Magufuli aagiza wanafunzi wasafiri bure

Magufuli aagiza wanafunzi wasafiri bure

AUDITOR OF MAFISADI

Senior Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
106
Reaction score
34
Pombe-11Agust2015.jpg

Serikali imeagiza wanafunzi na watu wenye ulemavu katika Manispaa ya Mtwara Mikindani na kata ya Msangamkuu, watasafiri bure kwenye kivuko cha Mv Mafanikio.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, wakati akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuzindua kivuko hicho.

Alisema wanafunzi wote waliovaa sare za shule hawatatozwa nauli kutokana na kundi hilo kuwa tegemezi.

"Walemavu na wanafunzi watavuka bure bila kutozwa hata shilingi 10, ili mradi tu awe amevaa sare za shule na walemavu pia hawatatozwa pesa yoyote na kwa wengine ni lazima tuendelee kuchangia mafuta ili kivuko hiki kitusaidie na kuwa endelevu," alisema.

Magufuli alisema kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100 pamoja na magari kimegharimu Sh. milioni 3.3, fedha kutoka serikalini.

Akihutubia wananchi wa Msangamkuu pamoja na Mtwara wakati wa uzinduzi huo, Rais Jakaya Kikwete alisema serikali imetatua kero hiyo ya kivuko iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda mrefu.

"Kupatikana kwa kivuko hiki ni fursa nzuri kwenu kitumieni kwa kuuza bidhaa mbalimbali, kama mkazi wa Msangamkuu una ming'oko yako unahitaji kwenda kuuza mjini tumia kivuko hiki kwa maendeleo yenu" alisema Rais Kikwete.

Alisema kutokana na wakazi wa maeneo hayo kukosa kivuko tangu kupatikana kwa uhuru, watu wengi walipoteza maisha na kuwataka kukitumia kivuko hicho vizuri.

Chanzo: Nipashe

kivuko kimegharimu milioni tatu na laki tatu (3300000 ) /= tu!!!!!!! tafadhali acha masiala,au umekosea kutaipu. Uwenda ulitakakusema bilioni 3.3.
 
Unaweza dhani ana huruma sana kumbe ni mbinu ya kisiasa tu. Kama kweli anajali kiasi hiki, mbona wale wengine aliwaambia wapige mbizi? Kweli siasa!!!
 
hawa ndio viongozi wanao jali wananchi.....................
 
From KUPIGA MBIZI hadi kusafiri BURE!

Eti bado kuna Watanzania hawatagundua hii janja ya nyani?

Kweli ndio maana mnanunuliwa kwa kilo ya chumvi na mche wa sabuni.
 
Kenya vivuko vyote bure kwa watembeao. Magari pekee ndiyo yanayochajiwa. Hili liserikali letu halina hata kitu kimoja linachokitoa kama service ya bure tu kwa wananchi wanaotoa kodi? Halafu wanataka washukuriwe kwa hili kama 'fadhila'. Kama hili lisirikali litarudi, daraja la Kigamboni watu watachajiwa shs. 1000.... Uroho wa pesa tu wa jiserikali hili. Kama wakichaji gari pekee sh. 2000 natumai zinatosha kwa mafuta na mishahara. Ila kuna mtu ataka apate zake kila mwezi!
Imagine mtu anaefanya kazi za ndani Dar anayelipwa 50,000 tu, nusu zitakwenda kulipia daraja!( Jiserikali letu halijali kuweka sheria ya malipo ya hawa wanaokandamizwa na wageni matajiri. Utakuta wanafanyishwa kazi masaa 16)
 
Hapo ndiyo utampenda magufuli maamuzi yameshaanza kuwatumikia watanzania kwa tija.
 
Hawadanganyiki, mateso waliyopata watu wa Mtwara na Lindi kutoka vyombo vya dola dhalimu ya CCM ni vigumu kuisamahe CCM.
 
Wakati huu wa vuguvugu la uchaguzi watawajali sana. Subiri uchaguzi upite.
 
Kenya vivuko vyote bure kwa watembeao. Magari pekee ndiyo yanayochajiwa. Hili liserikali letu halina hata kitu kimoja linachokitoa kama service ya bure tu kwa wananchi wanaotoa kodi? Halafu wanataka washukuriwe kwa hili kama 'fadhila'. Kama hili lisirikali litarudi, daraja la Kigamboni watu watachajiwa shs. 1000.... Uroho wa pesa tu wa jiserikali hili. Kama wakichaji gari pekee sh. 2000 natumai zinatosha kwa mafuta na mishahara. Ila kuna mtu ataka apate zake kila mwezi!
Imagine mtu anaefanya kazi za ndani Dar anayelipwa 50,000 tu, nusu zitakwenda kulipia daraja!( Jiserikali letu halijali kuweka sheria ya malipo ya hawa wanaokandamizwa na wageni matajiri. Utakuta wanafanyishwa kazi masaa 16)

unazungumzia kenya ipi we mtu mambo yenu ya kikabila huko kenya na alshababu wenu usituletee huku.
 
Back
Top Bottom