Magufuli aibua mjadala nafasi ya Gavana BoT

Magufuli aibua mjadala nafasi ya Gavana BoT

mtotomtamuu

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2016
Posts
602
Reaction score
1,464
Dar es Salaam. Kuenguliwa kwa Lawrence Mafuru
kutoka nafasi ya Msajili wa Hazina, kumeibua
mjadala wa nafasi ya Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu, ambaye
alikuwamo kwenye Bodi ya Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) ambayo Rais aliivunja mwezi
uliopita.
Kuondolewa kwa Mafuru na nafasi yake kujazwa
na Dk Oswald Mashindano, kunaweza kuwa ni
moja ya muendelezo wa harakati za Rais John
Magufuli kutengeneza timu yake ambayo anaamini
itaendana na kasi yake.
Mafuru, ambaye aliteuliwa kushika nafasi hiyo
mwaka 2014, aliondolewa siku chache baada ya
kutoa kauli iliyoonekana kutofautiana na ya Rais
kuhusu suala la wakurugenzi wa taasisi za umma
kuweka fedha kwenye akaunti za muda maalumu
na baadaye kuchukua ongezeko linalotokana na
riba, kwa ajili ya matumizi yao binafsi.
Wakati Rais akisema wakurugenzi wakuu wa
taasisi za Serikali huweka fedha kwenye akaunti
hizo maalumu na baadaye kujinufaisha na riba,
Mafuru alisema haiwezekani watumishi hao
kuchota fedha za umma kutoka benki kwa kuwa
miamala ni ya wazi na akaongeza kuwa
wamemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kuzikagua.
Kauli yake ilikuja siku mbili baada ya Gavana
Ndulu kutoa kauli kama hiyo akiwa mjini Arusha,
aliposema kuwa hakuna sheria inayozuia taasisi za
Serikali kuweka fedha kwenye akaunti ya muda
maalumu, ambazo riba yake huzalisha faida
ambayo Rais Magufuli alisema imekuwa ikichotwa
na kutumiwa kwa masilahi kwa binafsi na viongozi
wa taasisi hizo.
Mjadala huo usio rasmi uliibuka baada ya Rais
Magufuli kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi
ya TRA, Bernard Mchomvu Novemba 20 na
kutangaza kuivunja bodi yote.
Siku nne baadaye, Rais alisema alichukua uamuzi
huo baada ya bodi kuidhinisha maombi ya TRA ya
kuweka fedha kwenye akaunti ya muda maalumu.
“Juzi hapa tumekuta Sh26 bilioni zilizokuwa
zimetolewa TRA kwa ajili ya matumizi ya TRA,
zikapelekwa kwenye mabenki matatu kama ‘fixed
deposit account’ na bodi ikapitisha. Ndiyo maana
nilipozipata hizo hela, nikazichukua na bodi
kwaheri,” alisema Rais Magufuli alipokuwa mgeni
rasmi kwenye mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania (OUT).
Tangu wakati huo, Rais hajatangaza hatua zozote
dhidi ya wajumbe wa bodi hiyo, ambao watano kati
yao wanaingia kutokana na nyadhifa zao. Wajumbe
hao ni Gavana wa BoT, Kamishna Mkuu wa TRA,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha Zanzibar na Katibu Mkuu wa
Mipango.
Lakini kati yao, ni Gavana Ndulu pekee
aliyejitokeza kuzungumzia suala hilo, na kauli
yake—kama ilivyokuwa ya Mafuru—inaonekana
kutofautiana na Rais Magufuli.
“Kwani (Rais) amesema fixed account zote ni
mbaya pamoja na za watu binafsi? Ndiyo hivyo
sasa. Nilijua mtachomekea hilo kwa hiyo nilikuwa
tayari,” alisema mhadhiri huyo wa zamani wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati
alipozungumza na waandishi mjini Arusha
alikoenda kuhudhuria mkutano wa taasisi za fedha.
Wadadisi wanasema hiyo inaweza kuwa sababu
kubwa ya Rais kufanya mabadiliko kwenye nafasi
hiyo.
Sababu ya pili inayoweka rehani nafasi ya Gavana
Ndulu ni ukweli kwamba alikuwa mjumbe wa bodi
ambayo iliidhinisha fedha kuwekwa kwenye
akaunti ya muda maalumu baada ya Rais kutoa
maagizo ya kuzuia fedha za umma kuwekwa
kwenye akaunti hizo.
Ukiacha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha - Zanzibar,
wateule wengine watatu—Kamishna Mkuu wa TRA,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha (Muungano) na
Katibu Mkuu wa Tume ya Mipango—ni wateule
wapya na huenda bado ana imani nao.
Sababu nyingine ambayo si muhimu sana lakini
inayoweza kuwa na maana kipindi hiki, ni ukweli
kwamba Rais anapanga safu yake ya uongozi, hasa
katika taasisi nyeti.
Ndulu amekuwa kwenye nafasi hiyo tangu mwaka
2008 baada ya aliyekuwa Gavana, Daudi Balali
kuenguliwa kutokana na sakata la malipo ya fedha
kwa wafanyabiashara kutoka Akaunti ya Madeni ya
Nje (Epa).
Baada ya kufanya kazi na Gavana Ndulu kwa
mwaka mmoja, sasa Rais Magufuli anaweza
kufanya mabadiliko ya mkuu wa taasisi hiyo nyeti
bila ya kuweka hofu kwa jumuiya ya wahisani,
wafanyabiashara na wawekezaji, ambao uamuzi
wao kuhusu masuala ya kifedha hutegemea uimara
wa chombo hicho.
Wachambuzi wazungumza Profesa wa Uchumi
katika Kilimo wa Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua),
Damian Gabagambi alisema kwa sababu Rais
hakusema sababu za kutengua uteuzi wa Msajili wa
