Magufuli airudishia pumzi CCM Arusha, Waibwaga CHADEMA

sirjohn

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
767
678
Kuna habari nimeiona ikisema Magufuli airudishia CCM pumzi Arusha, inasemekana kulikuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa, CCM wameshida. Mwenye taarifa kamili atujuze.

Hapa CCM wajifunze kuwa wananchi wanataka KAZI TU na siyo maneno maneno ya kwenye kanga bila kazia..mfano wataisoma namba nk.

MY TAKE

Wananchi msije mkafanya kosa hasa 2020 kuiapa ushindi CCM kwa kila ngazi hakikisheni upinzani unakuwa na kuongezeka hasa bungeni ikiwezekana iwe 50/50 na hapo ndipo tutawapata akina Magufuli wengi..
 
Hatimaye Kasi ya Magufuli yaanza kurejesha heshima ya CCM ndani ya Jiji lililokuwa ngome ya Chadema...jiji la Arusha.

Chadema yaangukia pua kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mitatu ya jiji la Arusha.

Ninachowapendea watu wa Arusha ni msimamo usio na unafiki...ukiwapuuza wanakupotezea...
 
SOURCE PLZ.

NA NI MITAA IPI, NA PIA MH. MAGUFULI AMEHUSIKAJE HAPO???
 
Kuna habari nimeiona ikisema Magufuli airudishia CCM pumzi Arusha, inasemekana kulikuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa, CCM wameshida. Mwenye taarifa kamili atujuze.

Hapa CCM wajifunze kuwa wananchi wanataka KAZI TU na siyo maneno maneno ya kwenye kanga bila kazia..mfano wataisoma namba nk.
A
MY TAKEd

Wananchi msije mkafanya kosa hasa 2020 kuiapa ushindi CCM kwa kila ngazi hakikisheni upinzani unakuwa na kuongezeka hasa bungeni ikiwezekana iwe 50/50 na hapo ndipo tutawapata akina Magufuli wengi..
Kama umepagawa vile kamanda,kwa upinzani upi hasa wa kutoa 50-50?
Huwezi kuingia ikulu kwa ghilba za kuzungurusha mikono na kunywa uji sokoni tandika au kupanda daladala gongo la mboto
 
Kama umepagawa vile kamanda,kwa upinzani upi hasa wa kutoa 50-50?
Huwezi kuingia ikulu kwa ghilba za kuzungurusha mikono na kunywa uji sokoni tandika au kupanda daladala gongo la mboto

Chochote kwenye siasa kinawezekana. Hakuna mtu alijua mwaka jana ingeweza kuwa vile......
 
Chochote kwenye siasa kinawezekana. Hakuna mtu alijua mwaka jana ingeweza kuwa vile......
Upinzani wa Tanzania umejengwa na matukio ya makosa ya serikali ya awamu ya nne pamoja ghilba,
Ndio maana mpaka leo miezi sita baada ya uchaguzi hutajaona maandamano wala operesheni sangara
Watu wanatafakari kila kete wanayotaka kuitumia haina mashiko,labda Lugumi nayo itategemea bungeni itakuaje .
Kama mambo yakiwa hivi 2020 wazungurusha mikono itabidi labda wazungurushe viuno ndio wataeleweka kwa wananchi
 
yaan uchaguzi wa mitaa nane na saba ilikuwa ya ccm halafu wakashinda 2 na moja ya tatu walimnunua mgombea wa chadema akajitoa. Chadema wao wameshinda tano nani kapoteza? kweli macc kwa akili ya kawaida nani kapata?
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
WILAYA YA ARUSHA MJINI
S.L.P 12525, NGARENARO - ARUSHA

MATOKEO YA UCHAGUZI WA MARUDIO WA SERIKALI ZA MITAA, 2016
ARUSHA MJINI

1. ELERAI - AZIMIO CHADEMA 524 VS ccm 283
2. ELERAI - MAMA MUSA CHADEMA 196 VS ccm 166
3. MOSHONO - KALIMAJI ccm 199 VS CHADEMA 167
4. KATI - BONDENI ccm 207 VS CHADEMA 110
5. SINONI - MAKAO MAPYA ccm 338 VS CHADEMA 262
6. DARAJA II - NDARVOI CHADEMA 452 VS ccm 181
7. DARAJA IISANARE CHADEMA 381 VS ccm 381
8. SOMBETINI - OLAMURIAKI ccm (KO) VS CHADEMA (Tulikimbiwa na Mgombea wetu)

Maelezo sahihi;
Baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 14/12/2014
ccm MITAA 78
CHADEMA MITAA 76
JUMLA ni MITAA 154

Katika Uchaguzi huu wa Marudio wa Serikali za Mitaa
Wenyeviti wa ccm waliojiuzulu nyadhifa zao na kuhamia CHADEMA 7
Mwenyekiti mmoja (1) wa CHADEMA alifukuzwa Uanachama 1
Jumla ya nafasi zilizogombaniwa ni nane (8)
ccm Viti 4
CHADEMA Viti 3
Mtaa mmoja wa SANARE Kata ya DARAJA MBILI Uchaguzi utarudiwa kwa sababu Wagombea kura zimelingana

Current status

CHADEMA Viti 78
ccm Viti 75

Imetolewa na;

KURUGENZI YA HABARI NA MAWASILIANO
CHADEMA WILAYA YA ARUSHA MJINI
 
Watu wa lumumba hata hawaelewi nini kinatokea Arusha..wanasoma tu gazeti la uhuru.....tulizen sis huku tuwaambie kuwa Chadema imeongeza mitaaa iliyokuwa yenu....na bado mtaa mmoja tunasubiri kurudia uchaguz...
 
Lumumba tatizo kweli. Yaani 2014 serikali za mitaa ccm walikuwa kileleni, tumefanya uchaguzi wa marudio mitaa 8 tu. CHADEMA tupo kileleni. Alafu MTU mtu anasema. Magufuri kawaongezea pumzi ccm!!! KWELI AKILI NDOGO HAIWEZI KUTAWALA AKILI KUBWA
 
Viti 6 chadema 2 ccm, sasa hapo ingekuwa anagalau 4 kwa 4 ccm si wangefanya maandamano ya ushindi nchi nzima? Mnasikitisha sana kupata viti 2 ndio kusema mmeimwaga chadema? Mtasubiri sana. Kuna mtaa mmoja ccm imepata kura 181, chadema 452, mtaa mwingine ccm 283 chadema 524, ccmhap nddio mna imba wimbo wa Magufuli mpango wa Mungu, hamna hata haya kusema mmeigaragaa chadema?!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom