Magufuli, a one man show nani atamfunga speed governor akikosea?

Na bado. Mmezowea uhuni uhuni. JK mlidema dhaifu huyu one man show,wabunge kazi yao nini? Mlipoweka mafuriko shoe output ilikuwa nini. Tulip mchagua tutamdhibiti kama huwaamini wabunge uliowachagua. Tulimkataa mwizi ili tudhibiti wezi. Na uwezo wako wa matumizi ya akili yako yanajidhihirisha na hoja ya uuzaji wa nyumba za serikali.Ulizia ni kikao kipi kiliamua. Omba na orodha ya wajumbe wa kikao hicho.
 
Pambaf. Tanzania tunamuhitaji Magufuli. Baba ritz kapiga pesa sana bila huruma na kuiacha nchi mufilisi. Ili TZ izaliwe upya tunamuhitaji mkereketwa Magufuli.

Unaemambia ni mmoja kati ya watoto kama sio wajomba wa baba Ritz. Hapa analeta kilio cha msiba wa Msoga.
 
Kinachonifariji na kunipa nguvu za kuendelea kuandika ni yale maneno yaliyotamkwa na mwandishi maarufu wa vitabu wa zamani wa Marekani, Mark Twain, kwamba andika lakini usiogope shutuma au kulaniwa (write and be condemned). Nitaendelea kuandika kwa kuwa niko tayari kukosolewa, kushutumiwa na kulaaniwa.

Pombe Magufuli ni mtu mwenye maamuzi ya pupa na ya jazba, na hivyo anahitaji mtu wa juu yake mwenye mamlaka zaidi wa kumdhibiti na mtu huyo ni rais! Hebu fikiria mtu wa namna hiyo akiwa yeye mwenyewe ndiyo rais! Hata kwenye zama zake za uwaziri, John Pombe Magufuli hakupata kunisisimua kuwa ni presidential material.

Nimekuwa nikifuatilia utendaji wake kwa muda mrefu, na nadiriki kusema kwamba John Pombe Magufuli ni mchapakazi hodari lakini mwenye kasoro kadhaa kubwa za kufanya maamuzi ya pupa, kuzomoka na kutoa kauli tata hadharani bila kwanza kupima athari zake. Kauli hizo ni kama ile ya kuwaambia wana Kigamboni wapige mbizi kama hawataki kulipa nauli mpya ya kivuko! Kwenye urais hafai; maana anahitaji ufungwa gavana na viongozi wengine wa juu zaidi yake yeye yaani waziri mkuu au rais. Uzoefu unaonyesha kwamba, wakati wa uwaziri wake, kazi hiyo ya kumfunga ?gavana? ilifanywa (si mara moja au mbili) na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda au Rais Kikwete mwenyewe.

Labda nitoe mfano mmoja unaohusu suala lile alilolivalia njuga mwaka 2011 la bomoabomoa ya nyumba zilizowekwa ?X? kwa kujengwa katika maeneo ya hifadhi ya barabara, Itakumbukwa kwamba Magufuli aliielekeza Tanroads kupima barabara zote kuu nchini na kuwekea ?X? nyumba zote zilizojengwa katika eneo la hifadhi ya barabara hizo. Zoezi hilo la kitaifa lilitumia mamilioni ya fedha za walipakodi kulikamilisha. Na lilipokaribia kukamilika ndipo John Pombe Magufuli akaanza vitisho vyake kwa wote ambao waliwekewa nyumba zao ?X?.

Akawapa muda fulani wazibomoe wenyewe; vinginevyo zingebomolewa na matingatinga ya Tanroads bila ulipaji fidia. Waathirika wakaanza kulalamika na kutoa shutuma kibao kwa waziri huyo na serikali. Mfano mwingine wa pili ni wa tukio lile la mgomo ule wa wenye malori ya mizigo baada ya John
Pombe Magufuli kuagiza watozwe asilimia tano kwa kila lori litakalozidisha uzito. Wamiliki hao walikataa, na badala yake wakaamua kugoma.

Wakati mgomo huo ukiendelea, John Pombe Magufuli, akitiwa nguvu na sheria kuhusu tozo hiyo mpya, akatamba lazima wenye malori walipe tozo hiyo, na kama hawataki, wayaondoe malori yao barabarani na kuyaegesha majumbani mwao! Japo kweli tozo hiyo ipo kisheria, John Pombe Magufuli hakufikiria athari za kiuchumi kwa taifa kutekeleza agizo lake hilo kibabe. Baada ya mgomo wa wenye malori kuendelea kwa siku kadhaa na kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya pesa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akaingilia kati na kumpiga stopJohn Pombe Magufuli kwa kusitisha ulipaji wa tozo hiyo ya asilimia tano, na pia kuagiza pande mbili zikae chini kutafuta mwafaka - jambo ambalo Magufuli alilikataa mwanzoni.

Baada ya agizo hilo la Waziri Mkuu, mbwembwe, vitisho na jazba alizokuwanazo John Pombe Magufuli kuhusu tozo na mgomo huo wa wenye malori vikayeyuka haraka kama liyeyukavyo pande la barafu ukiliweka kwenye jua kali! Huyo ndiye John Pombe Magufuli mtu ambaye CCM imemuona ndiye anayefaa kuwa rais wetu mpya.

Na hapo, bado sijazungumzia kabisa mambo yake mengine yenye utata kama vile uamuzi wa kuuza nyumba za serikali na ule ya kukamata meli ya
samaki ya kichina bila utafiti wa kutosha au hata suala la uwezo wake mdogo wa kuleta mageuzi ya maana (reforms) ndani ya CCM.

si bure wewe umetimbuliwa ndo maana una majungu na hakuna point hapo.watanzania wanamuhitaji huyo acha afanye kazi tuliyo mtuma
 
Umepokwa ugali sio na vijisafari vya nje hakuna pia inawezekana ulinufaika sana kifisadi awamu iliyopita sass hela zimepotea na hata kukufanya ushindwe kwenda sehemu za starehe ulizozoea shame on you.
 
Back
Top Bottom