Hazina, inawezekana zipo nzuri na tofauti kabisa.
Alisema kama sababu ni kuhusu kupishana kwa
kauli zao kama ilivyokuwa kwa Mafuru, basi na
nafasi ya Gavana itakuwa shakani kwa sababu na
yeye alifanya jambo kama hilo.
Alisema pamoja na mambo yote, bado ipo haja ya
kufikiria mara mbili kuhusu Gavana kwa sababu
yupo katika nafasi nyeti na inayohitaji umakini na
kuaminika zaidi.
“Kama kweli sababu zinazodhaniwa, ambazo mimi
binafsi hainiingii akilini kuwa nchi imefika hapa
ilipo zikiwa kweli, basi hakutakuwa na maoni ya
kitaalamu badala yake watu watatoa kulingana na
Rais anataka kusikia nini.
“Kwa utaratibu huo nchi itakuwa na wanafiki
badala ya watendaji wanaofanya kazi, kutoa maoni
kitaalamu, tutafurahi kwa muda mchache, lakini
baada ya muda tutagota,” alisema Profesa
Gabagambi.
Naye Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu
cha Ruaha (Ruco)
alisema kama sababu zilizomuondoa mtu makini
kama Mafuru ni hizo litakuwa siyo jambo zuri kwa
maendeleo ya nchi.
“Kama sababu ni hiyo, ina maana wale wote
waliopingana na Rais katika kutoa maelezo ya
kitaalamu wajiandae akiwamo Gavana, ingawa
kuna ukakasi kukubali na kuamini kuwa mtu
anayejibu kitaalamu anaonekana mbaya sababu tu
watu wanataka kusifi alisema.
“Kama hivyo ndivyo, hali ita mbaya zaidi huko
baadaye na ha mtaalamu atakayetoa maoni hata
yatakapohitajika kwa mustakaba Taifa, ”alisema
Profesa Mpangala Gavana Ndulu alipoulizwa ku
suala hilo alijibu kwa kifupi, “siyo Ikulu siwezi
kulizungumzia kwa heri”.
Wadau wamzungumzia Mafuru Kwingineko,
wasomi na wana wamedodosa mabadiliko yaliyofa
na Rais, wakitaka madaraka yake galiwe upya
katika Katiba Mpya.
Mafuru aliondolewa katika n hiyo wakati Rais
alipotangaza ma liko ya watendaji katika serikali
ambako aliyekuwa msemaji wa Christopher Ole
Sendeka anaye Mkuu wa Mkoa wa Njombe, uteu
balozi mmoja na mabadiliko ya m tibu wakuu wa
wizara.
Akizungumzia mabadiliko hayo fesa Kitila Mkumbo
wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Chang’ombe
(Duce), alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano
inampa mamlaka makubwa Rais.
“Huo ni mtindo wake wa uongozi na Katiba ya
Jamhuri inampa madaraka hayo. Swali ni kwamba
madaraka hayo ni sahihi? Anaweza kuteua na
kutengua wakati wowote bila kushauriana na
yeyote? Hii ndiyo sababu ya wananchi kutaka
mabadiliko ya Katiba kwa sababu inamfanya kuwa
kama mungu wa pili,” alisema.
“Anachokifanya Rais Magufuli ni ushahidi wa kile
tulichokuwa tunakisema kinadharia kuhusu
madaraka makubwa aliyonayo Rais. Anatusaidia
kutuonyesha ubovu wa Katiba yetu na sababu ya
kutaka mabadiliko.”
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, Julius
Mtatiro alisema mabadiliko hayo ni staili yake na
kwamba itaendelea hadi 2020.
“Ukichunguza hizi sekta na taasisi anazohamisha
watendaji wake hazipigi hatua. Hali hii
inasababisha kusiwe na taasisi imara,” alisema
Mtatiro.
Mtatiro alisema inaonyesha kama Rais amelipiza
kisasi kwa mtaalamu aliyetoa maoni yake
hadharani yaliyokwenda tofauti na alichokisema
yeye.
“Hii ni sms (ujumbe) kwa watendaji
watakaokwenda kinyume na kwa kila jambo
analoliamini Rais Magufuli.
Mafuru alisimama katika ukweli kutokana na
profession (utaalamu) yake,” alisema.
Mjumbe wa Jukwaa la Katiba, Hebron Mwakagenda
alisema Katiba za nchi nyingi zinatoa madaraka
kwa marais kuteua na kutengua viongozi na
watendaji wa Serikali bila kushauriwa na mtu.
“Sina tatizo na hilo, ila kwa watumishi wa umma,
anapaswa kuangalia. Tumekuwa tukisikia watu
wakitenguliwa na kuambiwa watapangiwa kazi
nyingine, lakini hadi leo hawajapangiwa. Akiteua
mkurugenzi mwingine wanakuwa wawili, ila
mmoja anafanya kazi, kwa hiyo hapo kubana
matumizi hakupo tena,” alisema.
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Juju Danda
alisema hakubaliani na uamuzi huo wa Rais
kumuondoa Mafuru kwa kuwa hakulenga
kumkosoa Rais.
“Ifike mahali Rais aweke utaratibu wa kuamini
watendaji wake. Sikuona kosa la Mafuru... ni
mtaalamu na alikwenda kufafanua hoja,” alisema
Danda.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum
Mwalimu alisema suala la panga pangua si jambo
baya na geni kwa Rais Magufuli ila sababu
zinaweza zikawa shida.
“Leo hii ukiniuliza Rais Magufuli katika panga
pangua yake amelenga nini sijui? Kwa sababu yupo
katika kila sekta na kazi zote anazifanya yeye,”
alisema Mwalimu.
Alisema haoni tatizo la akaunti za muda maalumu
na kwamba Mafuru alieleza vizuri na si kisiasa
kwa kuwa ni mtaalamu. “Sina uhakika kama ni
sababu ya kueleza ukweli ndiko kumemponza au
la? Kama zipo sababu Rais atueleze,” alisema.

