamilioni ya Watanzania! Na tena barabara hiyo inataka kupanuliwa iwe njia sita kuanzia Dar es Salaam mpaka Morogoro ( Morogoro Expresway, 200km) kama upo ktk road reserve usijenge au kuendeleza utabomolewa tu, nafikiri mushauri na huyo mwenzako (Wantabe) anaelialia na road reserve ya Morogoro road
4. Mugongo Fimbo tena professor wa Land Law pale UDSM akiwaongoza wenzake , lakini wakashindwa - hicho ndo nataka unielewe na si vinginevyo na wala usipotoshe ninachokuelekeza !
5. Magufuli ni Waziri pekee anayesimamia sheria hasa road reserve na ndo maana unaona miradi mingi inajengwa na bila hivyo ni ndoto kuyapata haya yanayotokea ya Ujenzi wa barabara mfano: Mwenge-Tegeta, Morocco-Mwenge, Kamata - Rangi Tatu ( juzi tu wameboa nyumba), barabara ya mabasi yaendayo kwa kasi n.k
6. Bila kuwa jasiri - Wizara ya Ujenzi ni ngumu sana kutekeleza Majukumu hasa ukizubaa na kufuata hizi porojo porojo za wanasiasa uchwara

7. Ndo maana utaona Magufuli mambo yake yanaenda - lakini pia huwa anawakumbusha wananchi, kama umeonewa unaenda mahakamani.
8. Mkuu mpaka hapa kama hujanielewa basi na wewe utakuwa mbulula!

Aidha, ukae ukijua watu wanakula rushwa sana sana si ajabu kuona kesi nyingi za wazi wazi kushinda kwa upande wa Serikali unakuta eti Serikali imeshindwa. Mfano kipindi kile Magufuli akiwa Ujenzi alibomoa kile kituo cha mafuta Mwanza, wale jamaa wakaishitaki Serikali na wakaja kushinda kipindi Magufuli amehamishiwa Wizara nyingine la sivyo wasingeweza kushinda, na ndo maana utaona ile sehemu waliyobomolewa walitaka kuendelea na Ujenzi wa kituo cha mafuta wakapigwa stop!!!!! Kuna kitu hapo kilienda isivyo hebu jiulize kulikoni.

Pia, kaa ukijua wabunge wote wa CCM na wale wa Upinzani wanazijua sana sana hizi sheria so Magufuli asingekuwa anavunja sheria mbele ya bunge wakimnyamazia.
 

Kuna kesi iliwekwa hapa kuhusu maeneo ya Mbezi na serikali ilishindwa. Nakushauri utafute huo uzi usome utajua makosa ya kukurupuka ya Magufuli. Pia kuhusu MgongoFimbo huwa anashindwa kesi za kutosha t.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…