Magufuli aiteka Manyara na kuizika UKAWA

Magufuli aiteka Manyara na kuizika UKAWA

Mr Chin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
4,625
Reaction score
1,024

Mkutano wa hadhara wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ukiendelea katika uwanja wa Kwaraha, wilayani Babati mkoani Manyara jioni ya leo, ambapo umati mkubwa wa watu ulijitokeza kusikiliza sera zake.PICHA NA MICHUZI JR-BABATI,MANYARA.

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia na kujinadi kwa kijinadi kwa Wakazi wa mji wa Babati mjini na Vitongoji vyake kwenye mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kwaraha,mkoani Manyara.

Wakazi wa mji wa Babati mjini na Vitongoji vyake wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao na kuwaomba kura za kutosha ifikapo Oktoba 25 Mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu,ili awe Rais wa Tanzania wa awamu ya tano.Mkutano huo wa hadhara uliofana kwa kiasi kikubwa ulifanyika mjini humo katika uwanja wa Kwaraha,mkoni Manyara.

Maelfu ya wakazi wa mji wa Babati wakiwa wemekusanyika katika uwanja wa Kwarahaa mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,alipokuwa akiwahutubia mjini humo mkoa wa Manyara.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Babati wakishangilia jambo wakati mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye uwanja wa Kwaraha,mkoani Manyara.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akijinadi mbele ya Wakazi wa mji wa Babati mjini na Vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kwaraha,mkoani Manyara.

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea Ubunge,Mbunge wa Babati vijijini Ndugu Jitu Soni ambaye tayari alikwisha kabidhiwa kitabu cha Ilani ya CCM

Maelfu ya wakazi wa mji wa Babati wakiwa wemekusanyika katika uwanja wa Kwarahaa mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,alipokuwa akiwahutubia mjini humo mkoa wa Manyara.

Mgombea Ubunge wa jimbo la Hanang,Mama Mary Nagu akimuombea kura mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wakazi wa mji wa Babati mjini jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni,uliofanyika katika uwanja wa kwaraha.

Maelfu ya wakazi wa mji wa Babati wakiwa wemekusanyika katika uwanja wa Kwarahaa mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,alipokuwa akiwahutubia mjini humo mkoa wa Manyara.

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji wa Kondoa mapema leo mchana kwenye uwanja wa sabasaba,amapo mkutano wa hadhara wa kampeni ulifanyika.Dkt Magufuli akitokea mkoani Singida kuelekea mkoani Manyara kuendelea na kampeni zake za kusaka Urais,aliwahutubia wakazi wa wilaya ya Chemba,wilaya ya Kondoa,na vitongoji vingene kadhaa na hatimae kuibukia wilayani Babati na kuhutubia mkutano mkubwa katika uwanja wa Kwaraha.
​

12118816_887749144649677_7934887807908940614_n.jpg

Yaani hapa tupo kwenye ng'ome yao... MANYARA OYEEE... HAPA KAZI TU
 
Ndio maana lema kaingiza baridi
 
Ukweli mchungu ila lazima usemwe. Magufuli ndiyo kiongozi pekee anayehitajika kwa Tanzania ya Leo.Waliozoea kutuibia na kutunyonya wamekimbia kwenda kujificha kwenye kichaka cha CHADEMA. Wanawalaghai wananchi kwa kuimba wimbo wa Mabadiliko kumbe wanamaanisha hivii; {Mabadiliko ya kupiga dili kupitia CHADEMA Kama watashinda}.
 
Hii nyomi inaongeza level ya anxiety na fear pale Ufipa. Huyu ndiye rais wetu, Mungu ampe afya na hekima
Kingunge naye eti anataka MABADILIKO. Toka lini Team Lowassa wakataka mabadiliko? Toka wampokonye dili la kukusanya ushuru pale Ubungo terminal Mzee amechanganyikiwa.
 
Ukweli mchungu ila lazima usemwe. Magufuli ndiyo kiongozi pekee anayehitajika kwa Tanzania ya Leo.Waliozoea kutuibia na kutunyonya wamekimbia kwenda kujificha kwenye kichaka cha CHADEMA. Wanawalaghai wananchi kwa kuimba wimbo wa Mabadiliko kumbe wanamaanisha hivii; {Mabadiliko ya kupiga dili kupitia CHADEMA Kama watashinda}.
Maraisi wote kuanzia wa sasa na waliotangulia sijasikia yupo aliyehamia Chadema na wote pamoja na kuwa wakuu wa nchi na serikali walikuwa pia ni wakuu wa chama tawala CCM. Mwinyi hajahama, Mkapa hajahama na Kikwete ndiye sasa kwa miaka yake 10, kashfa za kifisadi zimeandama serikali yake hadi anashindwa kutulia nchini. Kila siku kiguu na njia angani kutembeza bakuli baada ya kukomba pesa zote hazina, hadi wengine wakisikia yuko njiani wanafunga milango. Come on COARTEM be serious, lini na wapi Lowassa aliwahi kuwa Jemadari Mkuu wa taifa hili?

attachment.php

Watanzania wamechoka na ulaghai wa miaka 50ya CCM, na sasa wako tayari kwa mabadiliko...Tanzania bila CCM yawezekana sana tu.
 
wakuu hivi yale majina matano kule dodoma yalitoka kwenye mfuko wa jk au mkapa? nimesahau kidogo wakuu...
 
hii nyomi inaongeza level ya anxiety na fear pale ufipa. Huyu ndiye rais wetu, mungu ampe afya na hekima

ebu waacheni wasanii na fiesta tuone hiyo nyomi mnayojivunia
unajua mtashangaa sana wakati matangazo ya urais yatakapotangazwa? Maana mnadhani watu kuja kuona fiesta wamekubali sera za ccm hapana watu walishaichoka ccm hakuna jinsi ya kujinasua mwaka huu
 
Mr. Chin bana, daaaah natamani kukuona hta kwa mbali. Umesahau kabisa kama hii ni Fiesta??? Pole sana kuweni na ufaham bac hata kidogo
 
Mkutano wa kampeni ulikuwa siku timu UKAWA walivyopita hapo , hii ya jana watu walienda kutizama burudani ya wasanii, tusubirini tarehe 25 October tujionee
Magufuri mpaka nyomi anaiba, nyomi za wasanii anaondamana nao anazikusanya zote katika kiwanja kimoja anasema ni zake! Lowasa haitaji msanii kupata nyomi za uhakika.
 
ebu waacheni wasanii na fiesta tuone hiyo nyomi mnayojivunia
unajua mtashangaa sana wakati matangazo ya urais yatakapotangazwa? Maana mnadhani watu kuja kuona fiesta wamekubali sera za ccm hapana watu walishaichoka ccm hakuna jinsi ya kujinasua mwaka huu
Kuwa muwazi..hilo bandikolako linawakilisha fikrazako pamoja na za mumewako
 
Watu wanaenda kuangalia show za diamond na si vinginevyo,magufuri hana cha kuwavutia watu kwenda kwenye mkutano, ni show tu ndio zinawapeleka.
 
Kingunge naye eti anataka MABADILIKO. Toka lini Team Lowassa wakataka mabadiliko? Toka wampokonye dili la kukusanya ushuru pale Ubungo terminal Mzee amechanganyikiwa.
Mzee ana tamaa sana huyu ndo maana kuna kipindi jinalake lilikuwa associated na ufisadi, ubinafsi na tamaa ya madaraka wa hali ya juu...jinalake sio symbol nzuri kabisa
 
Back
Top Bottom