Source: Mwananchi
 
Sijui kwanini Rais wetu hapendi kukosolewa. Nadhani ifike mahali tukubaliane kuwa panga pangua inaligharimu taifa na si ajabu muda wake wa kipindi cha miaka mitano ukaisha akipanga pangua na tukabaki tulivyo.
 
Sijui kwanini Rais wetu hapendi kukosolewa. Nadhani ifike mahali tukubaliane kuwa panga pangua inaligharimu taifa na si ajabu muda wake wa kipindi cha miaka mitano ukaisha akipanga pangua na tukabaki tulivyo.
Hapana usimkosoe hadharani.....hiyo ni insubordination/dharau....tafuta faragha mshauri mpe pross and cons uone kama hutosikilizwa...usisikilize maneno ya wazushi
 
Jamani, kwanza tuelewane,

Huwezi ukampinga Kiongozi wa nchi [Rais] mbele ya vyombo vya habari hata kama hajasema ama kuamua vizuri hili tuelewane hutakuwa sahihi.
Hapa hapa mwanaJF alitoa uzi kuwa ili upate ajira na ukae kazini usimpinge boss wako na kujionesha kuwa wewe unajua kuliko boss wako.

Haya twende tuangalie mfano mmoja, pale Marekani jenerali mmoja wa jeshi alimpinga rais Obama hakuchukua mwezi kazini aliondolewa, naye alifanya kama Mafuru kwenye vyombo vya habari.

Hata nyumbani pia, huwezi ukampinga Baba ama Mama / Mzazi wako mbele ya majirani zenu ama mbele za wadogo zako (mzazi ataeleza/kuongea jambo kama hayuko sawa , unamfuata baada ya pale unamwambia , lakini Baba ama Mama , jambo hili ukilifanya hivi halitafanikiwa ila hapa halitakuwa sawa Mzazi atakuelewa ila ukipayuko mbele za kila mtu lazima utaonekana huna akili kabisa na mzazi anaweza akakuchukulia hatua za ziada kwa kutomtii ama kumstahi).

