Magufuli aleta daraja kigamboni

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
Hatimae serikali kupitia wizara ya miundombinu,imedsaini mkataba wa ujenzi wa daaraja la kigamboni lenye urefu wa kilomita 4,2.
Mradi ambao utafadhiliwa na NSSF kwa asilimia 60 na serikali kwa asilimia 40,na utatekelezwa na kampuni ya china railways kwa ushirikiano na crje kutoka china pia.
Mradi utatoa ajira za kudumu zipatazo 1000 kwa wazawa kwa muda wa miaka mitatu. Na unatarajiwa kuanza tarehe mosi mwezi ujao,
MAONI YANGU
Serikali ya ccm imeepusha au kuupooza mgogoro uliokuwa unaendelea kati ya magufuli na wabunge wa dsm ambao wengi ni kutoka ccm
 
Huo mpango ulikuwapo kabla ya huyo Makufuli wenu kuwa waziri, hebu wacheni kumsifia huyo kibaraka wa Mafisadi hana lolote sifa za bure kazi Zero, arudushe nyumba zetu kwanza walizojiuzia.
 
Serikali haina hiyo 40% ya kuchangia hivyo kabla ya kusaini mkataba walikubaliana wapandishe nauli ili hiyo hela ipatikane waweze ku-top up kwenye ile 60% ya NSSF. Ni full usanii hi gov ya JK. Ndio maana yeye JK kwa kujua hilo kauchuna kimya utadhani yupo RSA kwenye centenary ya ANC!
 
Mwanzisha mada acha kupotosha kwa kichwa cha habari cha uongo.
Huo mradi ulikuwepo tangu miaka 30 iliyopita.
Angalau sema NSSF waleta daraja, nitakuelewa.
Kama hutaki PIGA MBIZI.
 
Kalileta kulitoa wapi kwao chato dah huyu mtu atakuwa baunsa ile mbaya kabeba daraja kalifikisha kigamboni?
 
Serikali haina hiyo 40% ya kuchangia hivyo kabla ya kusaini mkataba walikubaliana wapandishe nauli ili hiyo hela ipatikane waweze ku-top up kwenye ile 60% ya NSSF. Ni full usanii hi gov ya JK. Ndio maana yeye JK kwa kujua hilo kauchuna kimya utadhani yupo RSA kwenye centenary ya ANC!

ukiambiwa utoe udhibitisho wa serikali kutokua na hiyo 40% utatoa? mbona baadhi ya wana jf wazushi namna hi!! aah mnaudhi sana kwa kweli
 
Hilo daraja halitajengwa na magufuli bali ni serikali. Msimpe sifa za bure, ila tutamsifia kama atasimamia vyema katika ujenzi huo.
 
wana jf lazima 2fikir,m2 kasema kuwa maguful kaleta daraja kwa sbb yeye ndio msamiz mkuu wa kaz
 
Mwanzisha mada acha kupotosha kwa kichwa cha habari cha uongo.
Huo mradi ulikuwepo tangu miaka 30 iliyopita.
Angalau sema NSSF waleta daraja, nitakuelewa.
Kama hutaki PIGA MBIZI.
Ok ndibaleama, nimekuelewa mkuu ila niliona jina la makufuru liko chati ya juu, kwa sasa,na pia kwa sabnabu hiyp nikaongeza kwamba serikali ya ccm inaepusha mgogoro unaokisumbua chama kwa sasa kati yake na wabunge wa dsm (ccm).
 
makufuru ndo nani huyo?
 
huyu mheshimiwa magufuli aka piga mbizi alikuwa na haja gani ya kuwakejeli wakazi wa kigamboni wakati alijua fika kuna uzinduzi wa ujenzi wa daraja.kwani angeomba wananchi wavumilie bei mpya huku akiwajuza ujio wa daraja kungekua na issue hapa????
 
Mwanzisha mada acha kupotosha kwa kichwa cha habari cha uongo.
Huo mradi ulikuwepo tangu miaka 30 iliyopita.
Angalau sema NSSF waleta daraja, nitakuelewa.
Kama hutaki PIGA MBIZI.

After daraja kujengwa, najua nauli ya daladala toka kigamboni itakuwa sh. 300, si watalalamika tena ongezeko la nauli!!
 
Mshkaji wake sana bwana ODINGA.unajua masihara mengine hayafai. (KUPIGAMBIZI)lilikua neno dogo sana kisiasa si unajua ukipewa nafasi ya kuongea utani kidooogo ktk jambo la msingi.matokeo yake ndio hayo (kidaraja)pombe bwana alinifurahisha sana alipo takakujua watz presha iko vppppppppiiiiiiii!
 
After daraja kujengwa, najua nauli ya daladala toka kigamboni itakuwa sh. 300, si watalalamika tena ongezeko la nauli!!
Hata kama itakuwa shs. 500 sio tatizo kwani itakuwa ni safari ya moja kwa moja kama ilivyo safari ya Mbagala -Mwenge.
Pia hapatakuwa na upotezaji muda wa kusubiri pantoni.
 
Serikali haina hiyo 40% ya kuchangia hivyo kabla ya kusaini mkataba walikubaliana wapandishe nauli ili hiyo hela ipatikane waweze ku-top up kwenye ile 60% ya NSSF. Ni full usanii hi gov ya JK. Ndio maana yeye JK kwa kujua hilo kauchuna kimya utadhani yupo RSA kwenye centenary ya ANC!

sioni usanii wala tatizo lolote iwapo fedha zinazokusanywa zitatumika kujengea daraja.
 
After daraja kujengwa, najua nauli ya daladala toka kigamboni itakuwa sh. 300, si watalalamika tena ongezeko la nauli!!

Kwa namna moja daraja linaweza kua substitute ya panton, na pia lisiwe hivyo.
Panton unavukia ferry au magogoni karibu na kwa yule mpangaji wetu, so kama unafanya kazi Posta, au unasoma IFM inakua poa tu
But daraja unavukia vijibweni ambapo unakuja kutokea Kurasini eneo linaloitwa "Highway", ambapo mpaka uje uikute Posta itabidi upande daladala za Kariakoo-Shimo la Udongo ushukie Bandari, kisha utafute zingine za Posta kwani hizi hazifiki Posta.
Na kama ni mtu una usafiri wako binafsi, itabidi ukamuliwe mafuta zaidi kutokana na huu mzunguko ulioongezeka mpaka kuingia mjini.
Sasa wakazi wa Kigambini wanapolalamikia ongezeko la Nauli ya Kivuko, hakuna ahueni kwa uwepo wa hili daraja.
Sanasana litawasaidia wenye magari kupunguza foleni siku za wikiend wakitoka Beach.
|
Suala lingine ni kua ni wazi kua kipande cha barabara kutoka "keep-left" cha Bandari pale Kilwa Road inapoanzia mpaka "Keep-left" cha Gerezani ni chembamba mno kuweza kuhimili magari yaliyoko sasa yanayotoka Mbagala, Mtoni, Kurasini, Temeke, n.k, sasa ongezeko la magari ya kutoka Kigamboni ndio yatazidi kuongeza foleni, hivyo ujenzi wa daraja la kigamboni uende sambamba na upanuzi wa kipande hicho kinachopita pale nje ya BP.
 
Back
Top Bottom