Kwa hiyo Mafuru alikosea sana kuongea na kumpinga Rais kwa njia ile.


Pili, Mafuru kama mtaalam sawa alifanya waliyofanya juu ya FD Acc, ila ikumbukwe kuwa Rais yeye ameishakataza hela kuwekwa huko Fixed Deposit Account na hili tunasema kuwa ameonewa mtu?
Rais amesema anaelewa hela ya mashirika ya umma inavyochezewa kwa FDA, amekataa yeye na wenzake wanaitetea hiyo FDA, sasa kwa nini yeye Mafuru asielewe kuwa walikatazwa kuweka huko hela .

Sawa sikatai kuwa labda hakuna faida kuweka huko hela ila mwenye hela kasema hapana ilikuwa jambo rahisi tu kama wataalam na wasomi na uzoefu wao ni kuacha na baadaye kumueleza Rais kuwa serikali itapata hasara hii na hii kama hela haziko huko katika FDA na hata baadaye wamuite na kumuonesha hasara tuliyopata ni hii hapa kwa kutoweka hela katika FDA na siyo kutumia vyombo vya habari kama walivyofanya.

Ila kwa ujumla, Rais hakuamka tu na kuongea juu ya hayo yote atakuwa alipata taarifa sahihi juu ya yale yanayofanyika juu ya FDA na mishara kule hazina.


Ila mimi binafsi , naona Mafuru kala matunda ya maneno yake na amejitakia ''''' Ukimuuliza mtu yeyote mwenye hekima na anafanya kazi ofisini atakueleza kuwa Ex- Mhazina amekosea kuongea vile hata kama "alikuwa sahihi kwa alichosema".

Kuhusu Prof. Ndulu naye afate mkondo tu , hamna namna hasa pale unapokuwa na wafanyakazi wanaokupinga katika utendaji kazi wako na maono yako; hutafika kabisaa bora uwaondoe ufanye na wanoelewa unachohitaji kufanya.

Pia, binafsi nampongeza Rais. Magufuli kwa kumuondoa Mafuru, na wengine wangefatia kutimuliwa tu maana , ni lazima nchi iwe na msemaji siyo kila mtu tu anachomoka na kuongea chochote.


Ahsanteni.
 
Ila sidhani kama tatizo ni Rais kutotaka kukosolewa tatizo ni dhani ya upigaji dili" maanake iweje tatizo litokee TRA halafu wewe wa sekta nyingine uje utolee ufafanuzi? Haya utasema wao ni wajumbe wa bodi sasa mjumbe wa bodi ni ananguvu ya kujitetea kuliko mwenyekiti au katibu wa bodi? Hao wengine wote ni wanavitengo vikubwa kama cha usajili wa hazina au gavana huoni kuwa hivi vitu vinategemeana TRA wao wanakusanya mapato, Benki kuu ndio benki mama ambapo benki zote zinategemea hapa na ndani yake kuna kitengo cha hazina ambacho kinajihusisha na utunzaji wa fedha. Haya mfano rais alisema account za fedha za umma zipelekwe Benki kuu, wewe huoni hili ni kosa kwamba TRA wamekiuka huu utaratibu kwa kuweka fedha kwenye benki wanazozijua wao? Pili Gavana ndio kiongozi wa benki kuu na ni mjumbe wa bodi ya TRA hauoni nae atakuwa amekiuka hili agizo kwasababu yeye ndie anaepaswa kuhamasisha wizara zipeleke fedha za account zao benki kuu.Tatu msajili wa hazina hauoni pia anakosea kwasababu yeye anapaswa kupokea kiasi anachopewa na wizara husika na kukitoa kwa kadri inavyotakiwa na sio kutafuta riba kwenye pesa alizopewa? Mwisho pia kwanini waje watolee ufafanuzi huku kwenye media wasikae chini na Rais waongee naye kama hawakufikia muafaka au wameonewa basi wajiuzulu, ndio maana Rais amemsimamisha kazi Msajili wa hazina amesema atamtafutia kazi nyingine hii inamaanisha amepisha uchunguzi ikionekana hana hatia basi atarudishwa.
 
Hapana usimkosoe hadharani.....hiyo ni insubordination/dharau....tafuta faragha mshauri mpe pross and cons uone kama hutosikilizwa...usisikilize maneno ya wazushi
Hakuwa anakosoa, alikuwa akijibu hoja kwa kutumia taaluma yake. Tufike hatua tutambue na kuheshimu taaluma za watu!
 
Back
Top Bottom